PUFF DADDY
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 391
- 803
mambo yapo kiganjaniWewe unaangalia nini?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mambo yapo kiganjaniWewe unaangalia nini?
Azam huwa wanajitahidi sana kuhusu maadili iyo imekuwaje tena.Nawapongeza sana Azam TV kwa jitihada zao,ubora wa vipindi na mwonekano wa channel zao hongereni sana.
Nichukue fursa hii kuwaomba uongozi wa media yetu pendwa kubadilisha tamthilia ambayo imeanza kuoneshwa jana usiku majira ya saa mbili 28/11/2024 inayotambulika kwa jina la CECILIA (SINOS DEJAN).
Nimepitia maoni ya wadau wa tamthilia za Azam two kwenye magroup na mitandao mbalimbali,lakini pia nimeitazama hiyo tamthilia episod ya kwanza.
Niwe mkweli siku ya jana nimeaibika mbele ya familia yangu kupitia hii tamthilia na si mimi tu wengi wamelalamika juu ya hilo huko kwenye magroup.
Wakati wa saa mbili familia nyingi huwa ndio wakati wakupata chakula cha usiku wakiwa pamoja na watoto wao au wanafamilia kwa ujumla na kwakuwa Azam TV ni burudani kwa wote familia nyingi muda huo hufungulia Azam two
Imezoeleka hivyo na ushaidi wa hilo ni kupitia kipindi cha tuongee tamthilia kinachoongozwa na MRISHO SENGA kila siku huwahoji watu waina mbalimbali Kutoka sehemu mbalimbali.Idadi kubwa ya watoto wazee na hata vijana Kutoka katika MAKUNDI mbalimbali ya kijamii wanafatilia Azam two na wanazijua hizo tamthilia kiundani .
Kwanini tunaomba mtubadilishie
1: Maadili ya tamthilia husika yako kinyume kabisa na maadili yetu waTanzania. Sote tunajua waMexico hawafanani nasi katika tamaduni hata silka na hilo tumelithibitsha kupitia tamthilia zao zilizokuwa zikiruka katka media nyingine na channel ya Azam one. Je hatuoni kama tunaharibu tamaduni zetu na maadili yetu.
2. Wakati walioweka tamthilia bado watoto wengi wanakuwa hawajalala .Na hata ikitokea wamelala watoto wengi huangalia marudio na ningumu kuwazuia kitu kilochezoeleka,labda uwe na TV mbili na hilo ni gumu Kwa watu wengi wenye uchumi wa chini.
3. Hatujawazoea AZAM two kuleta tamthilia za aina hii kwa wakati huo hivyo inatupa tabu ukizangatia tunalipia hela zetu hivyo tuna haki yakuletewa vitu visivyotulea madhara.
Jana watu wengi wameshika rimoti mkononi ,wengine wakiwafunika watoto wao mito wakizuga kama wanacheza nao ilimradi kukwepa aibu na fedhea ya kutazama watu wakiwa uchi na mbele ya wanao.
4. Kulinda brand yao ,Azam TV wanapaswa kuwa makini sana hususan katika kipindi hiki ambapo wanawashindani wengi sana kibishara na malalamiko yamekuwa mengi upande wao kutokana na kusuasua kwa huduma zao mifano halisi kuna tamthilia nyingi zinarudiwa ,kuna tamthilia nyingi zimekatishwa,vifurushi vimepandishwa bei,ngumi (boxing)hazioneshwi,visimbuzi vya antenna havioneshi maeneo mengi ya mabondeni mfano mburahati.n.k
Hivyo kama kampuni kubwa yenye watu wenye ujuzi wa bishara wanapaswa kufanya tathmini ya kina na kuja na mabadiliko yatakayoondoa kero za wateja wao Ili wasishushe brand yao na hatimae kupotea kama walivyopotea wengine.
*Mwisho niwaombe Azam TV wajue kuwa wanaushawishi mkubwa katika jamii na wanamchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yetu hivyo wanapaswa kutumia vizuri media yao.
Wasiwe chachu ya MMONYOKO wa maadili nchini ,wawemakini sana hasa kitengo chao cha maudhui kwani huenda kikawa kinalegalega kwa dalili tunazizona.
Tamthilia hii tunaomba ibadilishwe mara moja na si mimi tu ni wadau wote wenye kuitakia kheri Azam TV na kuitakia heri nchi yetu.
View attachment 3165044
Ndio washahribika sasaAzam huwa wanajitahidi sana kuhusu maadili iyo imekuwaje tena.
Nashangaa sanaMwanaume unakaaje sebuleni kuangalia tamthilia na watoto.
nina miaka 20 tangu niachane na huu ujinga, ila watu tunatofautiana sana aiseeKwahiyo saa mbili wewe huwa unakaa wapi?
Maana huo ni mud WAKULA chakula cha usiku na familia na Imezoeleka tv huwa on muda huo
Kwa hio kitazama Tv pamoja ndio ujanja? Aisee tunakwama sana sisi Wabongo,Usiwajibu kuna watu humu hawajui hata maana ya family ni nini, watu wako busy siku nzima ni afya family kukaa pamoja na kuangalia vitu pamoja kama family inajenga sana family imara huku mkipata dinner sasa nashangaa mtu anasema unatizama picha na watoto. Sisi kabla ya hii mitandao wazee wetu walikuwa wanataka kila mtu wakati wa dinner awepo nyumbani kuna maana kubwa sana. Sipendi tabia ndani ya nyumba kila mtu yuko kivyake na simu kila jambo lina wakati ila lazima mtenge muda kama family kuwa pamoja na best time ni saa 2 mpaka saa 4 usiku.