Awamu ya sita si awamu ya tano, hongera mama Samia

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana inatia moyo kuwa tuna mwanzo mpya. Katika awamu ya 6:

1. Urasimu uliokuwapo sasa unapigwa vita.
2. Upigaji mkubwa wa pesa uliokuwapo unapigwa vita.
3. Ugonjwa wa Corona uliopo sasa unakabidhiwa tume ya wataalamu waliobobea kwa ajili ya kushauri nini cha kufanya.
4. Tunatambua sasa umuhimu wa wakezaji kwamba tunawahitaji zaidi wawekezaji kuliko wanavyotuhitaji wao.
5. Tunawahitaji wengine kwenye mashirikiano ya kimataifa ili kuweza kufika mbali zaidi.
6. Kodi ya dhuluma haihitajiki.
7. Nk nk yakiwamo ajira, mzunguko wa pesa, masoko yakiwamo ya mazao nje.

Wandugu mwanzo huu ni mwema asiyeuona hivyo na aendelee kutokuuona.

Cc: Mjingamimi, Johnthebaptist na wale wenzetu na sisi.

Hiiiiii!
 
Mama atumbue wateule wote wanaopuuza maelekezo yake, ni dharau
Na atawatumbua kwelikweli bila huruma. Kuna watu wamepewa second chances ila wanaona aibu na fedheha kutenda kinyume na misimamo waliyoiishi enzi za JPM (Abass et al). Ukiiangalia body language ya PM, unaona kabisa huyu mtu yupo tortured kisaikolojia.

Mama keshadeclare. Ukimzingua, mnazinguana. Infact ukimzingua Mama, utazinguliwa wewe 10X

Bora PM, mie mapozi ya Ndugai tangu mama ashike usikani siyaelewi yaani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yaani yuko kama mtoto wa kufikiaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
PM angejiuzulu tu. Kwamba kodi hata hili la kodi tu kuwa kulishamiri hata kodi za dhuluma na walikuwapo?

Wajameni wanasubiria nini watendaji hawa ambao hawakuwa wanawatendea haki wananchi?

Hivi hawa kazi inapoendelea wana nini kipya cha kituambia?

Hiiiiii!
 
3. Ugonjwa wa Corona uliopo sasa unakabidhiwa tume ya wataalamu waliobobea kwa ajili ya kushauri nini cha kufanya.
Hii Tume iondoke na wale Mawaziri mzigo wa Afya na Nyungu
 
Bango moja linaondoka na DED au RC.
 
Hivi shost yangu mama D yupo kweli??? Maana sijamuona kabisa kwa siku mbili hizi?? Au bado anaugulia maumivu chato?πŸ˜„

Nimejaa tele lord denning
Si unajua shughuli ya jana ikuluπŸ˜πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‘
 
Nimefurahi sana leo nimekuona my dear! Nilikumiss πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Nami pia Lord denning, mimi nilikumiss sana tangu october 28
Tujenge nchi yetu Tanzania ndio baba na mama
 
Nami pia Lord denning, mimi nilikumiss sana tangu october 28
Tujenge nchi yetu Tanzania ndio baba na mama
Tunaijenga nchi yetu vizuri sana chini ya Jemedari wetu Samia Suluhu HassanπŸ˜€πŸ˜€. Au unateseka dear?πŸ˜ƒ
 
Jana nimemsikia Mzee mmoja wa Kiarabu akisema Samiha... halafu akaanza kusoma dua nikamuuliza kulikoni akaniambia kuwa kafilisiwa kwa sababu ya kuwakodishia nyumba yake wana CUF nilisikitika sana
 
Jana nimemsikia Mzee mmoja wa Kiarabu akisema Samiha... halafu akaanza kusoma dua nikamuuliza kulikoni akaniambia kuwa kafilisiwa kwa sababu ya kuwakodishia nyumba yake wana CUF nilisikitika sana
kwahyo alikua anamuombea nini Rais wetu kipenz
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Tunaijenga nchi yetu vizuri sana chini ya Jemedari wetu Samia Suluhu HassanπŸ˜€πŸ˜€. Au unateseka dear?πŸ˜ƒ
Huo ndio uzuri wa kuwa na chama imara. Resources za kutosha zilizo katika ubora wa hali ya juu

CCM wamejipanga vilivyo..... Hakunaga kuteseka

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Ironlady Samia Suluhu HassanπŸ˜πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…