AZAM imepata haki miliki ya kuonyesha Mechi zoote za LA LIGA. TIDO, anasema kwamba alikutana na Uongozi wa La Liga DUBAI,na kuwaambia uwezo wa AZAM TV.
Na haikuwa kazi rahisi kupata Haki miliki kwa kuwa jopo la La Liga lazima lijue uwezo wa Kituo husika na ubora wake.
Ilichukua muda mrefu saana tangu wawasilishe maombI yao, hatimae yamekuwa.
Amegusia tena kuhusu Arsenal TV, wapo kwenye mazungumzo hatua za mwisho na amesema kuna uwezekano wa kupata haki miliki ya kuonyesha mechi zao muda sio mrefu.
Manchester United na Liverpool wapo kwenye mazungumzo na yanaendelea vizuri.
Amegusia Tena Kuhusu EPL wapo kwenye mazungumzo nao, Uongozi mkuu wa AZAM TV ulitoka na kuwafuata viongozi wa EPL UK.
TIDO anakiri kwamba ni kazi kubwa zaidi kwa hili,lakini amesema watafika hatua nzuri tu.
AZAM TV ndio habari ya MJINI