Aweso: Maji tumejiweka tayari na Mvua za El-Nino

Aweso: Maji tumejiweka tayari na Mvua za El-Nino

Wizara ya Maji

Govt Institution
Joined
Oct 2, 2024
Posts
34
Reaction score
20
2 (2).jpeg
1 (2).jpeg
Serikali imejipanga na kujidhatiti kuhakikisha miundombinu ya majisafi na majitaka nchini inaendelea kutoa huduma kwa ufanisi kuelekea msimu wa Mvua zilizotabiriwa za El-nino kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA).

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo wakati akikagua miundombinu ya majisafi na majitaka ya Jiji la Dar es salaam ikiwa ni lengo la kuhakikisha serikali ina utayari na tahadhari za mvua za El-nino zinazotarajiwa hivi karibuni.

Waziri Aweso ametembelea Mto Mpiji uliopo Mabwepande eneo linapopita mabomba makubwa ya maji ya inchi 72'" na 54" yanayohudumia asilimia hamsini ya wakazi wa mkoa wa Dar es salaam na mkoa wa Pwani, pia amekagua bohari ya vifaa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kuona utayari na changamoto zozote zitakazojizokeza wakati wa mvua hizo ili wananchi wa Dar es salaam na Pwani waendelee kupata huduma ya maji pamoja na mvua hizo kubwa.

Amekagua miundombinu ya majitaka katika eneo la Mwenge na daraja la Salenda ambapo ameziagiza mamlaka za maji nchini kujidhatiti katika utoaji wa huduma ya maji hasa kuhakikisha madawa ya kutosha ya kutibu maji yapo kuelekea kwenye msimu wa Mvua za El-nino na kuhakikisha miundombinu ya majitaka katika maeneo yao inakua katika hali nzuri ili mvua zisisababishe kuzagaa kwa majitaka mtaani.

Ameridhishwa na maandalizi yanayofanywa na DAWASA kama tahadhari kuelekea kwa msimu wa Mvua za El-nino.
4.jpeg
 

Attachments

  • 1.jpeg
    1.jpeg
    123.4 KB · Views: 13
  • 2.jpeg
    2.jpeg
    143.9 KB · Views: 13
  • 3.jpeg
    3.jpeg
    156.8 KB · Views: 12
  • 4.jpeg
    4.jpeg
    109.8 KB · Views: 12
Wizara ya maji! Fikeni Kata ya Matundasi , Wilaya ya chunya,hakuna maji
 
Wizara ya maji! Fikeni Kata ya Matundasi , Wilaya ya chunya,hakuna maji
Matundasi si ni karibu na lake rukwa? Si kuna msitu wa TFS? Huu ni mwaka 2026 unaamini mtapata? ccm imeshindwa tu kuhakikisha mnapata maji itaweza kipi kingine

Yani najuta sana kuzaliwa hili li nchi la hovyo
 
Jamaa ana wake wawili!
Akili yake ni kumlinda yule mdogo asiliwe,wakati,tuliopitia hapo tunamtizama tu!
Awapelekee wananchi Matundasi maji!
 
Back
Top Bottom