Azam msione aibu kufukuza benchi la ufundi, timu haichezi vizuri

KWa Bangala sawa,ila kwa Fei umeongea kama shabiki wa Yanga mwenye chuki na Feitoto.
 
Coach Dabo hana mbinu
Ngoja ligi ianze acheze na Singida au coast
Wamekupa wachezaji wa maana anashindwa kuwatumia
Hata ukimuangalia FEI Toto hajaongeza kiwango chake kutoka kile alichotokanacho Yanga. Anatumia jitihada binafsi kufanyakazi ambayo ilipaswa kufanywa na washambuliaji.
 
Ligi bado mbichi mkuu
Mkuu mchelea mwana kulia hulia yeye, ngojangoja huumiza matumbo, ajizi ni nyumba ya njaa, chelewachelewa utamkuta mwana si wako, udongo upate ungali maji, samaki mkunje angali mbichi, ukicheka na nyani, mwenye aibu hazai. Wahenga waliona mbali wakaja na misemo hii. Chukua hatua leo kabla hujachelewa.
 
😁😁😁 Haohao walisema Mvumilivu hula mbivu, Penye nia pana njia .
 
😁😁😁 Haohao walisema Mvumilivu hula mbivu, Penye nia pana njia .
Inategemea unavumilia nini, unamvumilia nani, na unavumilia ukiwa wapi. Ukiona watu wameshaanza kukuvua suruali kimbia hakuna mbivu hapo zinazokuja. Dabo kaja siku nyingi na alikutana na uwekezaji mkumbwa. Kapewa Kila alichohitaji kwa maelekezo yake yeye. Kasema anataka aletewe Fei Toto kwa gharama yoyote Ile akaletewa. Lakini nakwambia kama isingekuwa mechi ya Tabora united kucheza pungufu (8) Leo hii wangekuwa wanashiriki CAF confederation cup. Kikosini walichonacho msimu huu sio cha kufungwa goli 4-1 na Yanga, 4 na wydad, kufunga goli 1 na Lyon na APR za Rwanda. Hawashtuki TU bado wanasubiri mbivu?
 
😁😁😁 Noma mkuu ..
 
Timu inabebwa na akamiko kucheza rafu na kuumiza wengine, Fei Toto na kipre kwa juhudi zao binafsi.
Akaminko ni wa kumkanya anaumiza sana wachezaji hata Skudu Makudubela alimkalisha nje, huyu jamaa hafai kucheza ligi yetu ni rafu mwanzo mwisho. Namchukia sana binafsi.

Tukirudi kwenye mada, Azam ni timu bora ila inahitaji haraka mbadala wa Dube, Azam hawana tena goal poacher baada ya Dube kusepa na waliyataka wenyewe kwa kumuiba Feisal wakapewa za uso. Bila kupata namba tisa bora kama Dube Azam hawatoboi ligi zote.
 
Azam ilipokuwa inafukuza makocha nilitamani wamchukue uchebe aliyeijenga Simba ila hawakumuona leo yupo Singida bstars.......unaleta wachezaji unaowasifu ni bora na hawachezi kocha anauwezo mdogo sana wa kufundisha kabumbu.
Kocha mzuri kumbe ni yule anaye watengeneza wachezaji huyu wa Azam fc nadhani yeye anafuata mfumo tu bila kuboresha ujuzi wa mtu mmoja mmoja, (individual skills development)
 
Muombe radhi fei
 
Walipomchukuwa Fei kihuni Walisahau kuwa hakuna mchezaji hapa nchini na Africa mashariki na kati ambae hapendi kucheza Yanga na Simba.

Azam inasuasua hata Dube alipokuwepo huko pia. Shida pale ni kocha na uongozi. Dube na Che Malone wamewarahisishia kazi mashabiki wa Simba na Azam kuwafichilia siri za matokeo mabovu ya timu zao. Kazi ni kwao.
 
Huu ndo ukweli, uwezo wa Dabo na benchi lake umefika kikomo, hana maajabu atayoweza kufanya.
 
Baada ya kutimuliwa kocha wa Coastal atayefata ni Dabo.
 
Kocha mzuri kumbe ni yule anaye watengeza wachezaji huyu wa Azam fc nadhani yeye anafuata mfumo tu bila kuboresha ujuzi wa mtu mmoja mmoja, (individual skills development)
Azam inaenda Rwanda mechi ya marudio wakiwa roho juu. Mechi ya nyumbani kwenye uwanja wako mwenyewe unashindwa kupata ushindi mnono. Angekuwa mm ningemfukuza kocha hapohapo bila kupepesa macho.
 
Azam inaenda Rwanda mechi ya marudio wakiwa roho juu. Mechi ya nyumbani kwenye uwanja wako mwenyewe unashindwa kupata ushindi mnono. Angekuwa mm ningemfukuza kocha hapohapo bila kupepesa macho.
Wakifungwa mafuvu yataamsha bongo lala, binadamu akipata changamoto huamsha ubongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…