Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Ni kweli mkuu...lakini hujajiuliza growth rate ya soko la ving'amuzi vya azam itakayokuwa influenced na uoneshaji wa soka....na hiyo growth rate ni dynamic as it changes yearly, umewaza hicho?

Point yetu ni kuwa..kwa namna moja ama nyingineaazam anapata faida ndio maana hata kaamua kuwekeza, lakini pia anapata/atapata faida kubwa kuliko thamani ya mkataba..ni either mkataba ufupishwe au thamani yake iongezwe.
No way hakuna Faida short term hapo,

Mfano mwengine nakupa
Kwese (zaidi ya milioni 200 wapo) wamelipa 34m usd around bilioni 80 kuonesha world cup, hii ni sawa na Bilioni 20 kwa population yetu ama rahisi zaidi.

Unafikiri Ligi ya Tanzania ina thamani hiyo?

Na ligi zote za Nje camera na broadcast nzima hufanywa na wa andaa mashindano, Bongo ni Azam wenyewe wanafanya viwanja hata camera havina.

Azam hapati faida hapa atleast short term, kama kuna mtu Ana data alete, tusipigane kamba aisee.

Ligi zote Rwanda, Kenya, Uganda anadhamini Azam na Kote analipa bilioni Around 4, kwetu tu Ndio Bilioni 20.
 
TFF na Bodi ya Ligi wameingizwa choo cha kike, huwezi kuingia mkataba muda mrefu namna hiyo lakini kitu kingine sidhani kama walipokuwa wanatangaza tenda walitangaza utakuwa mkataba wa miaka 10. Ilitakiwa angalau uwe mkataba wa miaka mitano ili kusudi wanapotaka kungia mkataba mwingine wafanye evaluation ya mkataba uliopita.

Pia nimeona vilabu ambao ni wanufaika watapata asilimia 67 na vilabu vinachekelea bila kuangalia vilabu ndio vinabeba gharama kubwa kuliko wadau wengine.
 
Mkuu umetumia busara sana kuhitaji arguments za sisi tunaoona pesa ni ndogo...Iko hivi

1. Umewahi kujiuliza ni vibanda umiza vingapi, watanzania wangapi na lounge au lodge ngapi zinazolipia kile kifurushi ili tu kuangalia mpira (hapa naongelea active customers)..achana na channel zingine.

Mfano, tuweke makadirio ya chini..wenye ving'amuzi nchi nzima ni Milioni moja...na tuweke makadirio ya chini tu kuwa kifurushi kwa mwezi ni elfu kumi.

so, mapato kwa mwezi 1 tu ni 1,000,000 * 10,000 = 10,000,000,000 (bilion 10) ambayo ni sawa na Bilion 80 kwa mwaka (nimepiga mahesabu tu ya ile miezi 8 ambayo ligi inakuwa active)..Hapo sijaongelea wateja wapya wanaonunua ving'amuzi vyao kwasababu tu ili waone mechi za vpl.

Kumbuka hapo bei halisi sio 10k (kwa sasa ni 20k) na wateja wanaohitaji kuangalia mechi ni zaidi ya 1m...Hapa lets assume ile gharama nyingine ya king'amuzi na idadi ya nyongeza ya wateja (10,000 * 500,000 = 5b kwa mwezi), mapato yao yatatumika kwenye kucover costs of operations..

2. Channel zao zinazoonesha mechi zitapata matangazo ya wadhamini wengi sana...kama ambavyo hawa wauza solar wanatangaza kwenye hizi channel...

3. Miaka 10 ni muda mrefu sana, ndani ya huo muda usitegemee gharama ya kulipia vifurushi itabaki constant (20k per month).. Kuna expectation kubwa kuwa itapanda maana demand ya service inaongezeka...hapo faida itakuwa maradufu.

Risk pekee kwa azam ni endapo majanga kama haya ya covid yatatokea (siombei yatokee).

Wengine wataongezea.
Bado na matangazo, aisee wanapiga helaa
 
DStv walikuwa na subscribers 400,000 wakati Azam walikuwa nao 200,000..
Startimes ndo walikuwa nao zaidi ya milioni..

Kama azam inawalipa why DStv isiwalipe?
Startimes je??
Hujui ulisemalo. Subscribers laki 4 [emoji23][emoji23]. walikuja hapa kufanya utafiti wa kuinyesha games 4 au 5 nadhani 2011 au 2012 wakasepa mazima hawajawahi hata kutoa ofa tena walichogundua ndo kilichowakimbiza.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
No way hakuna Faida short term hapo,

Mfano mwengine nakupa
Kwese (zaidi ya milioni 200 wapo) wamelipa 34m usd around bilioni 80 kuonesha world cup, hii ni sawa na Bilioni 20 kwa population yetu ama rahisi zaidi.

Unafkiri Ligi ya Tanzania ina thamani hio?

Na ligi zote za Nje camera na broadcast nzima hufanywa na wa andaa mashindano, Bongo ni Azam wenyewe wanafanya viwanja hata camera havina.

Azam hapati faida hapa atleast short term, kama kuna mtu Ana data alete, tusipigane kamba aisee.

Ligi zote Rwanda, kenya, Uganda anadhamini Azam na Kote analipa bilioni Around 4, kwetu tu Ndio Bilioni 20.
Lakini Kwese si imeshakufa?

Au bado ipo
 
Hujui ulisemalo. Subscribers laki 4 [emoji23][emoji23]. walikuja hapa kufanya utafiti wa kuinyesha games 4 au 5 nadhani 2011 au 2012 wakasepa mazima hawajawahi hata kutoa ofa tena walichogundua ndo kilichowakimbiza.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app

Azam ana subscribers wangapi?
Dstv?
Startimes?
 
Azam ni wakati wake wa kula mavuno, alirisk kipindi hicho hamna anaetamani ligi ya bongo wakiwemo hao DSTV. Now ligi ishakuwa brand kubwa mnaanza kumchukulia poa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Japo na mimi ni mfuasi wa mitano tena ila umeongea kweli mkuu hapo nyuma kidogo hawa akina DSTV sijui kina nani hawakutamani hata kujua kama kuna ligi yetu hapa.

Walidharau pakubwa leo mtu kaja kaitoa gizani ligi yetu tena kaanzia matopeni kwenye risk kubwa kawekeza pakubwa leo ligi inafuatiliwa hamasa imekuwa kubwa tumeanza kumbeza Azam media tumesahau alikotutoa.

Sio poa kabisa alipotutoa ni mbali mno mafanikio tunayoyapata leo hata kwenye vilabu vyetu financially hata kukuwa kwa mpira wetu 75% yamekuzwa na Azam media nishauri wadau husika waingie kufanya resech kwanza ndio waje na mkataba mzuri ili kila upande unufaike ili baadae isije kusa azam alitupiga pakubwa.
 
Kaka hata kwa hesabu ndogo kiasi gani hio sio pesa ndogo imagine simba ndio club yenye mkataba mnono kwa sasa na ana ana mkataba wa billion 2.5 per year toka vunja bei sasa chukua bilion 225 gawanya kwa mwaka unapata bilion 22.5.

Zigawe kwa vilabu 16 vitavocheza ligi kuu msimu ujao unapata karibia billion 1.5 kwa club sasa unakuaje mkataba mdogo tena wenye kuwa na muda wa miaka 10 na ukizingatia ligi yetu kiuhalisia ni chenga na utopolo mtupu.

Tuwape hongera Azam kwa kutufikisha Hapa mwaka 2011 kurudi ulikua huwez hata kuona mechi yoyote bongo labda Simba na Yanga tena kwa low quality na nina uhakika tulikua hatuoni madudu ya marefa na ubovu was team za ligi ilikua ni ukanjanja mtupu kabla.

Azam media group wamefanya makubwa hata kuwa na team nzuri hata huo ubora simba na yanga wanajisifu nao Azam wamechangia pakubwa mno.

Upo sahihi ila watu tunajudge hiyo miaka 10 na ukizingatia kila siku bidhaa hiyo inaongezeka thamani pamoja na gharama za uendeshaji kwa vilabu, nafikiri wengi mnakimbilia kuangalia bonus kwa bingwa atapata nini na anaemfuatia na kwa mbaali yule mshindi wa tatu ambavyo bila shaka katika kipindi hicho cha miaka 10 timu 3 ambazo wote tunazifahamu uenda zikabadilishana tu nafasi hizo hizo karibia miaka 9 hivi kama sio miaka yote.

Vipi kwa zile timu zingine ndogo katika Ligi Kuu ambapo sio ajabu pesa hizo watakazo gaiwiwa ndo wakawa wanaingiza kama chanzo chao kikubwa cha mapato ukilinganisha na udhamini mwingine watakao kuwa nao kwasababu hizi timu zinakuwaga na wadhamini wachache ambao pia wanawapa dau kidogo au mara nyingine wanakosa kabisa wadhamini ukilinganisha na hao wakubwa?!

Ambao sio ajabu ukakuta kiasi cha pesa watakachopata plus na bonus hizo ukikiweka kwenye mzani unaweza kuta thamani yake inashika nafasi ya 3 na kuendelea katika chanzo cha mapato klabuni.
 
Mkuu umetumia busara sana kuhitaji arguments za sisi tunaoona pesa ni ndogo...Iko hivi

1. Umewahi kujiuliza ni vibanda umiza vingapi, watanzania wangapi na lounge au lodge ngapi zinazolipia kile kifurushi ili tu kuangalia mpira (hapa naongelea active customers)..achana na channel zingine.

Mfano, tuweke makadirio ya chini..wenye ving'amuzi nchi nzima ni Milioni moja...na tuweke makadirio ya chini tu kuwa kifurushi kwa mwezi ni elfu kumi.

so, mapato kwa mwezi 1 tu ni 1,000,000 * 10,000 = 10,000,000,000 (bilion 10) ambayo ni sawa na Bilion 80 kwa mwaka (nimepiga mahesabu tu ya ile miezi 8 ambayo ligi inakuwa active)..Hapo sijaongelea wateja wapya wanaonunua ving'amuzi vyao kwasababu tu ili waone mechi za vpl.

Kumbuka hapo bei halisi sio 10k (kwa sasa ni 20k) na wateja wanaohitaji kuangalia mechi ni zaidi ya 1m...Hapa lets assume ile gharama nyingine ya king'amuzi na idadi ya nyongeza ya wateja (10,000 * 500,000 = 5b kwa mwezi), mapato yao yatatumika kwenye kucover costs of operations..

2. Channel zao zinazoonesha mechi zitapata matangazo ya wadhamini wengi sana...kama ambavyo hawa wauza solar wanatangaza kwenye hizi channel...

3. Miaka 10 ni muda mrefu sana, ndani ya huo muda usitegemee gharama ya kulipia vifurushi itabaki constant (20k per month).. Kuna expectation kubwa kuwa itapanda maana demand ya service inaongezeka...hapo faida itakuwa maradufu.

Risk pekee kwa azam ni endapo majanga kama haya ya covid yatatokea (siombei yatokee).

Wengine wataongezea.
Mkuu, mkataba wa Azam ni wa kuonyesha mpira Kama mdau wa sekta ya utangazaji (TV)

Bado sekta nyingine zina nafasi k.v vinywaji, mawasiliano,utalii n.k katika kutangaza biashara zao.
 
timu zetu zikiendelea kufanya vizuri sana michuano ya kimataifa basi bila shaka kutakua na uhitaji wa kuuza rights za kuonesha mpira nje ya nchi,...... (hatujui hiki kipengele wamekiweka vipi)

Ni afadhali kama Azam kapewa rights za ndani pekee, ila kama kapewa mpaka za nje ya nchi basi itakua ni bonge moja la kosa bodi ya ligi wamefanya.....!

Lakini pia, in the next 5 years sidhani kama uchumi wetu kama nchi utabaki hapa hapa, hivyo azam atauza ving'amuzi vyake vingi sana na atapata matangazo mengi sana ya kibiashara!
Kisimbuzi cha Azam kinauzwa Malawi, Uganda na hapa Kenya pia.
 
Data nyengine hizi, hii mechi baina ya Ruvu shooting na Prison iliingiza kiingilio 245,000 mechi nzima, then watu wanakwambia Bilioni 22 ni ndogo

Kwenye mgawanyo Prison wa kapata 32,000 😂, serious dah.

Azam anatoa tu sadaka.
League yetu ni Simba na Yanga tu.

Pesa ya viingilio inakusanywa nyingi ikitokea timu inacheza na Simba au Yanga.
 
Vodacom wanafadhili league kama hisani tu. Makampuni mengi kibongo bongo hayana stiff competition kwamba mpaka wafanye promotion kubwa ndio mambo yaende.

Ndio maana walishawahi kujitoa, hakuna aliyeingia mpaka wakaamua wenyewe kurudi.
Yaani bongo population ni kubwa lakini hamna biashara za ushindani yaani unashangaa hadi media kubwa hazina matangazo ya kuwafanya waendeshe vituo vyao kwa faida kubwa na kwa ubora.. wanafika kujilizaliza kuomba matangazo.

Hakuna stiff competition kabisa.
 
Back
Top Bottom