gigabyte
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 5,717
- 6,465
Kwa hichi walichokifanya Azam nichakupongeza kwa mtu yoyote mwenye akili timamu na mdau wa maendeleo ya soka letu.Kwanza ameipa thamani kubwa ligi yetu bila kuangalia athari zakisiasa kiuchumi na kijamii zinazoweza kujitokeza.Tukubali kua ligi bado haina thamani ya hiyo pesa ila azamu kaamua kuipandisha kwa nguvu hadi hapo.Mkataba wa miaka 10 ni sahihi kabisa kwasababu ili tuje tushuhudie mafanikio ya kweli ya hii pesa ambayo azam kaiwekeza kwenye vilabu vyetu sio chini ya misimu 4 hadi 7.Kwahiyo ligi ikishafika kwenye kiwango bora cha ushindani ndipo tutakapoanza kuona wawekezaji wengine wenye dili kubwa wakijitokeza kuwekeza kwenye vilabu vyetu.Sasa hii ni mwanzo mzuri ngoja tuone tutakapofika.Kwangu nampongeza sana kwa kuthubutu kufanya hiki alichokifanya.