Iruru
JF-Expert Member
- Jan 27, 2014
- 1,471
- 2,891
Huu uchambuzi unakusaidia nini? Mnahangauka sana, mwakani tunawasubiria timu ikiwa uwanjani mlete huu uchambuzi.
Ukiangalia wachambuzi wa super sport huwa wanakuwa wapo neutral kwanzia anayefanya marejesho ya video hadi wachambuzi na kuchambua kila aina ya tukio kwa kufuata sheria za soka kwa marejeo ya video juu ya tukio husika. Nimeshangazwa sana na tukio la leo lililoleta utata na ugomvi, kutojadiliwa kabisa eti kisa fundi mitambo kashindwa kufanya marejeo ya video kashindwa kuweka hilo tukio la goli walilofunga Berkane.
Mtangazaji kamuuliza yule dada mchamguzi kuwa goli walilofunga Berkane ni halali au sio halali, yule dada alisema ni goli halali kwavile Kanoute alivunja offside, lakini akaomba apate tena marejeo iili apate kujiridhisha zaidi ila hakuwekewa marejeo ya video. Mchamguzi mwingine naye kaulizwa, akashindwa kutoa majibu kabisa naye akaomba marejeo ya video lakini cha ajabu aliyeko studio kashindwa kuonesha tena marejeo ili wachambuzi waseme kilichoonekana kama ilikuwa ni clear offside au lah Mwisho wa siku waka skip hilo tukio wakajadili ishu zingine kabisa cha ajabu kwenye matukio mengine fundi mitambo anaonesha marejeo ya video.
Watu wengi wanategemea kupata majibu ya maswali kupitia hawa wachambuzi ambao huwa wanaongea kwa kutafsiri tukio vs sheria ya soka. Hata watazamaji pia wapo wenye uelewa wa sheria ila kitu pekee ambacho huwa tunatamani kukiona ni ni replay ya tukio husika na ndio maana warusha matangazo ya mpira wengine matukio yote yenye utata wanaonesha kila kitu kwa ufasaha.