Azam TV badilisheni muda wa kuonesha Tamthilia ya ECILIA (SINOS DEJAN)

dawambili

Member
Joined
Nov 28, 2024
Posts
25
Reaction score
13
Nawapongeza sana Azam TV kwa jitihada zao,ubora wa vipindi na mwonekano wa channel zao hongereni sana.

Nichukue fursa hii kuwaomba uongozi wa media yetu pendwa kubadilisha tamthilia ambayo imeanza kuoneshwa jana usiku majira ya saa mbili 28/11/2024 inayotambulika kwa jina la CECILIA (SINOS DEJAN).

Nimepitia maoni ya wadau wa tamthilia za Azam two kwenye magroup na mitandao mbalimbali,lakini pia nimeitazama hiyo tamthilia episod ya kwanza.

Niwe mkweli siku ya jana nimeaibika mbele ya familia yangu kupitia hii tamthilia na si mimi tu wengi wamelalamika juu ya hilo huko kwenye magroup.

Wakati wa saa mbili familia nyingi huwa ndio wakati wakupata chakula cha usiku wakiwa pamoja na watoto wao au wanafamilia kwa ujumla na kwakuwa Azam TV ni burudani kwa wote familia nyingi muda huo hufungulia Azam two

Imezoeleka hivyo na ushaidi wa hilo ni kupitia kipindi cha tuongee tamthilia kinachoongozwa na MRISHO SENGA kila siku huwahoji watu waina mbalimbali Kutoka sehemu mbalimbali.Idadi kubwa ya watoto wazee na hata vijana Kutoka katika MAKUNDI mbalimbali ya kijamii wanafatilia Azam two na wanazijua hizo tamthilia kiundani .

Kwanini tunaomba mtubadilishie

1: Maadili ya tamthilia husika yako kinyume kabisa na maadili yetu waTanzania. Sote tunajua waMexico hawafanani nasi katika tamaduni hata silka na hilo tumelithibitsha kupitia tamthilia zao zilizokuwa zikiruka katka media nyingine na channel ya Azam one. Je hatuoni kama tunaharibu tamaduni zetu na maadili yetu.

2. Wakati walioweka tamthilia bado watoto wengi wanakuwa hawajalala .Na hata ikitokea wamelala watoto wengi huangalia marudio na ningumu kuwazuia kitu kilochezoeleka,labda uwe na TV mbili na hilo ni gumu Kwa watu wengi wenye uchumi wa chini.

3. Hatujawazoea AZAM two kuleta tamthilia za aina hii kwa wakati huo hivyo inatupa tabu ukizangatia tunalipia hela zetu hivyo tuna haki yakuletewa vitu visivyotulea madhara.
Jana watu wengi wameshika rimoti mkononi ,wengine wakiwafunika watoto wao mito wakizuga kama wanacheza nao ilimradi kukwepa aibu na fedhea ya kutazama watu wakiwa uchi na mbele ya wanao.

4. Kulinda brand yao ,Azam TV wanapaswa kuwa makini sana hususan katika kipindi hiki ambapo wanawashindani wengi sana kibishara na malalamiko yamekuwa mengi upande wao kutokana na kusuasua kwa huduma zao mifano halisi kuna tamthilia nyingi zinarudiwa ,kuna tamthilia nyingi zimekatishwa,vifurushi vimepandishwa bei,ngumi (boxing)hazioneshwi,visimbuzi vya antenna havioneshi maeneo mengi ya mabondeni mfano mburahati.n.k

Hivyo kama kampuni kubwa yenye watu wenye ujuzi wa bishara wanapaswa kufanya tathmini ya kina na kuja na mabadiliko yatakayoondoa kero za wateja wao Ili wasishushe brand yao na hatimae kupotea kama walivyopotea wengine.

*Mwisho niwaombe Azam TV wajue kuwa wanaushawishi mkubwa katika jamii na wanamchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu hivyo wanapaswa kutumia vizuri media yao.

Wasiwe chachu ya MMONYOKO wa maadili nchini ,wawemakini sana hasa kitengo chao cha maudhui kwani huenda kikawa kinalegalega kwa dalili tunazizona.

Tamthilia hii tunaomba ibadilishwe mara moja na si mimi tu ni wadau wote wenye kuitakia kheri Azam TV na kuitakia heri nchi yetu.

 
Mbona azam huwa wanakata sana vipande vya chumbani na wet kiss,hyo jana nini hicho walichoonesha
 
AZAM media kamatieni humo humo. Watu tunataka haya mambo mapemaaaaaaaa. Ww jamaa ukiwa na familia yako unaeza ukaweka ata TBC ukaachana na ulichokisema apo
 
Kwani lazima muangalie kuna channel nyingine kama sinema zetu,cheka plus na nyingine angalieni tuacheni sisi tuangalie muda huo😀😀
 
Kwani lazima muangalie kuna channel nyingine kama sinema zetu,cheka plus na nyingine angalieni tuacheni sisi tuangalie muda huo[emoji3][emoji3]
Hiyo hoja nimejibu kumbuka kuna mazoea na pia watu wanalipia Mimi sijajizungumzia binafsi bimezungumzia majority ya watu
 
TUKIONGEA TUNA FACT HATUROPOKI MBONA HATUJAWAHI KUSEMA JAMBO KAMA HILI?HUKO NYUMA.

Unayeleta hoja watoto wanalala saa mbili je hawawatoto wanohojiwa na MRISHO SENGA wanaishi mbingu ya ngapi?
Jiulize wewe mwenyewe wanao hawafatilii hizo tamthilia au mnajibu kiushabiki?
Ukweli hakuna mtoto anayelala sa mbili kama simgonjwa.
Huu ni wakati WAKULA Kwa familia nyingi.
Nyie shupalieni shingo watakaoharibika sio watoto wabakhresa niwako wewe na wangu mie.
Hatukatai kuoneshwa hii tamthilia tatizo ni muda mbaya Kwa watoto.
Muda na maudhui HAVIENDANI .
Leo Kila mtu kageuka mtoto wake analala saambili,Kila mtu kageuka mwanae haangalii tv ,Leo Kila mtu kageuka anaangalia taarifa ya habari .
Twendeni tutafika tujitoe fahamu,tujitoe akilia ila tujue watoto wanaelekea kuangamia kwakukosa maadili na likioz ndio hiyooooooooooo.Sijui utashinda nyumbani kukontorl rimoti au uende ukasake Hela .
 
USHUHUDA KUTOKA KOMENT YA MDAU MMOJA KWATUKIO LA JANA

"Nilikuwa na waaminia kweli ila mmeniharibia usiku wangu Jana, unaambiwa siku uliyo vaa vibaya ndio unakutana na wakwe, Sasa Jana nipo nimekaa na Mr seblen anatia story huwa kwa kawaida hapendelei sana kukaa sebleni maana hatumpi nafasi ya kutizama tv so huwa anaenda kutizama chumbani, ss Jana story zimemnogea Hadi kipindi kikaanza ss bwana alicho kiona mbona nilibadilishiwa kibao, Azam wamenikeraaaa sanaaa habari ziwafikiee mmetuvunja uwaminifu siwaanini tena looo"
 
MAONI YA MDAU MWENGINE

Inawezekana mnaokoment saa mbili watoto watakuwa wamelela mnakomenti tuu ili mradi,au watoto wenu hamkai nao hapo,mmeshakuza,,,au wengine ni mabechelor....kama tamthilia Ina maudhui ambayo hayafai kwa wa toto,au kukaa kuangalia na wazazi wetu ni bora azam waitoe.....tuna mabint wa KAZI nyumbani ambayo tunawaaachia watoto.....channel wanazoangaalia ni sinema zetu na azam two..maisha ya Sasa yamebadilika jamaniii sio kama tulivyokuwa sisi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…