Azam FC imewatimua makocha wake wote raia wa Hispania

Kali Ongara hawezi....

Ile timu ni kubwa sana. Imagine Stewart Hall aliikimbia..... Kwa visingizio vya ajabu ajabu.
Haiwezi kwani anaibeba mgongoni ile sio Ndala FC ambayo hawaamini kocha

Mpaka mzungu wa watu mnamlazimisha cheo ambacho hakikuwa katika mahesabu yake
 
Ni bora wakuvyowatimua ili wajipange upya lakini hata uongozi wa Azam Fc siuamini pia.
 
Sikumbuki nilikuwa nachangia thread ya nani lakini nilisema hawatamaliza msimu.
Makocha wote wageni na wachezaji wengi wapya ilikuwa mchanganyiko mbovu sana

Mpira wetu Bongo una vimelea vya EPL zaidi kuliko la Liga. Makocha hawakutambua hilo

Waende tu hawakuwa na jipya. Ili kuleta ushindani wa kweli kwa Yanga na Simba, viongozi wa Azam6watulize vichwa wakati wanatafuta kocha mpya.

Omog ni kama anawasuta kiana. Pale Simba kwa resources kidogo anafanya vizuri zaidi. Azam wajiulize tatizo liko wapi?
 
Tatizo kubwa la Azam FC ni CEO wao Sad Kaemba kama sijakosea jina lake. I do not see kama he fits for the job. Azam FC wamewekeza sana kwahiyo hawanabudi kusajiri wachezaji na makocha wa viwango vya juu. Kigezo cha kwanza kwa professionals lazima awe anachezea timu ya taifa lake na si vinginevyo if they real serious na uwekezaji kwenye football club businesses.
 
Unanipa shaka kidogo! Yaani Saad Kawemba ni chanzo cha Azam FC kutofanya vizuri?

Unamaanisha hata akija Kocha yeyote pale Azama, haitofanya vyema mpaka saad kawemba aondolewe?

Acha utani mkuu! Kama unabifu naye binafsi naona ni wakati muafaka ukamfuata na mkayamaliza.

Saad hasajili wachezaji

Saad hasajili makocha

Saad hausiki na Ufundi

Saad hausiki directly na utendaji & performance ya Klabu.

Kama una uhakika kuwa yeye huwa anahusika mpja kwa moja kuscout wachezaji, kuajili Makocha, tupe ushahidi hapa ili tuamini ukisemacho. Vinginevyo si kweli ulisemalo
 
Haiwezi kwani anaibeba mgongoni ile sio Ndala FC ambayo hawaamini kocha

Nimecheka sana ulivyo quote hii post!

Ati leo, tena mbele ya Mashabiki wenzako wa Matopeni FC unasema kuwa Mabingwa watetezi wa LigiKuu ''Hawaamini Makocha".

Klaba ya kuandika ungejiuliza tangu Yanga wawe na Hans Van De Pliujm.... Simba imekuwa na Makocha wangapi na imefukuza wangapi?

Unheanzia hapo usinhekuwa na la kuongea kuhusu Makocha.
 
Mpaka mzungu wa watu mnamlazimisha cheo ambacho hakikuwa katika mahesabu yake



Inaonekana Babu Hans amewasababishia Ukavu wa Makombe pale Matopeni hadi mnamchukia kiasi kwamba hamtaki hata kuuona uso wake....

Mlitarajia tutamfukuza arudi kwao?

Hapana! Tumemuweka karibu ili aendelee kuwapa tumbo joto kila aonekanapo uwanjani!

Kama anawatisha inabidi mukwepeshe sura. [emoji23]
 
Rudi kwenye mada ya Azam FC wewe Madeni FC..!
 
Wale makocha wa kihispania walikuwa wanaifundisha Azam kihovyohovyo tu. HALAF NILIKUA NIKIWAANGALIA NAONA WAMEKAA KIUBISHOO ZAID KULIKO KIUKOCHA.
 
Binafsi hatufahamiani kabisa na Saad Kawemba na personally simchukii yeye as an individual , mimi ni mpenzi wa vitu vya kitanzania sana na mpenzi wa kati ya timu zetu kongwe nchini. Pamoja na kuwa mpenzi wa hiyo timu kongwe, binafsi kama mtanzania mzalendo na mwanamichezo sipendezwi na mifumo ya kizamani ya uendeshaji wa timu zetu hasa hizi kongwe. Kwahiyo ujio wa Azam FC ktk soka letu kwangu yalikuwa ni mapinduzi na nilitegemea wangekuja kufanya kweli lkn as time goes on, nimeshuhudia mkombozi/change agent wetu (Azam FC) akideteriote year after year. Saad ni CEO wa hii team, in my view haijarishi kama ni yeye anasajiri makocha au wachezaji, kama mshauri mkuu wa sponsor/mmiliki wa timu, kama timu inafanya vibaya, he must take full responsibilities na awajibike. Like I said it before, ninaifuatilia sana Azam FC pamoja na watendaji wake kwa wema thus why I was even convinced kuomba hata uanachama but I couldn't kwa sababu sikujua ni namna gani unaweza kujoin. Otherwise I like Azam FC as football club.
 
Kocha anaeiwezea Azam ni Stewart Hall,sitashangaa kama watamrudisha.
 
Sikuridhia aslan, wachezaji wana lao jambo. Haiingii akilini mfungaji kuweka mbwembwe pahala pa kufunga halafu anasingizia mfumo, HATA KUFUNGA BASI et MFUMO!!!!!!!!!!!!!!? Huyo Kali ataifikisha wapi timu kimataifa? Niliisha toa rai kuwa pana watu hapo Azam walichokifuata ni noti tu lakini Usimba na Uyanga umo ndani yao.
 
Kweli mkuu, ipo haja ya mwenye timu kuanza kuwaangalia viongozi wa timu kwani wanafanya mambo yale yale ya Simba na Yanga kwani wengi wao wametoka huko huko.
 
Kocha anaeiwezea Azam ni Stewart Hall,sitashangaa kama watamrudisha.
Hakuna Kocha aliyepewa muda na Azam kama Stewart Hall.

Kwanza aliikimbia ligi ya Bongo. Kaona aende Kenya ambapo hakuna Yanga na Simba.

Hawezi kurudishwa.. Naona kocha mwenye uzoefu na soka la Kiafrika akiingia pale.
 
Kweli mkuu, ipo haja ya mwenye timu kuanza kuwaangalia viongozi wa timu kwani wanafanya mambo yale yale ya Simba na Yanga kwani wengi wao wametoka huko huko.
Viongozi azam ndii tatizo,si wa kweli wanamdanganya mmliki ,asiposhtuka Azam itakua timu ya kawaida tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…