Awamu ya Sita inaendeleza tabia ya kuitenga mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kusini

Awamu ya Sita inaendeleza tabia ya kuitenga mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kusini

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Salamu kwenu.

Naona viongozi wa awamu ya 6 wanaendelea na tabia ya kuitenga mikoa ya Kusini kwenye maeneo mengi tu.

Chief Hangaya yeye amejikita Dodoma, Kanda ya Ziwa, Dar, Kanda ya Kaskazini na Zanzibar.

Mwisho wa mwaka Rais alikuwa awe mgeni Rasmi Siku ya Ukimwi Duniani na hakuja, hakuna sababu zilitolewa.

Kanda nilizotaja hapo juu wanarudia mara mbili mbili, hii tabia inaonyesha wazi kabisa kwamba hata kwenye mgawanyo wa miradi ya maana hawajengi huku Kusini ndio maana hawaoni haja ya kuja.

Tuna miradi mingo tuu ilishakwama Miaka na Miaka kama Liganga na mchuchuma, uwanja wa Songwe, barabara kibao tuu za kuunganisha Mkoa na Mkoa Bado mavumbi, Southern Circuit ya Utalii ilishatelekezwa, Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya Udsm Mbeya wametelekeza kwa kisingizio cha kukosa Ardhi, Tazara nk.

Mkoa wa Ruvuma kwa mfano haijaunganishwa na barabara yeyote ya maana na nchi jirani wala Ziwa Nyasa hakuna meli ya abiria.

Ikiwa Hawa wa awamu ya 6 nao wameamua kuwa kama awamu ya 5 ni vyema watu wa Kusini tuamue kutembea na Upinzani ijulikane moja.

Kanda ya Kusini/ Nyanda za Juu Kusini iko namba 3 kuchangia Pato laTaifa ambalo linawanufaisha wengine, hii sio sawa. Ona hapa Rais anaenda Tena Kaskazini wakati katoka huko si zaidi ya miezi 2👇

Kilimanjaro.jpg
 
Hii ni kweli kabisa kila kitu kanda ya ziwa na kaskazini angalia Tazara ilivyotelekezwa, ukienda ofisi zake kama magofu, vyoo katika hali mbaya nadhani inatakiwa kuwe na uwiano wa miradi ya maendeleo hata kutembelewa na viongozi wakuu wa nchi kwani ndio njia nzuri ya kutatua kero za wananchi kwa usawa sio kila kitu mwanza tu
 
Hii ni kweli kabisa kila kitu kanda ya ziwa na kaskazini angalia Tazara ilivyotelekezwa , ukienda ofisi zake kama magofu, vyoo katika hali mbaya nadhani inatakiwa kuwe na uwiano wa miradi ya maendeleo hata kutembelewa na viongozi wakuu wa nchi kwani ndio njia nzuri ya kutatua kero za wananchi kwa usawa sio kila kitu mwanza tu
Hatuna chetu kwa CCM, tufanye kitu 2025
 
Mkuu Kwanza hongera Sana kwa kuliona hili

MKOA WA RUVUMA n mkoa ambao haujaunganushwa kabisa na nchi jiran

Na boarder pekee za kuunganisha nchi hiz jiran n mbambabay ..nyasa ambako hakuna meli ya uhakika kabisa

Pili boarder ya MPITIMBI..MUHUKURU MITOMONI.hii inaunganisha nchi ya msumbiji

Nadhan ndyo mkoa pekee hapa nchini haujaunganishwa kabisa na nchi za jirani

JENISTER MHAGAMA najua upo humu na ushanitisha sana juu ya mabandiko yangu yanayohusu mkoa wa Ruvuma kupitia watu wako ukwel utabaki kuwa ukweli wewe ndye mbunge mbovu kupita wote kutokea miundombinu n ya hovyo Sana

Tunaomba Sana serikali itusaidie jaman huu mkoa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kiasi kikubwa, ulichoandika ni sahihi. Viongozi wa kitaifa hawaendi mikoa ya Kusini wala Nyanda za Juu Kusini kwa sababu hakuna miradi mikubwa ya maana inayoendelea huko licha ya ukweli kwamba mikoa hiyo inachangia kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa.

Chuki za awamu ya 5 kutokana na watu wa Mbeya na Njombe kutamka wazi mwaka 2015 kuwa wasingeichagua CCM, kulimfanya marehemu kutafuta namna ya kulipiza kisasi baada ya kuwa Rais. Baada ya hapo watu wa maeneo haya wakazidi kuichukia CCM na mgombea wake wa Urais mwaka 2020.

Njombe ndiyo eneo pekee Marehemu Magufuli alilazimika kupiga magoti wakati wa kuomba kura. Kinachoendelea sasa kitazidi kuchochea mikoa hii kuzidi kuichukia CCM, na CCM ili kuendelea kuyashikilia majimbo ya maeneo haya watalazimika kuendelea kutegemea uporaji wa kura na hadaa mbalimbali, na siyo kura za wananchi.
 
Salama , nlipotea sana humu nilikuwa na
Salamu kwenu.

Naona viongozi wa awamu ya 6 wanaendelea na tabia ya kuitenga mikoa ya Kusini kwenye maeneo mengi tuu...
case clearance sana na ndio maana nimepotea sana.

sasa nitakupeni siri, SAMIA anajaribu kuwaomba msamamaha wachagga kwa anachofanyiwa MBOWE, kumbuka kesi ya mbowe iliandaliwa na MAKONDA NA JIWE, kuifuta hawawezi wanasubiri uamuzi, WANAKWENDA KILIMANJARO KUJIPENDEKEZA KWA machifu
 
Tatizo nyie mnajifanyaga wanaharakati kama Sugu! Ila kiuhalisia bado hamjafikia level ya Serikali kuwaona tishio! Acheni ujuaaji! Watu walio waangusha ni akina Mwandosya!
Kwa kiasi kikubwa, ulichoandika ni sahihi. Viongozi wa kitaifa hawaendi mikoa ya Kusini wala Nyanda za Juu Kusini kwa sababu hakuna miradi mikubwa ya maana inayoendelea huko licha ya ukweli kwamba mikoa hiyo inachangia kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa...
 
Nimeandika kwa jazba hadi nimekosea heading
kwani hujui kwa nn wanapenda kwenda huko?ndo ngome za upinzani na ndo mtaji wao wamccm kupata kura kwa kuwa mikoa hiyo ina idadi kubwa ya watu pia ina watu ambao ni critics.kusini na ss tujenge ngome zetu ili kuilazimisha serikali iwekeze kwetu sababu tunachangia sana katika pato la taifa vinginevyo tuanzishe tudai serikali za majimbo.
 
Back
Top Bottom