Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Kwa hichi walichokifanya Azam nichakupongeza kwa mtu yoyote mwenye akili timamu na mdau wa maendeleo ya soka letu.Kwanza ameipa thamani kubwa ligi yetu bila kuangalia athari zakisiasa kiuchumi na kijamii zinazoweza kujitokeza.Tukubali kua ligi bado haina thamani ya hiyo pesa ila azamu kaamua kuipandisha kwa nguvu hadi hapo.Mkataba wa miaka 10 ni sahihi kabisa kwasababu ili tuje tushuhudie mafanikio ya kweli ya hii pesa ambayo azam kaiwekeza kwenye vilabu vyetu sio chini ya misimu 4 hadi 7.Kwahiyo ligi ikishafika kwenye kiwango bora cha ushindani ndipo tutakapoanza kuona wawekezaji wengine wenye dili kubwa wakijitokeza kuwekeza kwenye vilabu vyetu.Sasa hii ni mwanzo mzuri ngoja tuone tutakapofika.Kwangu nampongeza sana kwa kuthubutu kufanya hiki alichokifanya.
 
Kumbuka klabu pia zinapata pesa kutoka vodacom, pia tuelezeni kati ya wale biders nani alikuwa yupo tayari kutoa pesa zaidi ya hiyo?
Sijajua kwa kweli..washindaji walikuwa TBC (Starting), Startv(Continental) na wale ATN (TING)
 
Wewe ndiye ng'ombe tena Maksai,thamani ya shilingi inaongezeka kila siku bill 225.6 ya mwaka huu siyo ya mwaka 2029/31 mpaka kufika kipindi hiko hao TFF watakuwa wanaokota machenji change tu hamna kitu.

Mwenye akili angewabana mikataba iwe ya muda mfupi ili kuendana na thamani ya shilingi wakati husika.
Bro..huo mkataba unakipengele cha than a kuongezeka kila mwaka..kwa maelezo yao mpaka kufika mwisho wa.mkataba Bingwa atakuwa anapata milioni 750 as bonaus
 
Bro..huo mkataba unakipengele cha than a kuongezeka kila mwaka..kwa maelezo yao mpaka kufika mwisho wa.mkataba Bingwa atakuwa anapata milioni 750 as bonaus
Sawasawa mkuu umefafanua vizuri,tatizo hapa tunajadili kitu ambacho hatujakisoma wote ila hapa nimeelewa vizuri.
 
Hela ndogo sana hiyo...miaka 10, at least ingekuwa Trilion 1.
Trilion 1 kwenye ligi hii ambayo ndo inathaminishwa sasa hivi.Hizo bil alizozitoa kwa miaka 10 bado ni ela ndefu sana kwa ligi hii ambayo timu zenye ushindani mkubwa ni 2(3).Ligi ambayo mechi kubwa inaweza kuhairishwa masaa machache kabla kwa tamko tu bila sababu za msingi.Changamoto za hii ligi ni nyingi sana kuanzia Tff kwenyewe hadi kwenye vilabu.Kwahiyo wacha kwanza tuone vilabu vyetu vikitumia huu uwekezaji kusimama angalau kiwango chakushawishi wawekezaji wengine wakubwa kuona kuna umuhimu wakuwekeza kwenye hizi timu ndo tuje sasa kuzungumzia kupandisha tena thamani ya ligi na muda wa mkataba.Ila kwa kuanzia sasa Azam anastahili pongezi kubwa.
 
Ishu sio udogo wala ukubwa
Ishu miaka 10?
DStv akija na ofa mara tatu ya hiyo baaada ya miaka 5 hawawezi vunja mkataba?
Kuongezea je kulifanyika mchakato wa kushindanisha wazabuni? Maana hata Rioba TBC wangeweza kuifanya. DSTV wanaweza kuleta upinzani sana. Ni pesa ndogo sana hii. TAKUKURU watie miguu.
 
Hujui kitu wew. Just imagine nafas ya tano atapokea 65ml. Yan iyo hela hata kwa sas iv kwa nauli ya nusu msimu haitoshi alaf TFF wamekubal ilo dili kwa mda wa 10yrs.
Azam amefany mambo makubwa kwasbb lig yetu ilkuwa haijulikan. Lakn ki uhalisia tuko nyuma ya mda.
Tuko nyuma ya muda kwasababu ligi yetu haikua na wawekezaji wakubwa.ndo Azam ameanza sasa na hichi alichokitoa.Ligi yenyewe mdhamini ni changamoto sasa wewe hiyo milioni 65 unaiona ni ndogo wakati kuna timu ata kulipa mishahara haiwezi.Angalia kule mbali miaka ambayo ligi itakua imeshapata ubora ndo uongee mambo mengine ila sio sasa.
 
Wengine wanasema Azam wanapata faida kubwa kuliko Kiasi walichotoa...

Sasa nani Anapenda hasara, Kama akiwa anaingiza Elfu kuni (10000) Eti Aweke Elfu saba (7000) au Sita??? YEYE HATAKI FAIDA?

Kuhusu mkataba kuwa wa miaka 10 sio mbaya kama kuna kipengele cha Kuvunja mkataba kwa Anayetaka kuingia Alipie Gharama za Kuvunja Mkataba.

Lakini tukubali Azam anastahili sababu Mfano tu msimu uliopita Hakukuwa na Mdhamini wa Ligi,. Sasa kama tunapata watu kama AZAM kwa nini Tujiulize mara mbili?
 
Mungu ibariki Azam, watu wanasema tu et thaman ya pesa, hebu watwambie miaka kumi iliyopita ni mdhamin gan alikuja na pesa ya hata bil. 50 kwa miaka hata hii kumi ya sasa.
AZAM kula matunda pengine miaka ijayo tunawezapata zaid yako japo sina uhakika.
Kama kuna kipind ligi ilikosa mdhamini kwa nn tusikubali huyu alokuja na hiki kidogo.?
 
Mungu ibariki Azam, watu wanasema tu et thaman ya pesa, hebu watwambie miaka kumi iliyopita ni mdhamin gan alikuja na pesa ya hata bil. 50 kwa miaka hata hii kumi ya sasa.
AZAM kula matunda pengine miaka ijayo tunawezapata zaid yako japo sina uhakika.
Kama kuna kipind ligi ilikosa mdhamini kwa nn tusikubali huyu alokuja na hiki kidogo.?
Pointless
 
Leta ya kwako tukusikie, usije kuwa unabeza wakati ligi ikikosa mdhamin unailalamikia TFF.
Watu mnatakiwa muangalie Huu mpira kwa Mapana yake tuache ushabiki maandazi. Moo Dewji kila siku anatuambia anawekeza kwa Hasara pale Simba japo naye si mkweli lakini kwa hali ilivyo kuna vitu tunaviona japo kwa uchache wake.
 
Watu mnatakiwa muangalie Huu mpira kwa Mapana yake tuache ushabiki maandazi. Moo Dewji kila siku anatuambia anawekeza kwa Hasara pale Simba japo naye si mkweli lakini kwa hali ilivyo kuna vitu tunaviona japo kwa uchache wake.
Twambie sisi tusiovijua ili tuvijue!
 
Twambie sisi tusiovijua ili tuvijue!
Kitaaluma Mimi ni Mwalimu wa Mpira nausoma mpira na ninajuwa shida za Mpira na Nimeucheza mpira inauma Sana kuona Watu wanadharau hii football industry kwa sababu zao binafsi[emoji22][emoji22]
 
Tunaongelea Full Package 225 billion bila kuangalia hiyo miaka 10 yenyewe tutakuwa wapi katika Ramani ya Soka na Mtazamo wa Soka lenyewe kwa Mapana yake.
 
Merchant za klabu Pekee kwa Yanga na Simba Tayari ni Pesa kubwa Sana..
Angalia Simba Day.....
Mwananchi Day .........
Viingilio + Mauzo ya Product zao + Wauze haki yakuonyesha tu hizi Tamasha kwa Tv wanazo zitaka watapa Fedha kiasi Gani.??
 
Back
Top Bottom