Inaonekana huna hata ABC ya biashara. Unafahamu aliwekeza kiasi gani? Profit margin projections ilikuwa kiasi gani? Na alipoanza kuuendesha mradi, kulikuwa na tofauti gani kati ya projections na mapato halisi?Haha, uzi wako ulikuwa sio wa kuongelea matatizo ya mwendo kasi ila ni kunyoosha vidole utawala wa awamu ya tano.
Kama mwekezaji alikuwa anajuwa kigezo chake ni faida, kwanini alitaka kwenda kinyume na mkataba kwa kupandisha nauli wakati hakuna viashiria vyovyote vilivyo support upandishaji wa nauli? Bei ya mafuta ilikuwa ile ile, thamani ya shilingi haikubadilika sana, mfumuko wa bei ulikuwa unazidi kushuka, maishahara haikupanda. Kama sio ulafi na ubinafsi ni nini?
Unapotaka kuanzisha mradi, kuna projections za gharama za uwekezaji, uendeshaji na mapato. Mradi ukianza, unakutana na uhalisia. Yawezekana kwenye uhalisia, gharama halisi za uendeshaji na mapato halisi ya biashara, vikawa na tofauti kubwa na projections. Lazima ufanye review. Na kwenye review, kuna items ambazo utakuwa huna uwezo wa kuzibadili, kama vile bei ya mafuta, kodi, bei za vipuli, n.k. Hivyo unabakia na maeneo machache sana ya kufanyia marekebisho, zaidi ni kwenye nauli.
Huwezi kusema hakukuwa na mabadiliko ya gharama wakati hujui kama toka mwanzo alikuwa anaendesha kwa faida au hasara.