azam kutoa la-liga, na kuleta bundasilga ,nini maoni yako?

azam kutoa la-liga, na kuleta bundasilga ,nini maoni yako?

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
kwangu mimi naona huku ni kuchemka kabisa kama EPL imeshindikana ni bora tungebaki Spain, na la liga yetu, ambapo walau kuna mabingwa wawili, Barcelona na Real Madrid, kuliko huku ambapo unaona kabisa Bayern anatawala peke yake,

wewe unaonaje
 
Wamechemka. Ukilinganisha Laliga na hiyo Bundesiliga, hakika Laliga ilikua na unafuu na mvuto zaidi. Itatubidi sasa kuanza kuzikariri timu za Ujerumani!

Huku ni kuchoshana.
 
Messi anaondoka soon. Ligi hiyo mvuto wake ndiyo unaishia hivyo. Ramos kamuomba Messi abaki akisema Messi ni nembo ya La Liga. Akienda ni watu wangapi wataifuatilia La Liga?

Azam kaona mbali.
 
Messi anaondoka soon. Ligi hiyo mvuto wake ndiyo unaishia hivyo. Ramos kamuomba Messi abaki akisema Messi ni nembo ya La Liga. Akienda ni watu wangapi wataifuatilia La Liga?

Azam kaona mbali.
Hata Messi akisepa laliga huwezi linganisha na Bundesliga
 
Azam wameona mbali ukiangalia La Liga hata Dstv wanaonyesha ila Bunde hawaonyeshi so italeta kamvuto na pia Ligi ya Ujeruma ni nzuri sana sema imekosa promo angalia hata Timu zao UEFA zinafika mbali sana na kubeba ndoo wacha nianze kuangalia Bayern Munich Vs Dortmund Live.
 
[SUP]Bundesliga kwa sasa ni mzuri kuliko la liga. Vilabu kama Liverkusen, Monchengladbach, Leipzig vinacheza mpira mzuri na bora karibu sawa na BvB na Munich.[/SUP]

[SUP]Tuache kulialia tukubali mabadiliko. Laliga kwa sasa vilabu vyao vimekuwa vya kawaida na soka lao limepungua uboro.[/SUP]
 
Nilimsikiliza Charles Hilal Jana kwenye U live pale Ufm...point kubwa amesema "ilikua La liga ili watu wamuone Ronaldo na Messi...Ronaldo ameondoka, Messi alikua anatingisha kuondoka"
Kifupi nimemuelewa wameangalia biashara...lewandowisk...Mula..Gnabri...Sancho..Haland ni business kwa sasa kuliko kina Benzema..Ramos...Modric..pia kumbuka waliassume kama Messi anaondoka.
 
La Liga ina ushindani kiasi kuliko Bundes kwasababu La liga ina timu Tatu shindani ktk nafasi ya ubingwa Madrid, Barca na Atlético,,, na ktk nafasi sita za juu utawakuta kina Sevilla, Valencia na Villareal wakipambana.

Wakati Bundes ni Bayern miaka yote anatawala, wengne wote wamebakia kutengeneza wachezaji kuwauzia Bayern.

Ijapokuwa ktk angle ya kibiashara, La liga kumpoteza Cr7 imekuwa pigo kwao na endapo Messi nae akiondoka basi ligi itapoteza pakubwa sana. Mimi mwenyewe nilisikitika sana na nilipoteza hamu ya kuitazama Madrid baada ya Cr7 kuondoka

Hvyo hata Azam pengne wamepredict hilo baada ya Messi kuanza kutingisha kibiriti

Ila kiujumla La Liga ina ushindani kulinganisha na Bundesliga
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Back
Top Bottom