Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Uache siasa za changa la macho, Serikali ya JPM ndiyo imeua utendaji wa UDART.
Barabara za UDART kweli ni mali ya serikali lakini mradi wa mabasi mwendo kasi ulikuwa toka mwanzo ni mradi binafsi (private investment) uliowekezwa na mtanzania, Nd Kisenha.
Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane kulipa kodi.
Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.
Hii ingewezesha huduma iendelee, biashara iendelee na kodi ilipwe. Hili ni kosa, maana serikali haikuwa na msaada wowote kwa muwekezaji.
Pili, tunasikia tetesi kuwa sasa UDART ni mali ya Serikali maana baada ya Nd Kusenha kufunguliwa madai ya Uhujumu uchumi, kwawaida ya modus operadi ya Awamu ya 5kwa wafanyabiashara, serikali imejimilikisha uendeshaji.
Serikali zote toka Awamu ya kwanza hadi nafikiri Mwinyi (miaka zaidi ya33) mfupa wa DMT (Dra es Salaam Motor Transport) na UDA (Usafiri Dar es Salaam), ziliwashinda.
Sasa sijui Awamu ya 5 ndio wangeweza Kuendesha UDART?
Mbaya zaidi serikali inaua moyo wa wazalendo kuingia miradi mikubwa kiuwekezaji, kinyume cha wanachoongea majukwaani. Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa UDART kweli sioni mantiki yake zaidi ya kusema Serikali imachukua na kuanza mradi huu on a false start.
Sana sana ni kujikosha kwa wananchi kwa failures za serikali yenyewe, kusaidia wazalendo kuwekeza nchini mwao.