Azam FC mpeni timu huyu mzawa

Azam FC mpeni timu huyu mzawa

Kwa misimu mingi klabu ya Azam FC inahangaika sana kupata kocha atakayeifanya Azam iwe klabu tishio uwanjani.

Kwa maoni yangu kuna makocha wawili wazawa ambao wakipewa hii timu ya Azam wanaweza kuiletea mafanikio makubwa sana.

1. Fred Felix Minziro "Kataraiya Majeshi Baba Isaya"

Minziro ni moja ya makocha bora sana kwa sasa kwenye ligi yetu ya NBC. Akipewa timu ya Azam na wachezaji waliopo kwa sasa anaweza kufanya "kitu cha kuonekana".

2. Meck Mexime
Mexime ameibadilisha Kagera sugar kwa kipindi kifupi sana na "ameifufua".

Azam FC nawashauri Januari hii mpeni timu mmoja wa makocha hao. Lakini pia itakua faida kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 23/24 maana msimu huu wa 22/23 tayari mmeonekana kufeli pakubwa.

Kwa sasa Azam haina kocha anayemzidi uwezo Minziro wala Mexime.

View attachment 2477530View attachment 2477531
Wamchukue Mgunda.
 
Coast alikuwa na resources zipi ukifannisa na Azam? Unapotaka kumlaumu kocha angalia resources alizokuwa nazo na mazingira yanayo mzunguka hata kwa Simba Mgunda kajitahidi kuifikisha pale.
Mwambusi alionyesha ubora wake kwa resources hizo hizo ndogo akiwa Mbeya City, Mexime anaonyesha ubora kwa resources hizo hizo ndogo akiwa Kagera, na hata Minziro ni hivyo, yeye Mgunda alishindwa vipi mpaka timu kucheza play off mara mbili chini yake.
 
Kushinda mechi kuna mambo mengi yanachangia ikiwemo uwezo binafsi wa mchezaji. Ongala hana mbinu, anabebwa na uwezo wa wachezaji.
Basi anajua kuhamasisha, 🤣🤣 Wakati wa mzungu aliekuwa anacheza vizuri yule kapten na Kipre, baada ya mzungu team nzima ikaamka na kupata matokeo
 
Mwambusi alionyesha ubora wake kwa resources hizo hizo ndogo akiwa Mbeya City, Mexime anaonyesha ubora kwa resources hizo hizo ndogo akiwa Kagera, na hata Minziro ni hivyo, yeye Mgunda alishindwa vipi mpaka timu kucheza play off mara mbili chini yake.
Kwani Mgunda hajawahi kuonyesha ubora wake akiwa Coastal Union.?

Mbeya City ni timu ya jiji ina uhakika wa posho na mishahara na sio Coastal ya kuunga unga huwezi zifananisha.

Mexime alikuwa kwenye timu ya kampuni ya sukari nao hawanaga tatizo la posho na mishahara huwezi fananisha na Coastal.

Minziro alifikia mafanikio yapi ambayo yame mzidi Mgunda mpaka sasa.

Ninapo zungumzia resources na maanisha mishahara na posho kwa wakati, mazingira mazuri ya wachezaji na kocha mwenyewe na usajili wa wachezaji.
 
Minziro msimu wake wa kwanza akiwa Geita Gold amemaliza nafasi ya 4, amecheza hatua ya awali CAF CC akatolewa kwa tofauti ya goli 1.
 
Basi anajua kuhamasisha, [emoji1787][emoji1787] Wakati wa mzungu aliekuwa anacheza vizuri yule kapten na Kipre, baada ya mzungu team nzima ikaamka na kupata matokeo
Ni mhamasishaji mzuri kweli ila ki mbinu bado sana.
 
Kwa Tanzania..mambo Ni magumu sio uwekezaji pekee..kwa mechi za ndani Kuna kununua mechi flani flani ili kubaki juu..kwa mechi za kimataifa lazima ufanye figisu(kutumia vizuri uwanja wa nyumbani)
 
Kwa Tanzania..mambo Ni magumu sio uwekezaji pekee..kwa mechi za ndani Kuna kununua mechi flani flani ili kubaki juu..kwa mechi za kimataifa lazima ufanye figisu(kutumia vizuri uwanja wa nyumbani)
Mambo ni mengi sawa, hata kama unanunua mechi ila "boli lazima lionekane likitembea uwanjani".
 
Minziro msimu wake wa kwanza akiwa Geita Gold amemaliza nafasi ya 4, amecheza hatua ya awali CAF CC akatolewa kwa tofauti ya goli 1.
Kwani aliyeifikisha Simba Round makundi ya michuano ya mabingwa CAF ni nani?
 
Meck Mexime
Mexime ameibadilisha Kagera sugar kwa kipindi kifupi sana na "ameifufua".
Mtu hajafikisha hata mechi 10 hapo kagera mshaanza kusema sana. Tulia amalize msimu.
Pia rekodi zake za nyuma hazisadifu unachosema.
Aendelee kujifunza zaidi na ikiqezekana aongeze elimu kwa kuwa na CLASS A ya CAF.
 
Back
Top Bottom