Udart sasa nao wapo kwenye kutumikia karma ya maxcom na karma ya kudhulumu wafanyakazi stahiki zao ikiwemo mafao.
Ukweli hawa watendaji wasio na ujuzi na mambo ya magari ni tatizo sana kwa taasisi nyingi + ukabila uliokuwa umetamalaki kwenye huo mradi ni lazima haya yajitokeze, management iliyoshindwa kuendesha daladala zilizopewa njia bila mshindani kule mnazi mmoja kivukoni na baadae kwenye huu mradi kamwe hawakustahili kupewa hiyo nafasi, maana waliwaletea figisu maxcom wanawaibia pesa wakatolewa wakaanza kukusanya wao Pesa majumbani kwa watu na mifukoni, TTCL Sijui kitu gani kiliwashinda kirejesha mfumo kama ule wa awali wa maxcom, haiingii akilini Mashine za Ku swap kadi na ticket zipo na zimeagizwa kwa Pesa nyingi, cha kuzisimamisha kwa miaka mitatu ni hujuma kubwa sana hii.
Ukirudi kwa wafanyakazi waliomaliza mikataba wengi wao mafao yao na hata michango yao ya kila mwezi haikupelekwa hii pia ni uzembe au kuna watu walikuwa wananufaika na ucheleweshwaji wa kupelekwa kwa michango kwenye mifuko husika.
Miaka mitano sasa ni aibu mradi ule wa mabilioni kushindwa kujiendesha kwa faida na inasikitisha wao mishahara haikosekani ila faida na malipo kwa wastaafu hakuna.
Nitarudi baadae mjukuu wangu analilia simu.