Ayatollah Khameneei alivyoeleza maana ya 'Death to America'

Wewe binafsi umesema US ndio imeleta ustaarabu wa kuzuia vamizi na matumizi ya silaha na hapa unahalalisha tena matumizi ya silaha yoyote? Huoni unakinzana.

Ndio tafsiri ya vita. Vita haichagui silaha

Hizo zingine ni ulaghai
Kama wanavyofanya US Kutumia propaganda kuzuia wanaojitoa mhanga kama mbinu ya kuwaadhibu Marekani kwa Kuwaiti magaidi.

Duniani hakunaga ugaidi.
Vita ni Vita.

Ustaarabu ni kweli bila Amerika leo hii tusingekuwa hapa hilo wala halina mjadala.
Marekani anaudhalimu wake lakini kwenye ubora wake hapo huwezi mtoa
 
Hoja ya Wenyeji wa Amerika hiyo ni hoja nyingine.
Why unasema ni hoja nyingine wakati wameua wenyeji mamilioni sasa wanakuaje tena ndio wastaarabu na wana-demokrasia?

Kumbuka pia marekani ilipiga kura ya kukataa kutambua biashara ya utumwa wa waafrika kama uhalifu dhidi ya binadamu. Na hao ndio unawasifia kwa kuleta ustaarabu?

Usisahau pia hao US ndio walianzisha ukoloni mamboleo ambapo walitoa uhuru kwa nchi za Afrika ili kuja kuzitawala kwa mlango wa nyuma na mfiano unaijua kuanzia Angola, DRC, mpaka Libya. Hii ndio misingi ya demokrasia unayowasifia?
 
Hapana unakosea
Hiyo age ya age of reconnaissance hakukuwa na ustaarabu wowote. Ukisoma historia mpaka huko ulaya kulikuwa pakihuni sana. Tawala nyingi zilikuwa za kifalme, hapakuwa na demokrasia wala haki za binadamu.
Ndio kipindi hichohicho mambo ya utumwa yalipamba moto na ukoloni usemeje kulikuwa na ustaarabu?

Hiyo UN hapo nyuma ilikuwa League of Nation. Hili unalijua. Na bado ilianzishwa na haohao Wamarekani

Hoja ya Wenyeji wa Amerika hiyo ni hoja nyingine.

Hiyo America ilivamiwa kipindi hichohicho unachokiita cha age of reconnaissance alafu unasema ndio kulikuwa na ustaarabu.

Bila Waamerika hata uhuru wa kuabudu usingekuwepo,
Ubabe ubabe ungekuwa mwingi sana.

Dola pekee lililoleta maendeleo duniani ni Dola la Amerika. Hilo liko wazi.
Nimekutajia wazi concert of Europe ambayo ndio ilikua kilele cha age of reconnaissance yaani ustaarabu ulipoanzia. Na ndio miaka hiyo ya 1800 mwanzoni diplomasia ilikua juu kuliko wakati wowote ule duniani. Na hao ni zao la Vienna conference iliyoanzishwa kumaliza hizo Napoleionic wars ambazo ziliitesa dunia kipindi kile.

Nashangaa unaona league of nations ndio organ ya kwanza wakati zilishakuwepo nyingi tokea enzi za Prince Metternich wa Austria.
 
Why unasema ni hoja nyingine wakati wameua wenyeji mamilioni sasa wanakuaje tena ndio wastaarabu na wana-demokrasia?

Kumbuka pia marekani ilipiga kura ya kukataa kutambua biashara ya utumwa wa waafrika kama uhalifu dhidi ya binadamu. Na hao ndio unawasifia kwa kuleta ustaarabu?

Usisahau pia hao US ndio walianzisha ukoloni mamboleo ambapo walitoa uhuru kwa nchi za Afrika ili kuja kuzitawala kwa mlango wa nyuma na mfiano unaijua kuanzia Angola, DRC, mpaka Libya. Hii ndio misingi ya demokrasia unayowasifia?

Unachanganya mambo mawili tofauti.

Sijasema Marekani haina historia takatifu pekee. Mimi nimezungumzia
dunia imetulizwa na kustaarabishwa na Marekani

Mauaji ya wenyeji wa Amerika, utumwa, na baadhi ya sera za nje zinazopingwa ni sehemu ya historia mbaya
Lakini hoja yangu haikuwa kwamba Marekani ni taifa lisilokosea. Hoja yangu ni kwamba imekuwa na mchango mkubwa katika haki za binadamu, ustaarabu, maendeleo ya dunia ya kisasa, katika sayansi, teknolojia, tiba, elimu ya juu, uchumi, na taasisi nyingi za kimataifa. Huo mchango haupotei kwa sababu ya makosa yake, kama ambavyo makosa hayo hayafutwi kwa sababu ya mafanikio yake.

Kwa hiyo, kukiri mchango wa Marekani si kuhalalisha makosa yake, na kukosoa makosa yake si kufuta mchango wake. Historia inapaswa kuangaliwa kwa mizani, si kwa upande mmoja tu.

Unafikiri ni taifa gani sasa hivi linaweza kufikia walau robo ya mafanikio ya amerika dunia kama lingekuwa Supaerpowe
 
Ndio tafsiri ya vita. Vita haichagui silaha

Hizo zingine ni ulaghai
Kama wanavyofanya US Kutumia propaganda kuzuia wanaojitoa mhanga kama mbinu ya kuwaadhibu Marekani kwa Kuwaiti magaidi.

Duniani hakunaga ugaidi.
Vita ni Vita.

Ustaarabu ni kweli bila Amerika leo hii tusingekuwa hapa hilo wala halina mjadala.
Marekani anaudhalimu wake lakini kwenye ubora wake hapo huwezi mtoa
Unajichanganya sasa, nchi iliyoanzisha Nuclear bomb, Ugaidi, na kuvamia nchi nyingi kuliko taifa lolote tokea dunia kuumbwa inakuaje tena ndio imeleta ustaarabu?

Umesema zamani hakukua na zuio la silaha wala uvamizi wa nchi ila leo hii USA inatumia silaha hizo hizo zilizokatazwa, inavamia nchi, inaharibu demokrasia n.k sasa kivipi tena wameleta ustaarabu?

Hapa jibu ni moja haiwezi kuwa mawili. Ni either wamesema ustaarabu au wameharibu ustaarabu sio vyote.
 
Unafikiri ni taifa gani sasa hivi linaweza kufikia walau robo ya mafanikio ya amerika dunia kama lingekuwa Supaerpowe
China mbona imefika hivi nchi gani dunia hii haitumii product za China kuanzia madawa, teknolojia, engineering, etc. Pia Germany inaweza, uingereza ilifanikiwa kipindi chake, Japan ina mchango mkubwa kama Russia iliyosaidia sana nchi za Afrika na amerika ya kusini na Asia hasa kupata uhuru na kujitegemea kiuchumi, kisayansi na kimaendeleo.
 
Nimekutajia wazi concert of Europe ambayo ndio ilikua kilele cha age of reconnaissance yaani ustaarabu ulipoanzia. Na ndio miaka hiyo ya 1800 mwanzoni diplomasia ilikua juu kuliko wakati wowote ule duniani. Na hao ni zao la Vienna conference iliyoanzishwa kumaliza hizo Napoleionic wars ambazo ziliitesa dunia kipindi kile.

Nashangaa unaona league of nations ndio organ ya kwanza wakati zilishakuwepo nyingi tokea enzi za Prince Metternich wa Austria.

Kuna mambo nakubaliana na wewe. Ila kuna mengine naona kama unachanganya madesa na kunilisha maneno.

Nakubaliana kwamba Concert of Europe ilikuwa hatua muhimu sana katika historia ya diplomasia. Baada ya Congress of Vienna (1814–1815), chini ya ushawishi wa Prince Metternich, mataifa makubwa ya Ulaya yaliunda mfumo wa kushauriana ili kudumisha uwiano wa nguvu (balance of power) na kuzuia vita vikubwa vya bara la Ulaya. Hilo halina ubishi.
Lakini hiyo concert ilikuwa kwa maslahi ya mabeberu. Sio kwaajili ya ustaarabu wa dunia na watu wote. Weka kichwani hiyo.

Kusema ndiyo "kilele cha Age of Reconnaissance" si sahihi. Age of Reconnaissance au Age of Exploration kwa kawaida huwekwa kati ya karne ya 15 na ya 17, wakati wa Columbus, Vasco da Gama na Magellan. Congress of Vienna ilifanyika karibu miaka 300 baadaye. Ni mbali sana. Miaka 300 ni mingi sana Mkuu.

Pia, sikusema League of Nations ilikuwa mfumo wa kwanza wa diplomasia. Hoja yangu ni kwamba ilikuwa shirika la kwanza la kimataifa lenye uanachama mpana na katiba rasmi lililolenga kulinda amani duniani. Zingatia ni Duniani tofauti na hoja yako uliyoileta. Concert of Europe haikuwa shirika la kimataifa kwa maana hiyo; ilikuwa makubaliano ya mataifa machache makubwa ya Ulaya na haikuwakilisha dunia nzima. Ndio baadaye kinakuja kile cha Berlin conference. Sijui kama unaelewa hayo mambo. Au kwako huo ndio ustaarabu.

Kwa hiyo, Concert of Europe unaweza kuita mtangulizi muhimu wa diplomasia, lakini League of Nations na baadaye United Nations ndiyo zilianzisha mfumo wa taasisi za kimataifa wenye uanachama mpana na sheria za pamoja.

Kingine unachoshindea kuelewa yote hayo yanaanzishwa sio kwa sababu ya maslahi ya wakubwa. Marekani lakini faida kubwa ni kuwa Marekani yeye utawala wake hata mataifa madogo yanapatemo kidogo na yanakuwa na uhuru.
 
China mbona imefika hivi nchi gani dunia hii haitumii product za China kuanzia madawa, teknolojia, engineering, etc. Pia Germany inaweza, uingereza ilifanikiwa kipindi chake, Japan ina mchango mkubwa kama Russia iliyosaidia sana nchi za Afrika na amerika ya kusini na Asia hasa kupata uhuru na kujitegemea kiuchumi, kisayansi na kimaendeleo.

Mchango wao upo lakini hauwezi kulingana na mchango wa Amerika
Ndio maana hata wao China wenyewe wanakimbilia Amerika kutafuta fursa. Hiyo pekee inaweza kukuonyesha Marekani ni kitu gani.

Ustaarabu na Haki za binadamu Marekani ndiye kinara hilo halina ubishi. Lakini haimaanishi ni nchi takatifu kwamba haina mapungufu.
 
Kwa hiyo, kukiri mchango wa Marekani si kuhalalisha makosa yake, na kukosoa makosa yake si kufuta mchango wake. Historia inapaswa kuangaliwa kwa mizani, si kwa upande mmoja tu.
Unakosea kusema ndio wameleta ustaarabu ilihali ndio wameharibu ustaarabu. Kiufupi walichofanikiwa ni kuzuia wengine kufanya ili wao wafanye wenyewe

Ni sawa na kumsifia jambazi kuu kuzuia majambazi wengine kuiba ili aibe mwenyewe tu. Hii tunaita controlling the narrative ila sio kuleta ustaarabu ila ni kwamba wamehodhi kuvunja sheria, kuvamia nchi na kufanya ugaidi.
 
Kuna ustaarabu zaidi ya haki za binadamu?
Uhuru wa watu kuabudu.
Haki za wanawake sio kama nchi zingine wanawachukulia wanawake kama watumwa na kuwapa mastering yasiyo na kichwa wala miguu.

Haki za watoto
Kutokomeza ubaguzi wa rangi.
Haki za wafanyakazi.

Ni nchi gani unaweza kuilinganisha na USA kwa ustaarabu walau inayofikia nusu yake?
Taja mataifa makubwa unayoyajua.
 
Mchango wao upo lakini hauwezi kulingana na mchango wa Amerika
Kivipi haulingani, actually imports kubwa zaidi USA zinatoka China ikimaanisha USA inategemea China kupata bidhaa na huduma. By the way China mpaka imeikopesha marekani na inadai matrillion ya dollar kila mwaka je kuna nchi nyingine inadaiwa na China kuliko USA? Yaani kwa Pesa za Tanzania ni Trillion 1,730!!!

Hapa sijaongelea Afrika, Asia , Ulaya ambapo hakuna nchi haitumii bidhaa za China.

Ndio maana hata wao China wenyewe wanakimbilia Amerika kutafuta fursa. Hiyo pekee inaweza kukuonyesha Marekani ni kitu gani.
Hapana hiyo ni export services sio kwamba hakuna fursa, hata USA ina viwanda vingi sana China sababu ni nafuu kuzalisha China kuliko Marekani. Hata IPhone tu inakuwa assembled viwanda vya huko China. Hapo sijaongelea micro chips, drone technologies, telecommunications, robotics, na wanatengeneza mambo makubwa kwa bei ndogo alafu unasemaje haina mchango au fursa?
Ustaarabu na Haki za binadamu Marekani ndiye kinara hilo halina ubishi.
Sio kweli, hata Democracy Index score inayopima nchi zenye kusimamia demokrasia hiyo USA ni ya 34 (Flawed democracy) ikimaanisha kuna nchi 33 zenye kusimamia misingi 11 ya demokrasia kuliko USA. We unatoa wapi taarifa kuwa US ndio kinara wa demokrasia?

Kama ulikua hujui USA ndio ina highest jail population duniani almost 20 Million ni wafungwa yaani hata China na udikteta wote haifungi watu hivyo na wewe ndio unawaita vinara wa demokrasia?
 
Kivipi haulingani, actually imports kubwa zaidi USA zinatoka China ikimaanisha USA inategemea China kupata bidhaa na huduma. By the way China mpaka imeikopesha marekani na inadai matrillion ya dollar kila mwaka je kuna nchi nyingine inadaiwa na China kuliko USA? Yaani kwa Pesa za Tanzania ni Trillion 1,730!!!

Hapa sijaongelea Afrika, Asia , Ulaya ambapo hakuna nchi haitumii bidhaa za China.

Hapana hiyo ni export services sio kwamba hakuna fursa, hata USA ina viwanda vingi sana China sababu ni nafuu kuzalisha China kuliko Marekani. Hata IPhone tu inakuwa assembled viwanda vya huko China. Hapo sijaongelea micro chips, drone technologies, telecommunications, robotics, na wanatengeneza mambo makubwa kwa bei ndogo alafu unasemaje haina mchango au fursa?

Sio kweli, hata Democracy Index score inayopima nchi zenye kusimamia demokrasia hiyo USA ni ya 34 (Flawed democracy) ikimaanisha kuna nchi 33 zenye kusimamia misingi 11 ya demokrasia kuliko USA. We unatoa wapi taarifa kuwa US ndio kinara wa demokrasia?

Kama ulikua hujui USA ndio ina highest jail population duniani almost 20 Million ni wafungwa yaani hata China na udikteta wote haifungi watu hivyo na wewe ndio unawaita vinara wa demokrasia?

Unafikiri kwa nini hao wachina, waarabu, wahindi, wajapan na waafrika kwa nini wanataka kwenda kufanya kazi Amerika kuliko maeneo mengine?
Au kuajiriwa na makampuni ya amerika na wazungu?
Jibu utabaki nalo.

Kwenye suala ustaarabu na haki hakuna taifa mpaka muda huu linaizidi amerika
 
Kuna ustaarabu zaidi ya haki za binadamu?
Uhuru wa watu kuabudu.
Haki za wanawake sio kama nchi zingine wanawachukulia wanawake kama watumwa na kuwapa mastering yasiyo na kichwa wala miguu.

Haki za watoto
Kutokomeza ubaguzi wa rangi.
Haki za wafanyakazi.

Ni nchi gani unaweza kuilinganisha na USA kwa ustaarabu walau inayofikia nusu yake?
Taja mataifa makubwa unayoyajua.
Zipo kibao, Australia, Canada, Germany, Uingereza, Austria, Japan, Norway, Denmark, Norway na France, zote hizi ndio zina demokrasia ya kweli huku USA ikitupwa nafasi ya 34. na wala haipo kwenye kundi la nchi zenye Full demokrasia bali Flawed democracies yaani demokrasia yenye mashaka.

Tuongee kwa data sio maoni
 
Na hao ndio amerika wenyewe sasa.
 
Kwenye suala ustaarabu na haki hakuna taifa mpaka muda huu linaizidi amerika
Nimekuwekea data, au unataka za benki ya dunia pia? Ya hao hao wamarekani
https://data360.worldbank.org/en/dataset/EIU_DI

Naomba nikuulize niwaamini benki ya dunia na The economist au nikuamini wewe??
Unafikiri kwa nini hao wachina, waarabu, wahindi, wajapan na waafrika kwa nini wanataka kwenda kufanya kazi Amerika kuliko maeneo mengine?
Wanaenda kwa sababu za kiuchumi sio sababu ya demokrasia. Hivi marekani si ndio hio inafukuza wahamiaji, inaongoza kwa mauaji duniani (homicide), pia inaongoza kwa wafungwa duniani.

Actually ukiwa muarabu au mweusi una asilimia kubwa za kuuwawa au kuwekwa jela na ndio iliozaa kampeni ya black lives matter. Na inaongoza kwa ubaguzi wa rangi na jinsia kwa sababu jamii kubwa ni conservatives. Tafiti kibao na hii moja wapo iliwekwa na CNN ipitie alafu uniambie mweusi au muarabu gani anakua safe marekani.

Nimekuwekea data, au unataka za benki ya dunia pia? Ya hao hao wamarekani
https://data360.worldbank.org/en/dataset/EIU_DI

Naomba nikuulize niwaamini benki ya dunia na The economist au nikuamini wewe??

Wanaenda kwa sababu za kiuchumi sio sababu ya demokrasia. Hivi marekani si ndio hio inafukuza wahamiaji, inaongoza kwa mauaji duniani (homicide), pia inaongoza kwa wafungwa duniani.

Actually ukiwa muarabu au mweusi una asilimia kubwa za kuuwawa au kuwekwa jela na ndio iliozaa kampeni ya black lives matter. Na inaongoza kwa ubaguzi wa rangi na jinsia kwa sababu jamii kubwa ni conservatives. Tafiti kibao na hii moja wapo iliwekwa na CNN ipitie alafu uniambie mweusi au muarabu gani anakua safe marekani.

Taifa gani? Nitajie hayo mataifa bila ya mimi kuingia kwenye hizo link
 
Lakini hiyo concert ilikuwa kwa maslahi ya mabeberu. Sio kwaajili ya ustaarabu wa dunia na watu wote. Weka kichwani hiyo.
The same unaweza sema kuhusu UN unayoisifia ipo kwa maslahi ya mabeberu au ina faida gani hiyo UN kwa nchi maskini? Hata Benki ya dunia, ICC zote hizo ni kulinda maslahi ya mabeberu na kukandamiza nchi maskini.
Congress of Vienna ilifanyika karibu miaka 300 baadaye. Ni mbali sana. Miaka 300 ni mingi sana Mkuu
Ustaarabu ni gradual (taratibu) sio rapid event (haraka) kwahiyo unahitaji vizazi mpaka 10 kuelewa na kusimamia misingi ya demokrasia. Ndio maaa ufaransa walipindua mfalme 1789 na kuanzisha katiba, mahakama huru n.k ila mpaka inakuwa demokrasia iliyokomaa kabisa ni zaidi ya miaka 200 baadae ila mchakato ulianza miaka ya nyuma mnoo.
Ndio baadaye kinakuja kile cha Berlin conference. Sijui kama unaelewa hayo mambo. Au kwako huo ndio ustaarabu.
Ndio ni ustaarabu sababu huko nyuma wangepigania makoloni ila kuweza kuyagawa mezani bila vita ni ustaarabu. Hata UN tu imeshindwa zuia vita za Gaza, Iran, lebanon, Sudan, Ukraine etc kwahiyo haina la kuwazidi Concert of Europe au Berlin conference.
lakini League of Nations
Hii hamna kitu, hawa si ndio walishindwa msaidia mwanachama wao Haile selassie alipovamiwq na italia? Hii nayo yale yale sielewi hata unachoona ilikua "international" kuliko concert of Europe ni nini?
Kingine unachoshindea kuelewa yote hayo yanaanzishwa sio kwa sababu ya maslahi ya wakubwa. Marekani lakini faida kubwa ni kuwa Marekani yeye utawala wake hata mataifa madogo yanapatemo kidogo na yanakuwa na uhuru.
Hapana ni maslahi ya VETO powers pekee ndio maana waafrika walipodai biashara ya utumwa itambulike kama crime against humanity marekani na Israel walikataa kabisa na hoja ya madai ikafia hapo
 
Taifa gani? Nitajie hayo mataifa bila ya mimi kuingia kwenye hizo link
Canada, Japan, Germany, Norway, France, Denmark, Uingereza na zingine kibao ila USA ni ya 34 na haipo kwenye kundi la nchi zenye demokrasia kamili.

Ndio maana nakuuliza ni wapi umetoa ushahidi kuwa marekani ina demokrasia?

Na naomba uelewe demokrasia sio uchaguzi huru tu ila ina misingi 11 na nadhani wengi hamuijui ndio maana mnasemaga tu marekani ina demokrasia bila ushahidi.

Yaani hata the Republic of China inaizidi USA kwenye demokrasia!!!
 
Back
Top Bottom