Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 783
- 2,057
Waswahili husema mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, mchezaji wa Azam, Prince Dube ameandika barua ya kuvunja mkataba ambao umebakiza miaka 2!
Jambo hili sio jambo zuri hata kidogo kwenye soka letu, suala la mchezaji kukosa tu furaha na akaamka asubuhi na kuandika barua ya kuvunja mkataba ni jambo la ovyo sana!
Lilitokea kwa Feisal na watu wa ovyo ambao hawakujua ni kitu gani kinatengenezwa wakawa wanaunga mkono ujinga ule matokeo yake kilichofanyika ndio kinakwenda kufanyika Tena kwa Prince Dube!
Tuliwaonya Azam juu ya kile walichokifanya kwa Feisal Salum kumrubuni na kutumia njia za hovyo kumpata akiwa bado na mkataba wa mwaka mmoja na nusu lakini walitetewa na mchezaji alipata watetezi wapuuzi wapuuzi waliokuwa na maslahi na upande ule, sasa basi leo hii kile kile kimewakuta kwa mchezaji ambae bado ana mkataba mrefu kuandika barua ya kuvunja mkataba!
Kwa juu juu unaweza Kuona Kama ni jambo la kawaida lakini nyuma ya Prince Dube Kuna msukumo wa ushawishi Kama ilivyokuwa kwa Feisal, Kuna kisasi kinataka kulipwa hapa kwa njia zile zile na kwa muktadha ule ule!
Na jambo hili litaendelea kwa wachezaji wengine na wengine kwakuwa njia ya kufanya ivyo aliitengeneza Azam mwenyewe hivyo basi wasiweke ugumu wowote kumuachia na michango ya kuvunja mkataba wake tutatoa Kama ilivyokuwa kwa feisal tuwekewe tu account ya bank tuanze mdogo mdogo kuzichanga!