Awamu ya Sita inaendeleza tabia ya kuitenga mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Kusini

Naam acha jazba kuandika uchochezi
Wala hakuna uchochezi, watawala waikumbuke Kusini. Hongera MH Kassim Majaliwa kwa kuwa Mstari wa mbele kwote upo. Mikoa ya Kusini hata tuviwanda twa kuchakata sembe hamna. Mtwara gas walipiga bomba mchuchuma chali hadi leo. Kimsingi watawala wakisikia wakumbuke. Mama Karibu kusini utusalimie 2025 yaja.
 
Kumbe ukweli anaujua...

Kagera pamoja na kuwa na GDP per Capita ndogo kadri ya BOT...lakin ni mpaka mmoja tu wa huko kyerwa hauna lami...
Na wilaya zote zimeunganishwa na lami. Na sasa Hadi baadhi ya vijiji potential vinaunganishwa na lami.
Uwanja wa ndege uko busy
Meli ya mv Victoria inafanya kazi na imekarabatiwa....na Kuna mpya inajengwa.
Bandari zote zimekarabatiwa bukoba na kemondo...

Wakazi wake wanajenga nyumba Bora vijijini.


Halafu mtu anasema Ruvuma sijui njombe wakati Bado umaskini umetamalaki

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Kwenda Makete kuna lami ni kweli, ila kwenda Ludewa, mziki bado sana mkuu. Wameruka ruka sana. Ila barabara toka Mbinga kwenda Mbamba Bay imejengwa vizuri, hapa tuwe wakweli, kazi imefanyika hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…