Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Awamu ya Tano iliua UDART, hili tuliseme wazi si kumung'unya maneno

Kisena yule Fisadi! Enzi za JK alikuwa na nguvu hatari,aliwahi kumpiga OCD wa Maswa mtama lol.huyu atakuwa alikamatwa kwa uhalali.
Uko sahihi. Serikali ilikuwa sahihi sana kutafuta pesa yake iliyochotwa na mtu kama huyu kwa urafiki tu na rais. Akaachiwa eti naye akajiita mfanyabiashara.
Kuna mengi ya kuipa sifa awamu ya 5, badala ya kubeza.
 
You must be crazy and misinformed! Usijiandikie tu! Haya ndo yanayochotwa na wabunge na baadhi ya wana JF wasiokuwa na uelewa na kuwapotosha.
Hapakuwa na mwekezaji mwenye mtaji bali mtu tapeli na mwizi. Serikali ilidai hisa zake na zile za jiji. Iliidai UDA yake iliyochotwa kitapeli, sasa ulitaka aachiwe wizi wa wazi? Andikeni kama wenye uelewa na siyo mashabiki wa watu washenzi tu!
Mawazo ya kimaskini kabisa haya! Serikali sio mwizi imeleta tija gani na kama huyo alietaka kuchukua alikuwa mwizi kwanini Serikali ilishindwa kutafuta mwekezaji mwingine

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kujiuliza kwanini hiyo kampuni haipo, ila nimejiuliza sana ni kina nani walikuwa nyuma ya hiyo kampuni.
MaxMalipo ni sehemu ya ufisadi wa wakuu waliokuwa Benki kuu miaka hiyo. Akina Idrissa. Wakajidai kumuweka huyo Max kama mbunifu. Ila kwa ujumla imesaidia mambo ya e-commerce sana.
 
Uache siasa za changa la macho, Serikali ya JPM ndiyo imeua utendaji wa UDART.

Barabara za UDART kweli ni mali ya serikali lakini mradi wa mabasi mwendo kasi ulikuwa toka mwanzo ni mradi binafsi (private investment) uliowekezwa na mtanzania, Nd Kisenha.

Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane kulipa kodi.

Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.

Hii ingewezesha huduma iendelee, biashara iendelee na kodi ilipwe. Hili ni kosa, maana serikali haikuwa na msaada wowote kwa muwekezaji.

Pili, tunasikia tetesi kuwa sasa UDART ni mali ya Serikali maana baada ya Nd Kusenha kufunguliwa madai ya Uhujumu uchumi, kwawaida ya modus operadi ya Awamu ya 5kwa wafanyabiashara, serikali imejimilikisha uendeshaji.

Serikali zote toka Awamu ya kwanza hadi nafikiri Mwinyi (miaka zaidi ya33) mfupa wa DMT (Dra es Salaam Motor Transport) na UDA (Usafiri Dar es Salaam), ziliwashinda.

Sasa sijui Awamu ya 5 ndio wangeweza Kuendesha UDART?

Mbaya zaidi serikali inaua moyo wa wazalendo kuingia miradi mikubwa kiuwekezaji, kinyume cha wanachoongea majukwaani. Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa UDART kweli sioni mantiki yake zaidi ya kusema Serikali imachukua na kuanza mradi huu on a false start.

Sana sana ni kujikosha kwa wananchi kwa failures za serikali yenyewe, kusaidia wazalendo kuwekeza nchini mwao.
Uzuri sisi wengine tupo humu JF kitambo na akili zetu ni zile zile hatuendi na upepo. Soma huu uzi na comments zake alafu umpe JPM heshima yake.

Sijawahi kujiuliza kwanini hiyo kampuni haipo, ila nimejiuliza sana ni kina nani walikuwa nyuma ya hiyo kampuni.
 
Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane kulipa kodi.

Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.
Hili jambo mimi nilishindwa kabisa kulielewa, vifaa ambavyo vinaenda kusaidia wananchi serikali inagoma kabisa kuvitoa! Sasa walipata faida gani? Kodi hawajapata, wananchi huduma hawajapata. Si wangeweka special agreements, kila siku 50pc ya revenue iende kulipa kodi, how difficult was that! Watanzania hatujui ni namna gani Mungu ametuokoa na lile jitu.

Na huu ujinga wa BRT Phase 1 ndio umetunyima pesa ya Phase II na III, World Bank waligoma kutoa pesa tena. Maana hii ya kwanza tumechemka.
 
Serikali haiwezi kufanya biashara ndiyo maana hata ATCL ni hasara tupu pamoja na majigambo yooote ya mwendazake
Sasa hivi Serikali ndio inaendesha UDART badala ya muwekezaji aliyeondolewa kihuni.

Mfupa wa DMT na UDA uliishinda serikali, huu wa kisasa wa UDART ndio kabisa imejaribisha ulaji wa mameneja na wafanyakazi wake.
Hakuna cha ajabu hapo, serikali awamu iliyopita ilivurunda.
 
Kwa hiyo magu akaamua kumkomoa sio?
Acheni porojo someni huu uzi, msifikiri mambo mengi nchi hii ni mapya. Uzuri mengi yametokea technology tayari ipo juu.

Uache siasa za changa la macho, Serikali ya JPM ndiyo imeua utendaji wa UDART.

Barabara za UDART kweli ni mali ya serikali lakini mradi wa mabasi mwendo kasi ulikuwa toka mwanzo ni mradi binafsi (private investment) uliowekezwa na mtanzania, Nd Kisenha.

Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane kulipa kodi.

Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.

Hii ingewezesha huduma iendelee, biashara iendelee na kodi ilipwe. Hili ni kosa, maana serikali haikuwa na msaada wowote kwa muwekezaji.

Pili, tunasikia tetesi kuwa sasa UDART ni mali ya Serikali maana baada ya Nd Kusenha kufunguliwa madai ya Uhujumu uchumi, kwawaida ya modus operadi ya Awamu ya 5kwa wafanyabiashara, serikali imejimilikisha uendeshaji.

Serikali zote toka Awamu ya kwanza hadi nafikiri Mwinyi (miaka zaidi ya33) mfupa wa DMT (Dra es Salaam Motor Transport) na UDA (Usafiri Dar es Salaam), ziliwashinda.

Sasa sijui Awamu ya 5 ndio wangeweza Kuendesha UDART?

Mbaya zaidi serikali inaua moyo wa wazalendo kuingia miradi mikubwa kiuwekezaji, kinyume cha wanachoongea majukwaani. Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa UDART kweli sioni mantiki yake zaidi ya kusema Serikali imachukua na kuanza mradi huu on a false start.

Sana sana ni kujikosha kwa wananchi kwa failures za serikali yenyewe, kusaidia wazalendo kuwekeza nchini mwao.
Robert Kisena yuko jela mke wake yuko jela, buses 70 ziko tra, mkurugenzi wa fedha umemfukuza kazi, unasema mkajadiliane na tra kuhusu nini? hivi mumekuwaje? ndio maana ngosha alikuwa anawatukana pumbavu, mumwachie Kisena aje aendeleze shirika lake alipe na kodi aajiri watu aboreshe usafiri, hivi kweli ceo wa udart angekuwa mmarekani mngemfanyia haya?
 
Nani yuko kwenye hiyo Kampuni sio issue .. issue ni kuhusu performance

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Sina uhakika kama performance yao iko juu au chini, maybe you can explain more.

Nachojua mimi sera ya Tanzania ikija kwenye private sector, hakuna sekta itakuwa dominat player. Baadhi ya kampuni za simu wamejaribu kutumia mabavu na kuwa dominant lakini wameshindwa, kama Maxmalipo walidhani wanaweza kuliteka soko, itabidi wajipange upya. Hata mwendo kasi pia, makampuni mengine yanajipanga kujiingiza kwenye biashara.
 
Nilikuwa siamini kwamba kwenye kila analogusa Magufuli huwa ana haribu Ila kwenye Mwendokasi ndo sehemu niliyokuja kuamini kwa Mara ya kwanza!

Kwanza inabidi wote tujiulize mwendokasi ilianzia wapi?

Mradi wa mabasi ya mwendokasi ukianzishwa na kuasisiwa na Rais wa Awamu ya nne. Kwa Jinsi mradi ulivyokuwa umeandaliwa ulitakiwa kusimamiwa na kampuni binafsi na tangu mwanzo ulisimamiwa kwenye mfumo huo. Mradi huu ulikuwa chini ya Kampuni na Kisena na wakati unaanza kila kitu kilikuwa kinaendeshwa katika dunia ya kisasa. Ticket zilikatwa kielectronic na watu waliweka hadi kuwa na kadi ya kutumia mwezi mzima.

Alipokuja Magufuli kwanza alianza ku deal na kisena kwa sababu kisena hakuwa kwenye kundi la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Alimtesa kisena kumpa kesi za uhujumu uchumi na mkewe na baadae kumnyang’anya mradi na hatimaye akaondoa utaratibu wote mzuri uliokuwa umewekwa kwa ajiri ya kuendesha mradi.

Matokeo yake akawapa wanajeshi, na hapo ndo Tatizo lilipoanza. Mradi ulianza kuendeshwa kwa tabia za kiswahili na watu wakaanza kukata ticket kama daladala.

Mradi huu hadi kufikia sasa ulitakiwa uwe umeshaanza kujiendesha kwa faida Ila kwa roho mbaya ya magufuli na tabia zake za kuchukia matajiri ndo amefanya mradi ule uwe kituko na usifike popote.

Polee kisena. Buriani Mwendokasi.
Ukiyaangalia haya yote, hakika utawala wa Hayati Magufuli umeleta hasara zaidi kuliko faida. Ni machache mno mazuri ya kuyaendeleza kutoka kwenye utawala wa awamu ya 5.

Itachukua miaka zaidi ya 10 kuondoa athari mbaya zilizosababishwa na utawala wa awamu ya 5.
 
Mwekezaji alikuwa sio mtu wa kuaminika, ana makado-kando mengi sana tokea alivyokuwa Mwanza. Hata kupata huo miradi aliupata kimagumashi maana hajawahi kuendesha miradi kama huo popote pale duniani. Kwanza tatizo lilikuwa kwenye upangaji wa nauli ambapo yeye alitaka iwe juu zaidi, serikali ikamkatalia kupandisha nauli. Akaona apunguze mabasi kwa kusingizia mabovu ili asitumie gharama kubwa kuyaendesha na alinde mgao wake, kitu ambacho ni kinyume na dhana ya miradi huo. Matokeo yake, uhaba wa mabasi uliongezeka, abiria kujazana kwenye mabasi na mwisho watu kuyasusa kurudi kutumia magari yao.

Lakini tokea 2015, awamu ya tano imejaribu kutafuta wawekezaji wanaoelewa maswala ya usafirishaji mijini, lakini kila mwekezaji anayekuja anakutana na Madudu ya uzembe, anakimbia. Ili kupata mwekezaji mwenye nia, lazima serikali wasafishe wahuni wote waliokuwa kwenye miradi huo na kurudisha shirika kwenye hadhi ya kubinafshwa.
Inawezekana ni kweli mwekezaji alikuwa na matatizo, lakini kwa uhakika Serikali ilikuwa na matatizo makubwa zaidi kwa sababu haikuwa inaelewa kabisa inachofabya na athari zake.
 
Robert Kisena yuko jela mke wake yuko jela, buses 70 ziko tra, mkurugenzi wa fedha umemfukuza kazi, unasema mkajadiliane na tra kuhusu nini? hivi mumekuwaje? ndio maana ngosha alikuwa anawatukana pumbavu, mumwachie Kisena aje aendeleze shirika lake alipe na kodi aajiri watu aboreshe usafiri, hivi kweli ceo wa udart angekuwa mmarekani mngemfanyia haya?
Naona hata Amerika huijui! Angekuwa Mmarekani ktk awamu ya 2, 3, na 4 angepeta tu si wapo waliokuja na suti na wakaondoka na utajili? Mmarekani ktk awamu ya 5 au Mmarekani akiwa amerika hawezi kujitutumua kwa upuuzi kama wa Kisena unayemtaja. Amerika angefilisiwa na kufungwa, no nonsense!

Unawezaje kujimilikisha shirika la umma bila kuangalia mambo ya kisheria yanayokupa nguvu hiyo? Mtu anategemea 'misheni tauni' ili kufanikiwa maisha! Baadaye akibanwa na sheria unaanza oooh Kisena, Ooh mke wake! that is fallacy! Kwanza huyo Kisena ni stupid na foolish kabisa! aliingizaje familia nzima kwenye illegals mama wa watu akajikuta anaingia magereza kwa utapeli wa mume.
 
Kisena aliwekwa kama chambo tu. Ile kampuni ya SIMON GROUP ina wahusika wengi sana wakubwa, akiwepo Profesa Kapuya na Marehemu Idd Simba. Kuna vigogo kadhaa wamo mle. Ukipekua humu JF kuna mada inayoongelea SIMON GROUP, utayaona mengi sana
Hata kama walikuwemo, kuna ubaya gani? Si wawekezaji? Au kuna watu hawaruhusiwi kuwekeza?
 
Inawezekana ni kweli mwekezaji alikuwa na matatizo, lakini kwa uhakika Serikali ilikuwa na matatizo makubwa zaidi kwa sababu haikuwa inaelewa kabisa inachofabya na athari zake.
Kwani kati ya mwekezaji na serikali nani ana madaraka ya kumhukumu mwingine? Unawezaje kulinganisha mtu binafsi na serikali? Yaani mali ya umma inamilikiwa na ka-mtu binafsi halafu unasema kana nafuu!!
 
Back
Top Bottom