PostGE2025 Ayub Rioba: Mlitaka turipoti nini Oktoba 29? Kwamba angalia hapa wanavyochoma? au tukaripoti angalia wanavyopigwa risasi?

PostGE2025 Ayub Rioba: Mlitaka turipoti nini Oktoba 29? Kwamba angalia hapa wanavyochoma? au tukaripoti angalia wanavyopigwa risasi?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayub Rioba, amekanusha madai kuwa chombo hicho kilipokea shinikizo kutoka kwa viongozi wa juu wa serikali ili kukaa kimya wakati wa vurugu za uchaguzi za Oktoba 29.

Akizungumza kwenye mahojiano yaliyorushwa na Nijuze Julai 26, 2026, Dkt. Rioba amesema kuwa katika kipindi chote cha miaka kumi alichohudumu madarakani, hakuwahi kupewa amri ya kufanya jambo linalokiuka taaluma yake, na kwamba uamuzi wa kutangaza au kutotangaza matukio hayo ulizingatia misingi ya kitaaluma na wajibu wa vyombo vya habari.

Dkt. Rioba ameeleza kuwa kabla ya matukio hayo, viongozi na watendaji wakuu wa vyombo vya habari nchini walikutana katika ukumbi wa Millenium Towers na kutoa tamko la pamoja bila shinikizo lolote, wakiamini kuwa mazungumzo ndiyo njia pekee ya kujenga demokrasia na kulinda amani. Amebainisha kuwa misingi ya taaluma inavitaka vyombo vya habari kuchukua tahadhari kubwa wakati wa machafuko, kwani kurusha picha za uchomaji wa miundombinu au ufyatuaji risasi kunaweza kuchochea taharuki na kuharibu misingi ya usalama wa nchi.

Ameongeza kuwa udhibiti wa ghasia na ulinzi wa raia ni wajibu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wala si jukumu la wanahabari.

Soma pia PostGE2025 - Dkt. Rioba: Vyombo vya Habari vilitishiwa kuchomwa, tungeripoti vipi Oktoba 29?
 
Maadili ya uandishi wa habari Yako hivo.
Na Sio kuwapa hofu wananchi.
 
Yes tulitaka mripoti hayo yes

Kwani si ndio uhalisia au? Kwann mnaficha, mnamficha nani?
 
Ndiyo, mlipaswa kuripoti matukio yote, nyie mkakausha/mkapotezea. Wananchi tukakimbilia media za nje kuona kinachojiri, huko nako mkazuia tusione. Tubuni, mliwakosea wananchi kuwanyima taarifa nyeti
 
Back
Top Bottom