Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 533
- 1,499
Oya, huku mtaani hali ni tete kinoma! Hivi hawa wakubwa wanachukulia watu ni mazuzu au? Mlipiga kelele watu "wajiajiri," vijana tukajichanganya tukaingia kwenye mchaka wa kufungua makampuni ya utalii (tour companies). Tukaingia kichwa kichwa, tukauza hadi viwanja na kukopa mapesa ili tu tusake tonge kupitia utalii.
Lakini leo hii, mbona kama mnatupiga "tobo"? Kila siku mnazuka na tozo mpya na kodi za kijinga ambazo hazina kichwa wala miguu. Mnajifanya mnatangaza utalii kwa mbwembwe huko nje, wakati huku ndani "Field" mmepafanya kuwa kuzimu. Mnatukamua kodi kama vile tunachimba dhahabu, kumbe tunasotea watalii ambao wenyewe wanakimbilia nchi jirani maana huku kwetu bei zimekuwa za kichawi!
Rais na timu yako, acheni "uswahili" kwenye biashara za watu. Hawa wamiliki wa makampuni ya tour mliowaambia wajiajiri, leo hii wanapumulia mipira ya redio! Wanaishi maisha ya kihuni, wanadaiwa kila kona, huku nyie mkizidi kuwapiga mapingu ya kodi. Huu mchezo mnaoucheza ni wa "Kichina" sana; mnaua soko, mnamuua mzawa, alafu mnasubiri sifa za kipuuzi.
Acheni kutuzingua! Kama mmeamua kuua huu mchongo wa utalii kwa ajili ya washikaji zenu na makampuni ya nje, semeni tujue moja. Sio kutupiga fix za "kujiajiri" wakati mnatupangia mazingira ya kufilisika mchana kweupe. Huu ni uhuni wa kiwango cha lami!
Je, wadau mtaani hali ikoje? Au ni mimi tu naona huu uozo?