Azam msione aibu kufukuza benchi la ufundi, timu haichezi vizuri

Azam hawajawahi kuleta mwenye CV kubwa kwenye mashindano ya Caf....huyu mocha wa Apr ana uzoefu na mashindano kafundisha timu za Al
Mkuu unataka kuniambia kuwa wote waliopita azam hawana CV kubwa? Mbona Nabi alifanya makubwa akiwa na CV ndogo? Na unakumbuka lile kundi la wachezaji wakina Manula,boko,nyoni nk waliokaachwa halafu baadae wakawa tishio sana wakiwa na simba? Vipi kuhusu Mudathir nae?
 
Usajili ni mkubwa lakini timu haiko vizuri kusema ukweli. Hata nafasi hii ya kucheza CAF championship ilitokana na TFF kuruhusu Tabora united yenye wachezaji 8 uwanjani kucheza na Azam na kujipatia pts 3 na magoli meeengiiii yaliyosababisha kuishinda Simba kwa magoli kwenye msimamo wa ligi.

Azam ilifungwa na wydad goli nyingi, ikaifunga Lyon sports kwa shida kagoli kamoja, ikafungwa na Yanga kwa goli nyingi, ikaifunga coastal kwa shida na kuifunga APR kagoli ka kubahatisha. Benchi la ufundi hili halina uwezo mkubwa bhana.

Fukuzeni muanze upya.
Naunga mkono hoja.
 
hapa ndo mstari unacholwa 😂😂
Binafsi sijafurahishwa na Azam kutoka mapema kwenye mashindano haya na timu inayotoka kwenye ligi hafifu kuliko yetu. Nasikitika hata Simba haiko vizuri. Iachane haraka na kisingizio cha timu haina muunganiko, ni timu mpya sijui nini wakati huu ambao tayari mashindano ya CAF na ligi yanaendelea kutimua vumbi. Simba sio timu mpya na mashindano sio mapya, waliyajua kuwa yanakuja na wao watashiriki, wasilete visingizio vya kitoto. Kama kocha hafai wamtimue mapema kabla hajaleta madhara, maana mchezaji na kocha mzuri anahitaji mpira, uwanja mzuri na viatu vya kuchezea TU ili aonyeshe anajua kucheza mpira, hahitaji muda mwingi na muunganiko.
 
Mkuu unataka kuniambia kuwa wote waliopita azam hawana CV kubwa? Mbona Nabi alifanya makubwa akiwa na CV ndogo? Na unakumbuka lile kundi la wachezaji wakina Manula,boko,nyoni nk waliokaachwa halafu baadae wakawa tishio sana wakiwa na simba? Vipi kuhusu Mudathir nae?
Makocha wakubwa ndio namaanisha kama wanaoletwa Simba au Yanga,pia Azam huwezi kusikia wanasajili wachezaji wanaowika afrika kama kina Azizi Ki,Lomalisa,Mayele,Inonga,Pacome wanaletaga wachezaji ambao sio wa viwango vya juu Afrika......huwezi kushinda mataji kwa mwenendo huu.
 
Azam hata wamsaji mchezaji gani anayewika hawawezi kufika popote..Ila timu kuna shida kwenye management...

Na hata makocha wanaowasajili ukiachana na Aliyewahi kuwapa makombe mfululizo Stewart John Hall,wengine wanaowaajiri hua ni Average coaches.
 
NI sahihi uongozi wote wa juu ufumuliwe na kuleta watu professional kwenye soka sio kupeana tu kiundugulization Azam anafanya vizuri kwenye bidhaa zake karibu zote ila anachafuliwa kweye mpira wa miguu.

Unaweza kuona kwa nje ni matajiri kumbe ndani ni maskini kiundeshaji wa timu labda timu ina bajeti ndogo ndio maana hawawezi kuleta makocha wakubwa na wachezaji pia.
 
Kwahiyo tatizo ni wachezaji au kocha? Unataka kuniambia kuwa makocha wote wanaopita azam ni wakawaida?
 
Azam hata wamsaji mchezaji gani anayewika hawawezi kufika popote..Ila timu kuna shida kwenye management...

Na hata makocha wanaowasajili ukiachana na Aliyewahi kuwapa makombe mfululizo Stewart John Hall,wengine wanaowaajiri hua ni Average coaches.
Shida sio makocha
 
NI sahihi uongozi wote wa juu ufumuliwe na kuleta watu professional kwenye soka sio kupeana tu kiundugulization Azam anafanya vizuri kwenye bidhaa zake karibu zote ila anachafuliwa kweye mpira wa miguu.

Unaweza kuona kwa nje ni matajiri kumbe ndani ni maskini kiundeshaji wa timu labda timu ina bajeti ndogo ndio maana hawawezi kuleta makocha wakubwa na wachezaji pia.
Wafanyabiashara wakubwa sana wana madeni makubwa sana pia. Azam sio wa kushindwa kumzuia kipre Jr asiondoke Azam kwa gharama yoyote. Ameenda Columbia kuleta wachezaji rahisi wa daraja LA pili, watashinda vipi?
 
Hawawezi kufanikiwa mpaka wabadilike.
 
Back
Top Bottom