Itakua ulichanganya mkuu. Hakujatokea kitu kama hicho, huenda hiyo boat nyingine iliwasili kutoka Unguja au ilitokea pale wanapopark zinaposhusha sealink 1, 2 na ile ya Comoro.
Jumatano tumeondoka na 7 huku Zanzibar 1 akiwa nyuma yetu, kukaribia Chumbe alitupita ila tukashuka wote bandarini.
Zile Zanzibar 1 na 2 zinaenda hadi 37 knots wakati Azam K7 inaenda hadi 33 knots kama sikosei. Hivyo Zanzibar 1 akiikandamiza kabisa kwa mwendo atamuacha tu Azam.
Anazo mbili kwa sasa, ila Azam mkongwe kwenye hii tasnia atakuja na kitu cha kwenda mwendo wa hatari.
Pia hizi boat za Turkey na Zacharia wanazipumzisha. Kuna wakati upande mmoja unakua hauna boat, inaweza kupiga safari moja asubuhi, ikapumzika hadi saa kumi.
Bakhresa anaweza kuuza K5 na K6 alete toleo jipya, zile haziwezi kupambana na Zanzibar one hata siku moja, injini zake za propeller. K4 na K7 ndio jet kama Zanzibar 1 na 2.
Huu ushindani sio nafuu kwa abiria tu, hata wafanyakazi wanakua na kuchagua kitu kitakachoboresha maslahi yao pia. Jamaa kakomba wafanyakazi wa Azam wengi sana.