Azam Media yanunua haki za matangazo Ligi Kuu Kenya

Azam Media yanunua haki za matangazo Ligi Kuu Kenya

yote sawa, tisa kumi kwanini timu zetu azipe milioni mia tu kwa mwaka ambayo ni sawa na milioni tano za kenya, halafu wakenya awape milioni mia mbili kwa mwaka sawa na milioni kumi za kenya... Sababu hasa ni nini????????????

Pengine ni matangazo mengi ya makampuni yenye base Kenya yatakayokuwa yanaenda na mechi zitakazo oneshwa live ktk TV hivyo matangazo mengi siyo ya AZAM tu labda hata Heineken Beer n.k yataweza kupenyezwa wakati wa urushaji wa mechi live na hivyo timu za Kenya na Azam TV (Kenya) kugawana kipato zaidi.

Azam TV2 Tanzania nao labda mwakani wataweza kupata matangazo zaidi ya Juice/ice-cream na hivyo kuongeza kipato pale makampuni yaliyoko Tanzania wakigundua umuhimu wa kutangaza bidhaa na huduma zao AZAM TV Media Tanzania channel 2 sports.
 
Stop beating around the bush,nunueni EPL mfanye cha mana sio mbwembwe kibaoooo.eboo.
 
kuna watu walisema azam bado sana kwa sababu et dstv amechukua coverage ya kenyan league sasa naona taratibu tunaenda kule tunapohtaji.... imebak ya nigeria ghana congo na south africa wenywe naamin tutafika tu

Zote ni kabumbu tunataka anunue za soka kama uingereza,Spain na nyingine za mana sio mchangani tu.na aongeze hata afike 50 kwa mwezi.
 
Ligi ya Kenya ni mbovu wataangalia wakenya wenyewe, viwanja utazan ligi ya mchangani, bora ligi yetu mara buku
 
Hongera Azam TV, mwendo mdogo MDOGO! Hadi EPL. Bila shaka strategy zenu ni kuhakikisha mmeuza Ving'amuzi vingi kwenye huu ukanda wa Africa mashariki kabla hamja jitosa kununua Haki ya kuonyesha ligi kuu za Ulaya!!! Big up!!

Klabu zitalamba Kenyan shilling 1 m kila mwezi?? Inamaana ligi yao iko juu kuliko yetu???
Kama sikosei sisi timu zetu zinalamba milioni mia kwa msimu mzima!!

Ligi yao siyo lazima iwe juu kuliko yetu. Kwa haraka haraka, KES 1m/= ni karibu sawa na TZS 20m/= kwa miezi 12 ni sawa na TZS 240m/= kwa kila klabu wakati Bongo ni 100m/= kwa mwaka. Yanga walipogomea dau hilo walionekana wasaliti, sasa Kenya wanafaidi zaidi ya mara 2. Wakenya ni wazuri sana katika negotiation wakati Wabongo isipokuwa Yanga ni 'NDIYO MZEE'. Shame to Simba SC na mabinti zake!
 
Safi sana. Monopoly ya DSTV itapungua kidogo,lakini yule CEO Mzungu na assistant wake Tido D Mhando wanatakiwa wakaze, wakilemaa watapigwa fitina kali sana!

Nina imani kubwa sana na Tido Mhando!
 
Ligi yao siyo lazima iwe juu kuliko yetu. Kwa haraka haraka, KES 1m/= ni karibu sawa na TZS 20m/= kwa miezi 12 ni sawa na TZS 240m/= kwa kila klabu wakati Bongo ni 100m/= kwa mwaka. Yanga walipogomea dau hilo walionekana wasaliti, sasa Kenya wanafaidi zaidi ya mara 2. Wakenya ni wazuri sana katika negotiation wakati Wabongo isipokuwa Yanga ni 'NDIYO MZEE'. Shame to Simba SC na mabinti zake!
Hizo hesabu kuna mahali haziko sawa, ukichukua milioni moja kwa mwezi kwa timu utapata jumla ya milion 16, ligi ya kenya ina timu 16, na kwa msimu mzima kama tafsiri ya msimu ni mwaka mzima maana yake utapata milioni 192, hizo ni hela za kenya.

Lakini ukichukua kiasi cha hela ambacho kimetolewa kwa misimu mitatu yaani milion 204.75 kila msimu utakuwa na milion 68.25, kwa hiyo hela kila timu itapata ~milion 4.3 kwa msimu wote, kama bado tafsiri ya msimu mmoja ni mwaka mzima hivyo kila timu itapata ~milion 0.358 kwa mwezi.

Labda kama tafsiri ya msimu haimanishi mwaka mzima.
 
yote sawa, tisa kumi kwanini timu zetu azipe milioni mia tu kwa mwaka ambayo ni sawa na milioni tano za kenya, halafu wakenya awape milioni mia mbili kwa mwaka sawa na milioni kumi za kenya... Sababu hasa ni nini????????????

Nadhani shirikisho la soka ndio wanafanya negotiation na Azam sasa inavyoonekana wao Kenya wali demand milioni 10 na TFF kwa Tanzania aliridhika na ile milioni 5
 
Safari moja huanzisha nyingine

Naam.

Halafu hiyo signature yako design kama ngeli ya ugoko hivi.

Ras Yanga nini?

The future belongs to those...................

Hiyo ....is.....ichomoe mazee.

Samahani lakini....
 
Back
Top Bottom