Wanalia hela za bure mzee Bakhresa.Usajili ni mkubwa lakini timu haiko vizuri kusema ukweli. Hata nafasi hii ya kucheza CAF championship ilitokana na TFF kuruhusu Tabora united yenye wachezaji 8 uwanjani kucheza na Azam na kujipatia pts 3 na magoli meeengiiii yaliyosababisha kuishinda Simba kwa magoli kwenye msimamo wa ligi.
Azam ilifungwa na wydad goli nyingi, ikaifunga Lyon sports kwa shida kagoli kamoja, ikafungwa na Yanga kwa goli nyingi, ikaifunga coastal kwa shida na kuifunga APR kagoli ka kubahatisha. Benchi la ufundi hili halina uwezo mkubwa bhana.
Fukuzeni muanze upya.
Mzee una jicho sana la mpira fei huwez kumuwekea namba 10 wala namba nane hata sita kwenye kukaba sio mzuri kijana anajina kubwa lakn haliendani na uwezo wake watu wengi hawajui kuangalia mpira anachojua kijan ni kujiposition ili ashinde ndo magori mengi aliyo funga msimu ule ila kuisaidia tim kutafuta magori kama kiungo hawez zaidi na zaidi atatembea na mpirra katika maeneo yasio na faidaHajui kupanga beki, Bangala hana kasi anapigiwa counter attack kila game ila hambadilishi,
Sidibe beki mzuri akipanda juu hao mabeki wa kati hawawezi kuziba upande wa juu.
Asimwamini sana fei hapo anaweza kucheza mwingine
Huyo fei Taifa stars yetu dhaifu huyo fei anaanzia benchi kwasababu hana ubunifu wa kucheza na striker ni mbinafsi mno, anamchezesha sababu ya presha kwasababu akitoka Yanga
Long term plan misimu 10 mfululizo...Kwa hiyo usajiri woote ule ni kwa ajili ya ligi kuu ? Waste of resources
Tayari kashafukuzwa, tunaongea kwa facts. Ufundi wa Bado ndio umeishia pale, hawezi kufundisha bali anataka wachezaji wanaojifundisha wenyewe au waje wakiwa wameshafundishwa huko watokako.Ligi ndio inaanza, wafukuze benchi zima la ufundi halafu wafundishwe na nani?
Azam wako vizuri, tuwape muda tunaweza kuona mazuri zaidi.