Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Tunaongelea Full Package 225 billion bila kuangalia hiyo miaka 10 yenyewe tutakuwa wapi katika Ramani ya Soka na Mtazamo wa Soka lenyewe kwa Mapana yake.
Kama zabuni ilitangazwa, na yeye ndo akashinda kwa nn tusimpongeze?

Ukwel n kwamba wamejitahid kwa kiasi chao, tusubir iishe tuone tutakuwa wapi, na hii inaweza kuwa n chachu ya kuipandisha thamni ligi ili kuvutia wawekezaji wengine wenye pesa ndefu.
Kwangu mm namuona kama ametake risk kubwa kwa ninavouona mpira wetu.
 
Merchant za klabu Pekee kwa Yanga na Simba Tayari ni Pesa kubwa Sana..
Angalia Simba Day.....
Mwananchi Day .........
Viingilio + Mauzo ya Product zao + Wauze haki yakuonyesha tu hizi Tamasha kwa Tv wanazo zitaka watapa Fedha kiasi Gani.??
Na jiulize tofauti na Simba na yanga ipi event kubwa na kuingiza pesa kwa soka la hapa kwetu?.
Kuna timu zinasubir mechi za Simba na yanga kama chanzo kikubwa cha mapato.
Sasa kwa mantiki hiyo ni kwamba bado hatuna fan base ya kutosha kwa vilabu vidogo ambavyo hata mishahara tuu n tataizo.
 
Kuna Haja Gani ya Kuingia miaka10, kwa nn wasiingie kwa term ya 5yrs then 5yrs Tena? Je thaman ya Fedha ikipolomoka au kukiwa na fiscal cliff Unanilaumu Nani?
 
Kudos kwa hii analysis
 
Kuna Haja Gani ya Kuingia miaka10, kwa nn wasiingie kwa term ya 5yrs then 5yrs Tena? Je thaman ya Fedha ikipolomoka au kukiwa na fiscal cliff Unanilaumu Nani?
Mm sio mtaalamu wa mambo ya uchumi. Lakin nadhani viongozi wa TFF wametumia uzoefu wao katika thamani ya ligi yetu.
Kama mdhamin mkuu anatoa bonasi ambayo haizid mil. 100. Na anagharamia gharama za usafir kwa kila timu. Hatuoni kama Azam kaja kuwa dawa ya kulipa mishahara kwa ile bil 8 kwa vilabu?
Lakin pia wamesema pesa itapanda, kutoka mil 500 kwa mshindi had mil 700.

Jambo la thamani ya pesa kushuka Hilo linahitaji wataalamu wa uchumi pengine wanaweza kulielezea kwa uzuri zaidi.
 
Kuongezea je kulifanyika mchakato wa kushindanisha wazabuni? Maana hata Rioba TBC wangeweza kuifanya. DSTV wanaweza kuleta upinzani sana. Ni pesa ndogo sana hii. TAKUKURU watie miguu.
Mkuu hivi unajitoa ufahamu au? hukuona biders wengine wametajwa? kwa taarifa yako dstv hakubid kabisaa, nikuulize swali, ikiwa wewe ndio muamuzi wa mwisho kwenye tenda, azam kabid kwa 1b na tbc kabid kwa 1.5b utampa nani?
 
Tunaongelea Full Package 225 billion bila kuangalia hiyo miaka 10 yenyewe tutakuwa wapi katika Ramani ya Soka na Mtazamo wa Soka lenyewe kwa Mapana yake.
Kwani kuna mwingine aliyetoa pesa pungufu ya hiyo na akataka mkataba wa miaka mitatu?
 
mzee unachanganya madesa, mshindi wa 5 kupewa milioni 65 ni bonus tu kama vile watakavyompa mshindi wa kwanza mil500, hivi unavyosikia vodacom wanampa bingwa 80m unajua ndio hizo hizo?
 
Hii ni point ya msingi sana mkuu kwa uwekezaji walioufanya azam kiukwel ni mageuz katika soka letu
 
Nchi inaingia mikataba ya miaka 50 watu kimyaa ya Azam mapovu mimi na uhakika leo hii Azam anune tu sitaki tena nakuhakikisha million 500 hawapati nani wa kuwalipa? leo league imekuwa na thamani tu baada ya Azam kuibeba walikuwa wapi kabla ya Azam? Hebu watutajie kampuni moja tu hapa TZ ya kushindana na Azam, watu wako DSTV, hawa DSTV wana miaka mingapi nchi hii walikuwepo kabla hata ya kuzaliwa Azam walichangia nini katika mpira wa TZ, wao wamejikita na soko lao la ndani SA. Leo hii tumevishwa kidogo na Azam tunapendeza katika TV tumeshajiona tuko EPL. Hii league ya humu humu ndani tu tusidanganyane ni kama chips mayai iko Tanzania tu tusione sababu tunapenda sana chips mayai basi Africa nzima wanakula chips mayai. Hii league iko hapa sababu ya Azam siku wakizira tunarudi kule tulikotoka.
 
Ishu sio udogo wala ukubwa
Ishu miaka 10?
DStv akija na ofa mara tatu ya hiyo baaada ya miaka 5 hawawezi vunja mkataba?
Dstv wapo miaka yote waliweka sh ngapi tz harafu hao makaburu hata hatuwataki wanyonyaji tu. Azam waacheni wanafanya kazi nzuri. Wabongo kwa kulinga bila sbb tunapenda sana hv nyie mnaona rahisi kurusha mechi live nchi nzimaaaa
 
Sasa ndugu yangu unataka kufananisha EPL na VPL, ndio wanafanya mnada kwa sababu wahitaji wengi ile ni international brand yaani EPL wanaringa wakifanya mnada na sio wanauza mechi zote wanauza kwa mafungu ikija international wanafanya mnada tena ila mwaka huu wana renew bila bidding sababu ya corona. Huku kwetu unataka mnada kama hajatokea Azam tu na ukifanya mnada Azam si atajua mpinzani ana offer ngapi atapandisha kidogo tu. Hii ni deal kubwa kwa vilabu hakuna yoyote wakuwapa hiyo Simba tu imeuza maisha kwa Billion 20 tu bado ya mkopo Azam analipa kwa mwaka hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…