Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

KWANI HIZO TIMU ZINASEMAJE?

Maana miaka mingi imepita haikua hata ikioneshwa kwa runinga, mimi niko na mtazamo chanya nimeifurahia sana hii dili.
Nimapinduzi ya soka baadae tutaenda mbali zaidi wadau wengine wajitokeze itapendeza.
Sasa kwa clubs nao waendelee kujibrand nakujipa dhamani ya juu zaidi wavutie wawekezaji mfano Simba Sc wamalize ishu ya urasimishaji Bil 22 ziekwe mezani, na Yanga nao waendeleze mchakato wawekezaji waweke mpunga, wengine hivyo hivyo . . .

Uchaguzi TFF unakaribia wadau tufanye kweli tuweke watu wa mpira.
.....................................................................................................................................
 
Jambo la Kujiuliza Wanaingia Mkataba Na Vilabu au Tff/Bodi Ya Ligi?
Mfumo wetu wa uendeshaji soka umeshikwa na TFF/Bodi ya Ligi hivyo TFF/Bodi wanafanya kwa niaba vilabu vimeachiwa private Sponsor had pale vilabu vyote vitakapo kua na nguvu ndipo kuna weza kua na sauti ya Vilabu lakini kwa sasa ni vilabu viwili au vitatu ndivyo vinaweza kutunisha msuli.
 
Huu uwekezaji huwa unarudishaje faida? Muwekezaji atarudishaje hela zake? Huwa sielewi, ninaomba kueleweshwa
 
Kwa jinsi waTz tulivyo hata Azam angeweka Trillion Bado wangelaumiwa, Naamini Kuna hasara nyingi tu Azam pia anazipata
Muhimu tu appreciate alichokitoa Azam
 
Azam wanaona mbali sana, wameweka fursa kibindoni kabisa kwa miaka kumi.
 
nimekupata mkuu..kiukweli sitaki kuzungumzia kama tender ilitangazwa ama la maana sijui kama ilitangazwa..sina coment kwenye swala la tender mkuu.
Maoni yako nadhani yana msingi kama haya yalikuwa mazungumzo tu baina ya pande mbili hii litaleta shaka lakini sitaki kuamini hivyo sababu ni kinyume na ushindani. Kitu pekee nataka kuamini kulikuwa na tender ya uwazi. Kwenye suala hili hasa la mpira nadhani commercial inaweza kuwa 70% tech 30% ila mimi sijui kama tender ilitangazwa au hapana ila kama ilitangazwa na kashinda basi hakuna shaka katika hili.
 
Waacheni Azam wale matunda ya kazi yao. Wao ndio wamelileta soka letu lilipo sasa kwa kuliongezea thamani. Na zaidi walichukua risk kubwa awali.

Binafsi, ni Azam wamenifanya kutazama mechi nyingine tofauti na Yanga na Simba. Hata wakicheza Kagera na Polisi ninatazama. Pili, wamenifanya kuwa mfuatiliaji wa soka la nyumbani. Kwa dhati kabisa nasema ni muda wao Azam kuvuna. After 10 years watakaa na kuona. Si kila kitu tupinge na kujadili kiwapesi kama kujumlisha na kutoa.

Uchumi wetu bado sio stable kiufupi ni unpredictable - hii ni risk nyingine lazima itazamwe kwa projection za miaka 10 ya mkataba. Tukumbuke hii miaka 5 ya mwendazake kampuni nyingi zimeumia na kuumizwa. Kiufupi natoa baraka zote kwa hii deal kwa Azam.
 
Kwa jinsi waTz tulivyo hata Azam angeweka Trillion Bado wangelaumiwa, Naamini Kuna hasara nyingi tu Azam pia anazipata
Mihimu tu appreciate alichokitoa Azam
Kwa mfano hasara gani...yaani mtu apate hasara afu akuwekee mzigo kama huo.?

Unadhani Azam alikurupuka kuweka hiyo hela. Mpira unalipa, leo unaona timu zinapambana kuwekeza, unadhani kutakuwa kuna shida hapo.?
 
Katika kugawana pesa team zote hapa ndio TFF walitakiwa waweke wazi ili kuzisaidia team zote. Nadhani wangeiga mfumo wa EPL japo sio kila kitu ila wangechukuwa mfumo huo kwa maana kila aliye kwenye VPL haijalishi nafasi ya ngapi kuna kiasi unapewa halafu ziada inategemea kama game yako itakuwa live au game itakayokuwa inatizamwa na watu wengi unapata zaidi ukiondoa na zawadi ya wa kwanza mpaka wa 4 hii italeta ushindani mkubwa na kuzisaidia team ndogo kuweza kulipa vizuri wachezaji wao. TFF na Board ya league wanatakiwa waweke wazi pesa hizi zitanufaisha vipi team kwa ujumla na mgao utakuwa namna gani. Maana 22 Billion kwa mwaka sio pesa ndogo na kuna wadhamini wengine wadogo watasaidia ili ukiviwezesha vilabu ndio league inakuwa bora na thamani yake itapanda ila yakija yake magumashi tena mnagawa 10 billion tu zingine matumizi ya kawaida hapo vilabu visikubali kabisa team za VPL zipate mgao mkubwa na pesa kidogo sana ziende kuendesha au kusaidia TFF sio tena pesa ya VPL inaenda team ya Taifa hii haihusu, pesa ya VPL iwe kama kampuni team za VPL wawe ndio wanahisa tu copy mfumo wa EPL ndio maana team ya mwisho EPL unaweza kukuta wanapesa kuliko team ya 4 La liga. Team zikiwa na pesa zita invest pia huku chini kwa wachezaji wadogo baada ya miaka 10 unakuta team kama Mbeya city wanaweza kuleta wachezaji wazuri. Kitu kimoja team za jeshi hapana kama jeshi wawe na team moja tu hakuna sijui JKT Ruvu, Ruvu shooting, Prison, Police sijui nini Orjoro hapana hawa wanaturudisha nyuma.
 
Miaka 10 ni muda mrefu sana ni rahisi sana kulaliwa wamekurupuka sana Azam atafaidika sana na hakuta kuwa na ushindani kwake ambao ungeleta tija zaidi kwa vilabu miaka ya mbele
 
Patamu hapo ... Voda akitia hata na yeye hata 15-20 si mbaya kuanzia
 
Kwa mfano hasara gani...yaani mtu apate hasara afu akuwekee mzigo kama huo.?

Unadhani Azam alikurupuka kuweka hiyo hela. Mpira unalipa,leo unaona timu zinapambana kuwekeza,unadhani kutakuwa kunashida hapo.
Biashara yoyote Kuna faida na hasara, na ile ni biashara, siwez kutaja hasara anazozipata Mimi sio mtaalam wa sekta hiyo.
Azam hajakurupuka anawataalam wengi wanamshauri.

Labda wewe ungekuwa mdhani ungeweka dau gani?
 
HV Kenya ikoje kwenye biashara za namna hii ktk soka lao ...
Ila niseme tu kuwa moo wa Simba asilaumiwe kwa vile yeye anaendeasha hyo club kwapassion tu CYO Kama inamalipa Sana leo moo akijitoaa tu simba. Utaona simbaitakavyo yumba kwa vile wanachama Ni wachache Sana wanao weza kuchangishanaa Ila kwa moo wamuachee
 
Upo sawa mkuu, kuongozea hapo Azam anasaidia kuongeza mzunguko wa fedha, iwapo hizi timu zetu za mikoa wachezaji watalipwa ipasavyo itasaidia sana mzunguko mikoa yenye timu katika ligi kuu
 
Kumwaga pesa kwa Mo kwa clab ya Simba imechochea sana Azam pia kuongeza dau hili la la, kujitoa kwa Mo haya ndio matokeo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…