Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Kwakweli inafikirisha sana. Jinsi Magufuli alivyojipambanua kulinda mali za umma akateua wazalendo kila mahali na sasa haya ndio matokeo kila mradi. Hii ngozi kweli imelaaniwa.
Tatizo si ngozi , ni akili au short of.
Watu wengi wasio na akili hufikiri wale wenye madaraka ndio wanaweza kuendesha biashara, mfano huo sasa, UDART imefeli mikononi mwao.

Somo la kufeli DMT na UDA wala halikuwaingia kichwani
 
Hili jambo mimi nilishindwa kabisa kulielewa, vifaa ambavyo vinaenda kusaidia wananchi serikali inagoma kabisa kuvitoa! Sasa walipata faida gani? Kodi hawajapata, wananchi huduma hawajapata. Si wangeweka special agreements, kila siku 50pc ya revenue iende kulipa kodi, how difficult was that! Watanzania hatujui ni namna gani Mungu ametuokoa na lile jitu.

Na huu ujinga wa BRT Phase 1 ndio umetunyima pesa ya Phase II na III, World Bank waligoma kutoa pesa tena. Maana hii ya kwanza tumechemka.
Mkuu kuna watu serikalini wana vichwa vigumu sana.
Siyo bure mzee Assad amesema 60% ya wafanyakazi serikalini vichwa ni calas!
They cant think around a problem.
 
Nooo! Not genius! Totally human level quality! Kama huna quality hizo, I am sorry! Jitahidi uinuke. Ndo umuhimu wa JF na mijadala yetu.
Shida sio mjadala, shida ni kujadili kitu ambacho msingi wake hujaelewa. My original post had nothing to do na kuchezea mali za serikali, you're way off the mark
 
Huwezi kumtoa mwekezaji na kuvunja mkataba kama huna vigezo. Mwisho wa siku serikali itashitakiwa na kumlipa fidia mwekezaji kitu ambacho ni hasara kwa mlipa kodi. Dawa ni kumbana mwekezaji atimize wajibu wake, kama akishindwa ndio unapata sababu ya kuufuta mkataba.
Unafahamu kuwa huu mradi unaendeshwa na Serikali kwa amri ya Sadist Jiwe?
IMG-20210420-WA0099.jpg
 
Magu kwa UDART alibugi,hata pale wananchi walipopaza sauti hakujali.
Kwanini Waziri Mkuu anakuja sasa wakati shirika limeishateketea?
Uza UDART wanaume wa shoka wafanye kazi.
 
Magu kwa UDART alibugi,hata pale wananchi walipopaza sauti hakujali.
Kwanini Waziri Mkuu anakuja sasa wakati shirika limeishateketea?
Uza UDART wanaume wa shoka wafanye kazi.
60% ni shida.
Serikali ikiling'ang'ania hilo shirika litakufa kabisa.
 
Unafahamu kuwa huu mradi unaendeshwa na Serikali kwa amri ya Sadist Jiwe?View attachment 1758663
Hiyo inahusiana nini na kuondoa au kuharibika kwa mfumo wa ukataji wa ticket kwa njia ya electronic? Unajua nyie tatizo lenu mnapenda kuchanganya vitu kwa kutojua nani anaye wajibika. Mnataka ubepari kwa fikra za kijamaa.

Naomba nikuulize swali, waziri mkuu alihoji nini kwenye dirisha la ukataji wa Tickets? Na alibaini nini? Sasa nani anasimamia mfumo mzima wa utoaji Tickets, Rais?

Ndiyo mashirika mengi ya serikali yapo chini ya offisi ya Rais, lakini wasimamizi sio Rais peke yake kuna wasaidizi wake ambao ni watendaji wa serikali akiwemo, Waziri mkuu, waziri anaye husika wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano, Mayor na wakuu wa mikoa kwenye mikoa amabazo hayo mashirika yako, wakurugenzi wakuu na Board of directors kama wapo. Na kwenye Board of directors waziri mkuu na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano na hata Mayor wa jiji na mkuu wa mkoa si wanakuwa wapo? (Naomba mnisahihishe kama niko wrong)

Hawa members of the Board of directors mara kwa mara wana vikao vya kuangalia mwenendo wa shirika, mara nyingi inakuwa quarterly. Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa kwenye vikao vyao hawakuweza kubaini uchafu huu uliotokea? If that's the case, kwanini waziri mkuu haku-react mapema? Hiyo mimi naona ni uzembe wao wa kutojua majukumu yao.

Kwa uelewa wangu Rais anaweza akalaumiwa kwa kuwateua watendaji ambao ni vichaka kama huyu mkurugenzi mkuu, lakini sio katika uendeshaji wa shirika.
 
Toka lini serikali ikaendesha mradi ukaleta faida? Watu wanasema sio mradi wa baba zao
 
Back
Top Bottom