Babu yangu alinisimulia kwamba katika kipindi chao, wazungu walikuwa hawawezi kuwaruhusu waswahili kuendesha gari, waliamini mtu mweusi hana uwezo wa kuendesha gari, miaka ilivyozidi kwenda waafrica wakaanza kuendesha gari lakini wazungu walikuwa hawapandi gari yenye dereva wa kiafrika, Leo huu tunarusha dream liners, na wazungu wanazipanda bila kuuliza na wakiwa hewani wanapata usingizi mzito bila wasiwasi.
Niliwahi kusikia kwamba Charles Njonjo, M wanasiasa wa Kenya, alishawahi kusema hawezi kupanda ndege inayorushwa na mtu mweusi, wakati yeye mwenyewe ni mweusi zaidi ya lami mbichi. Hawa wanaopinga uwezo wa watanzania kujenga reli, ni "New edition" ya Charles Njonjo na wenzake.
Tunawahakikishia wa Africa kwamba, Tanzania itakua nchi ya kwanza katika kujenga reli yake na reli za nchi jirani, sio tu kwa kutumia pesa yake, bali hata wataalamu wake. Hiki kimya cha Magufuli kuahirisha uzinduzi wa Kipande cha Isaka to Kigali, alichopanga kuzidua October 2018, unakishinda kikubwa sana, "take my words"