DOKEZO Responded Ayra Starr amesainiwa Roc Nation. Tanzania tunafeli wapi wasanii wetu kusainiwa na lebo za kimataifa?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Huko Nigeria sasa hivi ni shangwe na vigelegele tu maana kuna msanii wao wa kuitwa Ayra Starr amemwaga wino kwenye kampuni iliyoanzishwa na JAY Z ya kuitwa Roc Nation.

Nilichopenda ni kuwa pamoja na kusainiwa Roc Nation, lakini Ayra ataendelea kuwa chini ya Mavin.

Yaani Roc Nation ni maalum kwa ajili ya kumpush Marekani na Ulaya alafu hawa wakina Don Jazzy wataendelea kudeal na masuala ya distribution na production.

photo_2025-07-17_12-51-30.jpg

Tuje Bongo. Sisi tunakwama wapi wakuu maana hizi deals za kimataifa huwa ni kama zinatupita tu. Shida ni nini?

Yaaani wasanii wetu mtu akishaenda WCB Wasafi na Konde Gang anaona amemaliza. Hizi deals za kimataifa kama Universal, Warner au Sony ni za kuhesabika sana. Hatuzipati kabisa tunazisikia kwa wenzetu tu.

At least Diamond ana deal na Warner Music lakini ni one artist out of maelfu waliopo. Jipu litakuwa wapi?

=========

Fukuto kwenye lebo za ndani

Tanzania karibu kila msanii ana lebo lakini lebo nyingi zinaishia katikati na bila shaka suala hili linatishia kampuni hizo za nje kuja kuwekeza na kusaini wasanii wetu.

Ukiachana na WCB Wasafi, lebo nyingine nyingi Tanzania zimekufa. Wasanii kama Joh Makini, Nandy, Navy Kenzo, Vanessa Mdee, Rayvanny na wengineo wengi, lebo zao zimeshindwa kulea na kujiendeleza kwa ukubwa zaidi.

Kama mazingira ya ndani yako hivyo na lebo zinakufa kila uchwao, hakuna mwekezaji kutoka nje atakuja kuwekeza

photo_2025-07-17_12-52-13.jpg

Streaming Numbers

Ukiachana na Youtube, wasanii wengi wa Kitanzania hawana numbers za kutosha kwenye streaming nyingine ambazo zinashawishi kampuni kama Roc Nation kuja kuwekeza Tanzania.

Huko Spotify na Apple Music wasanii wa Kitanzania ni kama hawapo. Diamond ambaye ndio msanii mkubwa zaidi Tanzania ana Wasikilizaji Milioni 1.2 Spotify wanaofuata unakuta wana 800k, 200k na kushuka chini. Hizi numbers HAZIVUTII WAWEKEZAJI kuja kuwekeza Tanzania.

asake.png

​
Streaming Farms
​
Suala la kudanganya numbers na kuchezesha views kwenye Youtube pia ni changamoto. Tunakumbuka kipindi kile Harmonize "alivyovunja" rekodi ya kupata views Milioni 1.3 ndani ya dakika ndani ya dakika 3 tu? Wasanii wetu kwa muda mrefu wamekuwa wakidanganya na kutumia "maroboti" mambo kama haya yanakimbiza "investors". Hata mimi ningekuwa Roc Nation nisingekuja kuwekeza kwenye industry kama hiyo.

Matumizi ya Kiswahili

Tofauti na Nigeria ambao most of their music ziko kwa kiingereza na pidgin, mziki wetu Tanzania 95% ni Kiswahili na hiyo ni DISADVANTAGE kubwa kwa sababu TUKO LIMITED.

Ukiangalia nyimbo za Nigeria zilizoenda kimataifa nyingi kuna kiingereza humo ndani kwa hiyo zinasikilizwa Marekani, Uingereza na sehemu mbalimbali za dunia.

Tanzania na Kiswahili chetu nyimbo ikihit sana itaenda Congo. Hili nalo ni Tanzania

photo_2025-07-17_12-56-05.jpg

​
Executives Factor

Sababu nyingine ni kwamba Watanzania hatuna viongozi wengi huko kwenye kampuni za kimataifa ambao wanaweza kupendekeza majina ya wasanii kusainiwa kwenye lebo hizo. Wanaijeria wengi wako kwenye kampuni za Universal, Warner, Sony na Roc Nation. Mfano MTV kipindi hicho kulikuwa na jamaa anaitwa Alex Okosi ambaye yeye ni Mnigeria aliyeileta MTV Base hapa Afrika.. Sisi music executives wetu ni kama Babu Tale na Salam. Wako based Tanzania hawana conneections

Historia ya Tanzania

Hizi kampuni za kimataifa zilishawahi kusaini wasanii wa Kitanzania lakini hizo deals huwa zinaangukia pua

Wasanii kama Rose Muhando, Abigail Chams, Ali Kiba, Aslay na wengineo walishawahi kusainiwa na kampuni za kimataifa lakini wengine walijitoa na wengine wakapotea kabisa.

Vanessa Mdee alionya kabisa kuwa mikataba ya kimafaifa ni ya KINYONYAJI na haina manufaa.

Hizi ni chache tu wakuu, mnadhani kwanini hizi kampuni kubwa haziji huku kwenye nchi za Matumbi wanaishia huko kwa wapopo?
 
Wakuu,

Huko Nigeria sasa hivi ni shangwe na vigelegele tu maana kuna msanii wao wa kuitwa Ayra Starr amemwaga wino kwenye kampuni iliyoanzishwa na JAY Z ya kuitwa Roc Nation.

Nilichopenda ni kuwa pamoja na kusainiwa Roc Nation, lakini Ayra ataendelea kuwa chini ya Mavin.

Yaani Roc Nation ni maalum kwa ajili ya kumpush Marekani na Ulaya alafu hawa wakina Don Jazzy wataendelea kudeal na masuala ya distribution na production.

View attachment 3408712

Tuje Bongo. Sisi tunakwama wapi wakuu maana hizi deals za kimataifa huwa ni kama zinatupita tu. Shida ni nini?

Yaaani wasanii wetu mtu akishaenda WCB Wasafi na Konde Gang anaona amemaliza. Hizi deals za kimataifa kama Universal, Warner au Sony ni za kuhesabika sana. Hatuzipati kabisa tunazisikia kwa wenzetu tu.

At least Diamond ana deal na Warner Music lakini ni one artist out of maelfu waliopo. Jipu litakuwa wapi?

=========

Fukuto kwenye lebo za ndani

Tanzania karibu kila msanii ana lebo lakini lebo nyingi zinaishia katikati na bila shaka suala hili linatishia kampuni hizo za nje kuja kuwekeza na kusaini wasanii wetu.

Ukiachana na WCB Wasafi, lebo nyingine nyingi Tanzania zimekufa. Wasanii kama Joh Makini, Nandy, Navy Kenzo, Vanessa Mdee, Rayvanny na wengineo wengi, lebo zao zimeshindwa kulea na kujiendeleza kwa ukubwa zaidi.

Kama mazingira ya ndani yako hivyo na lebo zinakufa kila uchwao, hakuna mwekezaji kutoka nje atakuja kuwekeza

Streaming Numbers

Ukiachana na Youtube, wasanii wengi wa Kitanzania hawana numbers za kutosha kwenye streaming nyingine ambazo zinashawishi kampuni kama Roc Nation kuja kuwekeza Tanzania.

Huko Spotify na Apple Music wasanii wa Kitanzania ni kama hawapo. Diamond ambaye ndio msanii mkubwa zaidi Tanzania ana Wasikilizaji Milioni 1.2 Spotify wanaofuata unakuta wana 800k, 200k na kushuka chini. Hizi numbers HAZIVUTII WAWEKEZAJI kuja kuwekeza Tanzania.

Matumizi ya Kiswahili

Tofauti na Nigeria ambao most of their music ziko kwa kiingereza na pidgin, mziki wetu Tanzania 95% ni Kiswahili na hiyo ni DISADVANTAGE kubwa kwa sababu TUKO LIMITED.

Ukiangalia nyimbo za Nigeria zilizoenda kimataifa nyingi kuna kiingereza humo ndani kwa hiyo zinasikilizwa Marekani, Uingereza na sehemu mbalimbali za dunia.

Tanzania na Kiswahili chetu nyimbo ikihit sana itaenda Congo. Hili nalo ni Tanzania

Historia ya Tanzania

Hizi kampuni za kimataifa zilishawahi kusaini wasanii wa Kitanzania lakini hizo deals huwa zinaangukia pua

Wasanii kama Rose Muhando, Abigail Chams, Ali Kiba, Aslay na wengineo walishawahi kusainiwa na kampuni za kimataifa lakini wengine walijitoa na wengine wakapotea kabisa.

Vanessa Mdee alionya kabisa kuwa mikataba ya kimafaifa ni ya KINYONYAJI na haina manufaa.

Hizi ni chache tu wakuu, mnadhani kwanini hizi kampuni kubwa haziji huku kwenye nchi za Matumbi wanaishia huko kwa wapopo?
Hata huko Nigeria wasanii kama Tiwa Savage alisainiwa ila baadae alijitoa in short label za kimataifa haziongezi chochote Kwa wasanii wa Africa zipo kinyonyaji zaidi
 
kwanza ilibidi ufikirie hili…mpaka kuitwa Msanii mkubwa Tanzania haijalishi wa kike au wa kiume..wanapitia mambo mabaya sana sana..fitna, majungu, chuki, ulozi, mfumo wenyewe haukubebi..ubinafsi…nk..sasa hawa wa kike ni Mungu awasaidie..
 
Hii hoja ya kusema wanaijeria wanaimba kiingereza sijui, wewe unawaelewaga wanaimba nini?
Unaniambia kuna mmarekani ataupenda wimbo wa Davido kwasababu ya rylics? Acheni kutuzingua bhana
 
Ni rahisi kwa Mmarekani kumuelewa Davido au Mmatumbi Mbosso ?
 
Lebo gani ya kimataifa itakubali kusaini masanii ambayo kutwa kujishikamanisha na mambo ya siasa,nani anataka kupata hasara ?

Hayo masanii yenu uchwara ya Tanzania yataendelea Kuwa ya hapo hapo Tanzania,kwanza kuimba hayajui,kazi kurukaruka tu utadhani mehu
 
Ni rahisi kwa Mmarekani kumuelewa Davido au Mmatumbi Mbosso ?

Unataka kuniambia nyimbo za Davido zinapendwa kwasababu ya rylics?
Most richest musician in Africa, Youssou Nd'ou aimbi kiingereza.
Kuna kipindi nilimkuta Angelique kule Maastricht, ndanindani huko Uholanzi alikuwa na sold out concert, nina uhakika more than half of the audience walikuwa hawaelewi maana ya nyimbo zake
 
Mkuu umetoka nje ya mada. Sijaongelea utajiri mkuu.

Nimesema in general ni ngumu wabongo kupenya coz tunazungumza kiswahili.

Wanigeria wanaongea kiingereza kwa hivyo wanaeleweka na watu wa mataifa yote.

Na ni common sense tu. Whether ni lyrics au beat lakini kiingereza kinawabeba sana.
 
International Record Labels ni biashara sio hisani. Zinaangalia zaidi numbers na growth potential - streams, fans, merchandise sales, revenues, costs na net profit.

Itawagharimu kiasi gani kumfanya msanii awe biashara, anaweza kustay afloat kwa muda gani na anaweza Kuingiza faida kiasi gani. Ndipo wanaweka mabillioni yao na mikataba iliyoenda shule sio hizi biashara zenu za hurumahuruma
 
Back
Top Bottom