Awaudhi Wapenzi wa Liverpool

Awaudhi Wapenzi wa Liverpool

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
Mshambuliaji nyota wa Liverpool, Fernando Torres ameitosa timu hiyo na kujiunga na timu ya Chelsea huku akiacha washabiki wengi wa Liverpool wakiwa na hasira juu yake wengine wakimaliza hasira zao kwa kuzichoma jezi za Liverpool zenye jina lake.
Fernando Torres amekamilisha usajili uliovunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kuitosa Liverpool na kujiunga na vijana wa darajani, Chelsea.

Torres amehamia Chelsea baada ya Liverpool kukubali kumuuza mchezaji huyo nyota kwa kitita kinono cha paundi milioni 50.

Chelsea pia imetumia kitita cha zaidi ya paundi milioni 25 kukamilisha usajili wa mlinzi hodari wa Benfica ya Ureno, David Luiz.

Wakati dirisha dogo la usajili likifungwa, Liverpool imeamua kuzitumia pesa za usajili wa Torres kwa kumsajili mshambuliaji hatari wa Newcastle Andy Carrol kwa usajili uliovunja rekodi ya uhamisho ya Newcastle, paundi milioni 35.

Carrol alipelekwa Liverpool kwa helikopta ili kutia saini mkataba huo.

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere amemtabiria Carrol kuwika zaidi akiwa na jezi ya Liverpool.
 
hahaaa Liverpool bana sa hasira za nini ...
 
toreeeeeees, what a goal by a spaniard! karibu sana darajani tores uje uendeleze vipigo tunavyogawa kwa timu nyingine
 
polen liverpool kupoteza lulu yenu na hongereni chelsea kwa kuinyakua ila mtumieni vizuri msimbemende kama shevchenko!!
 
Back
Top Bottom