AY: Nimetimiza ndoto yangu ya kuishi Marekani

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’, ambaye wimbo wake wa Microphone aliomshirikisha Fareed Kubanda ‘FID Q’ ndiyo mpya kwa sasa, amefunguka siri ya kuamua kuishi Marekani.
Akichonga na Star Showbiz, dairekti kutoka kwenye ardhi hiyo ya Donald Trump, AY mwenye makazi katika Jiji la Calabasas, California alisema ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu kwamba siku moja awe na makazi kwenye taifa hilo mbali na alipozaliwa Tanzania.
“Siri ya kuja kuishi Marekani ni kwamba hii ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu niwe na makazi huku. Kwa hiyo kwa kufanikisha kununua mjengo Marekani kwangu nimetimiza jambo moja muhimu sana maishani mwangu na ninamshukuru Mungu,” alimaliza AY.

Source: Muungwana blog
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…