Azam kuonesha mechi ya Yanga na Al Hilal

Azam kuonesha mechi ya Yanga na Al Hilal

Naam, baada ya vibonde Al Hilal kunusurika kupigwa kama ngoma uwanja wa Mkapa silaha yao kubwa iliyokuwa imebaki ni kutaka kuchezea mechi gizani, yaani isonyeshwe kwenye TV. Lakini Azam TV wamefanikiwa kupangua baada ya kuwashawishi ma bosi wa Al Hilal kuonyesha mechi hiyo.

Ikumbukwe kwamba Yanga kupitia kwa msemaji wao Ally Kamwe ilishawatoa hofu wana Yanga kwa kuwakumbusha kwamba Yanga ina uwekezaji mkubwa na ina wachezaji wakubwa wenye wasifukubwa kuliko Al Hilal.

Ikumbukwe yanga ina MVP wa Ivory Coast mwaka jana KI AZIZ, Yanga ina mchezaji mkubwa sana aliyecheza newcastle UTD Bigirimana. Jamaa anapiga pasi kinoma zenye macho, yaani ina kiungo bora namba 2 wa Ligi ya Kenya mwaka 2018 Khalid Aucho, ina kipa aliyecheza Kombe la Vijana la Dunia na kushika nafasi ya 3, Diarra
ina Bangal MVP wa bongo. Ina uwekezaji wa tajiri asiye mbahili anayemwga mapesa bila mawazo wala kuhesabu katoa sh. ngapi, Gharib.

Yanga alishinda goli 4 -0 ugenini dhidi ya Zalan, marudiano yalipofanyika nyumbani akashinda 5-0. Unadhani kwanini asishinde goli 2-0 hapo Sudan, Khartoum?


View attachment 2381596
We umesikia wapi?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom