Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

No way hakuna Faida short term hapo,

Mfano mwengine nakupa
Kwese (zaidi ya milioni 200 wapo) wamelipa 34m usd around bilioni 80 kuonesha world cup, hii ni sawa na Bilioni 20 kwa population yetu ama rahisi zaidi.

Unafikiri Ligi ya Tanzania ina thamani hiyo?

Na ligi zote za Nje camera na broadcast nzima hufanywa na wa andaa mashindano, Bongo ni Azam wenyewe wanafanya viwanja hata camera havina.

Azam hapati faida hapa atleast short term, kama kuna mtu Ana data alete, tusipigane kamba aisee.

Ligi zote Rwanda, Kenya, Uganda anadhamini Azam na Kote analipa bilioni Around 4, kwetu tu Ndio Bilioni 20.
 
TFF na Bodi ya Ligi wameingizwa choo cha kike, huwezi kuingia mkataba muda mrefu namna hiyo lakini kitu kingine sidhani kama walipokuwa wanatangaza tenda walitangaza utakuwa mkataba wa miaka 10. Ilitakiwa angalau uwe mkataba wa miaka mitano ili kusudi wanapotaka kungia mkataba mwingine wafanye evaluation ya mkataba uliopita.

Pia nimeona vilabu ambao ni wanufaika watapata asilimia 67 na vilabu vinachekelea bila kuangalia vilabu ndio vinabeba gharama kubwa kuliko wadau wengine.
 
Bado na matangazo, aisee wanapiga helaa
 
DStv walikuwa na subscribers 400,000 wakati Azam walikuwa nao 200,000..
Startimes ndo walikuwa nao zaidi ya milioni..

Kama azam inawalipa why DStv isiwalipe?
Startimes je??
Hujui ulisemalo. Subscribers laki 4 [emoji23][emoji23]. walikuja hapa kufanya utafiti wa kuinyesha games 4 au 5 nadhani 2011 au 2012 wakasepa mazima hawajawahi hata kutoa ofa tena walichogundua ndo kilichowakimbiza.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Lakini Kwese si imeshakufa?

Au bado ipo
 

Azam ana subscribers wangapi?
Dstv?
Startimes?
 
Azam ni wakati wake wa kula mavuno, alirisk kipindi hicho hamna anaetamani ligi ya bongo wakiwemo hao DSTV. Now ligi ishakuwa brand kubwa mnaanza kumchukulia poa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Japo na mimi ni mfuasi wa mitano tena ila umeongea kweli mkuu hapo nyuma kidogo hawa akina DSTV sijui kina nani hawakutamani hata kujua kama kuna ligi yetu hapa.

Walidharau pakubwa leo mtu kaja kaitoa gizani ligi yetu tena kaanzia matopeni kwenye risk kubwa kawekeza pakubwa leo ligi inafuatiliwa hamasa imekuwa kubwa tumeanza kumbeza Azam media tumesahau alikotutoa.

Sio poa kabisa alipotutoa ni mbali mno mafanikio tunayoyapata leo hata kwenye vilabu vyetu financially hata kukuwa kwa mpira wetu 75% yamekuzwa na Azam media nishauri wadau husika waingie kufanya resech kwanza ndio waje na mkataba mzuri ili kila upande unufaike ili baadae isije kusa azam alitupiga pakubwa.
 

Upo sahihi ila watu tunajudge hiyo miaka 10 na ukizingatia kila siku bidhaa hiyo inaongezeka thamani pamoja na gharama za uendeshaji kwa vilabu, nafikiri wengi mnakimbilia kuangalia bonus kwa bingwa atapata nini na anaemfuatia na kwa mbaali yule mshindi wa tatu ambavyo bila shaka katika kipindi hicho cha miaka 10 timu 3 ambazo wote tunazifahamu uenda zikabadilishana tu nafasi hizo hizo karibia miaka 9 hivi kama sio miaka yote.

Vipi kwa zile timu zingine ndogo katika Ligi Kuu ambapo sio ajabu pesa hizo watakazo gaiwiwa ndo wakawa wanaingiza kama chanzo chao kikubwa cha mapato ukilinganisha na udhamini mwingine watakao kuwa nao kwasababu hizi timu zinakuwaga na wadhamini wachache ambao pia wanawapa dau kidogo au mara nyingine wanakosa kabisa wadhamini ukilinganisha na hao wakubwa?!

Ambao sio ajabu ukakuta kiasi cha pesa watakachopata plus na bonus hizo ukikiweka kwenye mzani unaweza kuta thamani yake inashika nafasi ya 3 na kuendelea katika chanzo cha mapato klabuni.
 
Mkuu, mkataba wa Azam ni wa kuonyesha mpira Kama mdau wa sekta ya utangazaji (TV)

Bado sekta nyingine zina nafasi k.v vinywaji, mawasiliano,utalii n.k katika kutangaza biashara zao.
 
Kisimbuzi cha Azam kinauzwa Malawi, Uganda na hapa Kenya pia.
 
League yetu ni Simba na Yanga tu.

Pesa ya viingilio inakusanywa nyingi ikitokea timu inacheza na Simba au Yanga.
 
Vodacom wanafadhili league kama hisani tu. Makampuni mengi kibongo bongo hayana stiff competition kwamba mpaka wafanye promotion kubwa ndio mambo yaende.

Ndio maana walishawahi kujitoa, hakuna aliyeingia mpaka wakaamua wenyewe kurudi.
Yaani bongo population ni kubwa lakini hamna biashara za ushindani yaani unashangaa hadi media kubwa hazina matangazo ya kuwafanya waendeshe vituo vyao kwa faida kubwa na kwa ubora.. wanafika kujilizaliza kuomba matangazo.

Hakuna stiff competition kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…