Azam FC ni sikio la kufa ,hawajui hitaji lao nini asa ukiacha kukamia Simba na Yanga

Azam FC ni sikio la kufa ,hawajui hitaji lao nini asa ukiacha kukamia Simba na Yanga

King Leon 1

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2019
Posts
245
Reaction score
342
Kiukweli mimi kama mdau wa soka la Tanzania na dunia kwa ujumla, nashindwa kuelewa kuhusu Azam FC, kiufupi hii timu inawachezaji wa hali ya juu na vitu vyote vya kimichezo kama uwanja na facilities zote zipo lakini Azam Fc imekuwa ni timu ya mechi mbili tu yaani Vs Simba na Vs Young Africans.

Uku mechi za timu za daraja la chini yake ikishindwa kufurukuta. Asa apo Azam na viongozi wao waambiwe ukweli kama wanataka kuzichallenge Simba na Young Africans kuchukua ubingwa basi yawapasa waanze kuwa serious na mechi za daraja la chini yake na sio Simba na Yanga tu.

Ni heri upoteze mechi mbili na ushinde zilizobaki utakuwa na nafasi nzuri ya kuchuana kwenye ubingwa, vinginevyo na apo ni kuwa wasindikizaji tu.

Mechi ya juzi vsSimba tuliona Azam ilivyo tumia nguvu na jitihada zote yaani kiasi kwamba unasema wako final ila Azam ile ndio hii iko uwanjani inatolewa jasho na Namungo utafikiri Azam wachezaji wapya sio wale wajuzi aseeh inasikitisha sana maana siwaelewi ama wao ndio hawajielewi.

Ni lini Azam Fc itafufuka na kutambua kuwa ubingwa unaweza patikana kwa kushinda mechi izi ndogo nasio kukamia timu mbili tu!

Wachezaji,Viongozi na wamiliki wa Azam Fc wajitathmini tujue kama wao ni wasindikizaji ama lah???
 
Azam haina quality players wengi. Ukimtoa Feisal na Silah wana nani mwingine?. mechi ya juzi ni uzembe wa simba wenyewe, walikuwa na uwezo wa kushinda ile me

Azam haina quality players wengi. Ukimtoa Feisal na Silah wana nani mwingine?. mechi ya juzi ni uzembe wa simba wenyewe, walikuwa na uwezo wa kushinda ile mechi
Tazama kikosi cha Azam FC, wana qualities players wengi tu japo ndio hao leo high kesho low. Performance yao haitabiriki
 
Kilicho wagharimu Azam ni muda mfupi kucheza baada ya kutoka kucheza mechi ngumu.

Ata Simba angekua anacheza leo na Coast, Simba wangepoteza au kutoa sare.
Azam haina mjomba ndio maana amecheza back to back.
 
Leo wako kimya ila ona viongozi na waandishi wao wanavyojihangaisha mechi za Simba na Young Africans utafikiri timu ziko 2 tu kisha wachukue ubingwa
 
Fixture kwao haikuwa rafiki yametengenezwa mazingira ya azam kudondosha point
Hakuna kitu Kama iko mbona Singida hadondoshi alama kiasi iko kwa izo mechi anajitaidi kuchukua alama. Tatizo la Azam Fc ata Mayele alisema wanakamia tu Simba na Young Africans japo walipinga na kuona wanaonewa ila ukweli ndio huo
 
Hakuna kitu Kama iko mbona Singida hadondoshi alama kiasi iko kwa izo mechi anajitaidi kuchukua alama. Tatizo la Azam Fc ata Mayele alisema wanakamia tu Simba na Young Africans japo walipinga na kuona wanaonewa ila ukweli ndio huo
Duh sasa imekuaje Azam akawa juu ya Singida?
 
Back
Top Bottom