Azam Media yapata haki za kuonesha Ligi Kuu ya Hispania

Azam Media yapata haki za kuonesha Ligi Kuu ya Hispania

safi sana....Azam mnaweza kuwa washindani wazuri wa DSTV
 
Mkuu mbona wamesema mechi zote

Hawezi pewa exclusive right maana hata Dstv hana exclusive right ndo maana anaonesha mechi kadhaa.
Mechi 20 ni kazi na ndo maana hata EPL dstv haoneshi zote 20 kwa siku au wiki
 
Wataongeza tena fee zao? Maana tangu walipoongeza hizo fee, sijawahi kulipia kifurushi cha premium.

Vv
 
Hawezi pewa exclusive right maana hata Dstv hana exclusive right ndo maana anaonesha mechi kadhaa.
Mechi 20 ni kazi na ndo maana hata EPL dstv haoneshi zote 20 kwa siku au wiki

Mdau,
Kama unavyojua habari ya mjini, La Liga LIVE kupitia AzamTV, kuanzia msimu huu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 15 mwaka huu. Mtaweza kuona mechi zote za msimu mzima, LIVE!!!

Kama mdau wetu, tungependa kujua uko tayari kulipia nyongeza kiasi gani ili kuipata La Liga LIVE kutoka nyumbani kwako.
... Tunahitaji mchango wenu katika hili mkiwa kama wanafamilia wa AzamTV, ili kufanikisha kumudu gharama za uendeshaji na kukifanya kuwa kituo bora kabisa kinachotoa huduma nzuri na kwa gharama nafuu.
Hili ni letu, tujadili ‪#‎ongeanasi‬ uwanja ni wako!
 
Hawataonesha mechi zote.. hapo ni mechi moja kwa wiki tena zile kubwa kama El Clasico sijui

Mlianza kwa kudharau hivihiv kua hawez sasa mnasema sio mechi zote.tulieni muone.
 
Ni vyema sana kuonyesha ligi bora...ila real madrid Tv haionyeshi...wafanye marekebisho
 
Yeah! EPL ilikuwa na mvuto sana enzi hizo. Kwa sasa umepungua...Ngoja tuone mwaka huu!
 
Kupata rights za kuonyesha hii EPL na la liga ni expensive sana. Hapa kifurushi lazima kita shoot up mpaka 70 - 80 huko kwa hio la liga, bado kuna FA, CARLING CUP, EUFA, Ligi za ufaransa,italy na ujerumani. Kwa mpzi wa soka hawezi kuhama kisa ligi mmoja alafu aende kwenye kibanda kwenye mechi zingine. Once azam wakishapata hvi vyote lazima price itafika kama ya dstv tu. Mnakumbuka GTV kilitokea nn
 
Azam hawawezi hiyo kitu!' narudia tena hawawezi, wanataka watu wanunue vingamuzi vyao!' tu hawana lolote .........
 
AZAM imepata haki miliki ya kuonyesha Mechi zoote za LA LIGA. TIDO, anasema kwamba alikutana na Uongozi wa La Liga DUBAI,na kuwaambia uwezo wa AZAM TV.
Na haikuwa kazi rahisi kupata Haki miliki kwa kuwa jopo la La Liga lazima lijue uwezo wa Kituo husika na ubora wake.

Ilichukua muda mrefu saana tangu wawasilishe maombI yao, hatimae yamekuwa.

Amegusia tena kuhusu Arsenal TV, wapo kwenye mazungumzo hatua za mwisho na amesema kuna uwezekano wa kupata haki miliki ya kuonyesha mechi zao muda sio mrefu.

Manchester United na Liverpool wapo kwenye mazungumzo na yanaendelea vizuri.

Amegusia Tena Kuhusu EPL wapo kwenye mazungumzo nao, Uongozi mkuu wa AZAM TV ulitoka na kuwafuata viongozi wa EPL UK.

TIDO anakiri kwamba ni kazi kubwa zaidi kwa hili,lakini amesema watafika hatua nzuri tu.

AZAM TV ndio habari ya MJINI
 
Wekeni vifurushi vya Tsh 20, 35 na 50 ila muakikishe walau na hzi za clubs TV nazo zinaruka pls.. leteni Arsenal TV kwanza.
 
Hawezi pewa exclusive right maana hata Dstv hana exclusive right ndo maana anaonesha mechi kadhaa.
Mechi 20 ni kazi na ndo maana hata EPL dstv haoneshi zote 20 kwa siku au wiki

Mechi 20 kwa siku? Inamaana Ligi inatimu 40?
 
Kapandishana sana bei karibia 125% toka elfu12 had elfu30 ndani ya mwaka mmoja hii hatari sana inamaanisha miaka miwili bei itakuwa kubwa kuliko dstv..!!
 
Back
Top Bottom