Feasibility studies za BRT, Reli, barabara, madaraja na hata kwenye mawasiliano (rada) kote tumefanya wenyewe. Kuweka mataluma tumekuwa tukifanya wenyewe siku nyingi tuu na hiyo ya kuweka tuta ni civil work ambayo ndiyo taaluma kongwe ya kiuhandisi Tanzania.
Kitu ambacho hatukuwahi kufanya ni teknolojia ya kielektroniki ya kutengeneza njia ya reli (Railway signalling) ambayo baada ya reli hii kukamilika tutakuwa tumepata ujuzi. Kiukweli siyo ujuzi bali ni utundu, haya mambo msingi wake ni mmoja ila ni kubadilisha vitu vidogo vidogo kwa kazi husika.
Kwani unafikiri ujenzi wa reli ni mazingaombwe? Mass, length and time wanazosoma ulaya ndo hizo hizo tulizosoma sisi wamatumbi na ndiyo msingi wa kila kitu.
Bei kubwa mara nyingi sio ubora bali ni saikolojia, watu huamini kitu cha gharama ni bora zaidi na huu ndio msingi wa ubepari (perception). Miaka ya nyuma nilikuwa natengeneza bidhaa fulani (software) nikiuza kati ya $90 -$100. Nikajifunza mahali kuhusu "perceived value" basi nikaongeza bei mara tatu zaidi bila kubadilisha chochote, cha ajabu mauzo yaliongezeka.