Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Azam TV Limited yaingia mkataba wa kuonesha Matangazo ya Ligi Kuu kwa miaka 10. Mshindi misimu mitatu ijayo kulamba bonus Tsh 500m

Kaka hata kwa hesabu ndogo kiasi gani hio sio pesa ndogo imagine simba ndio club yenye mkataba mnono kwa sasa na ana ana mkataba wa billion 2.5 per year toka vunja bei sasa chukua bilion 225 gawanya kwa mwaka unapata bilion 22.5.

Zigawe kwa vilabu 16 vitavocheza ligi kuu msimu ujao unapata karibia billion 1.5 kwa club sasa unakuaje mkataba mdogo tena wenye kuwa na muda wa miaka 10 na ukizingatia ligi yetu kiuhalisia ni chenga na utopolo mtupu.

Tuwape hongera Azam kwa kutufikisha Hapa mwaka 2011 kurudi ulikua huwez hata kuona mechi yoyote bongo labda Simba na Yanga tena kwa low quality na nina uhakika tulikua hatuoni madudu ya marefa na ubovu was team za ligi ilikua ni ukanjanja mtupu kabla.

Azam media group wamefanya makubwa hata kuwa na team nzuri hata huo ubora simba na yanga wanajisifu nao Azam wamechangia pakubwa mno.
Broo..kwa.mwaka kila.klabu zitapata bilioni 8 zote kwa pamoja ..ndio zitagawana..hio..pia Kuna waamuzi hapo hapo nk..pi
 
Tena sio kidogo. Kutoka bil5 kwa miaka mitano hadi kukubali bil200+ kwa miaka 10. Aisee unaona hilo gape. Sasa pata picha washapiga hesabu wataingiza shingapi.
Wakianza kuonesha na ligi daraja la kwanza itapendeza zaidi
 
Kiukweli dili Ni nzuri..lakini miaka 10 imetia doa..kusaini miaka 10 Ni sawa na mkataba wa Carl Peter's na chief mangungo wa msovero..
 
Hicho kiasi kinatakiwa kiongezeke kila mwaka, sio kinabaki hapo hapo, naamini Azam wameshaona kumiliki haki za kutusha matangazo ya ligi kuu kunawalipa sasa wameamua kukomaa, inatakiwa hao bodi ya ligi na TFF waamke wajue ku negotiate, wakizubaa wataliwa.
Watu wanakurupuka tuu ndio maana hapo wamesema miaka 3 ijayo timu zitapata hicho kiasi but baada ya hapo kuna kiasi kitaongezeka
 
Kaka kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa competition, imagine Azama katoa hela yote hio wakati hakuna hata kampuni moja inayoweza kuwekeza kuonesha VPL achilia mbali hata kutamani ko Azam hata iwaje wanastahili pongezi ukizingatia deal lenyewe limeenda mara zaid ya 10
Mikampuni uchwara imekuwepo miaka yote hakuna hata moja imejitokeza kufadhili sasa bora hawa azam wapewe exclusive kabisaa
 
Kwa nature ya hii biashara (Haki za kuonesha mpira) ilivyo ni ngumu sana investors wawili kuexist kwa pamoja..Lazima mmoja afe..kwasababu

Market bado ni dogo sana kuhitaji two suppliers...Gharama za kuendesha biashara zinakuwa juu kuliko faida mtakayogawana..chukulia mfano kwenye soko la ving'amuzi tu..kuna kampuni zingine naamini zinapata faida ndogo sana au inawezekana zinapata loss kwasababu tayari soko ni dogo halitoshi watu wawili..Kuna aina za ving'amuzi huwa nazisikia tu redioni ila hadi leo sijawahi kuviona vinatumika majumbani..vipo ila wateja ni wachache sana.

sasa Ukimuweka AZAM na DSTV kwa ligi moja ya bongo na ambayo market 99.5% ipo bongo lazima wagawane faida na mmoja lazima aanguke maana cost of production ni kubwa kuliko market share.

Najua utakuwa unajiuliza kwanini kuna TIGO, VODA, AIRTEL, HALOTEL, ZANTEL n.k at the same time na wote wanapata faida...Jibu ni rahisi tu kuwa market ni kubwa (zaidi ya watu 30m wanatumia simu) na unakuta mtu mmoja anamiliki line zote...ila watu wanaomiliki ving'amuzi viwili kwa pamoja ni wachache sana kutokana na per capital income za raia.

So, kwa hii biashara ya kuonesha mpira wa ligi ya bongo (taking into consideration the current situation) ni ngumu sana sana sana DSTV na AZAM kuonesha kwa pamoja...Kwanza kati yao hakuna atakaekubali...Kitu pekee ambacho watakubali kufanya ni kugombania tender tu ila sio kuonesha kwa pamoja..

Ndio maana watu wanalalamika miaka 10 ni mingi sana ilibidi iwe michache ili kutoa nafasi kwa bidders kugombania tenda na TFF pamoja na vilabu kuzidi kupata masilahi mazuri. Hii ya mtu mmoja kumiliki soko kwa 10yrs inaua ubunifu.

swali fikirishi kidogo kwako mkuu:

Yule MO kama mjasiriamali, unadhani hajaiona fursa kwenye kuonesha soka?, unadhani anashindwa kuanzisha channel yake ili aoneshe?..Anaweza 100% ila tatizo soko automatically haliruhusu more than one supplier/producer...

Otherwise angekuwa tayari kuanzisha TV ili agombee tender lakini ndo hivo miaka 10 inabidi abaki na idea + ubunifu kichwani.....TFF wamefeli sana.
Voda ametangaza losses
 
TFF nao wameanza issue km za Serikali na mikataba mireefu...mkataba ni mzuri ila uwe wa muda mfupi mfupi...mkataba wa muda mrefu ni kuzinyima kampuni nyingine fursa ht km ni watatoa dau kubwa...Otherwise kampuni nyingine itabidi ziilipe azam kupata rights, then azam atakua anakula cha juu km middle man.
Mkataba ukiwa mfupi hakuna atakaekubali kutoa hayo mapesa mengi hayupo, azam hawezi weka pesa zote hizo eti kwa miaka 5.

Kumbuka hapo anajaribu kuziinua timu ziwe shindani na zisiuze mechi.

Pili ligi ikiwa imara ndio nae atauza ila kinyume chake hakuna kitu kama hicho
 
Azam kaona mbali DSTV anachukua haki za EPL Africa kwa muda mrefu ili kuzuia ushindaji lakini tujiulize kwa nini to AZAM tv alipoingia kurusha mpira kumekua na mabadiliko makubwa sana.Tuthamini vya kwetu huyo DSTV amekuja na kutoka mara nyingi na target yake kubwa ilikuwa mechi ya Simba v Yanga tu.Yani tutazame wageni wasiojali kama Njombe FC,Mbeya kwanza,Gwambina nk.Heko kwa azam.Vodacom nao ni muda wa kuboresha kifurushi kama kweli wanajiita wadhamini wakuu.Imani baada ya Azam kua seroius na Business na wadhamini wengine watakua serious,Serikali na CCM watakua seroius kwenye miundo mbinu.
Sijui hao washenzi wanaolilia DStv kama ni ya baba zao pumbavu,bora kampuni yetu mambo yakiwa mazuri wanaweza nunua East Africa yote
 
unapenda vitu vya muda mfupi mfupi kama mikataba ya simba na yanga.Ndio maana hatuendelei kwa kua tunataka kufurahia leo leo tu.
Saizi timu zitakuwa confidence na haziyauza mechi kishenzi. Heko Azam rusha na ligi daraja la kwanza
 
1.data Za Tcra kuna Madishi 1.1m Tanzania nzima, hapa Angalia

Ni data za mwaka uliopita, hio 1.1m ni wote DSTV, Zuku, Azam na wengineo.

Hivyo kuna uwezekano Azam hana 1m monthly subscribers.

2. Kama Data zako zipo sahihi anapata 80B kwa mwaka still kutoa 22B kudhamini ligi ni kubwa sana Kibiashara.
-Uganda azam analipa around 4B tsh
-kenya kila timu wanapewa ksh 10m ambayo ni around milioni 200 tsh.

Kwa East Africa hakuna anaepata kama sisi.

Si hivyo tu, hata ukiangalia makampuni ya Kimataifa dstv analipa epl around 200m akiwa na Pato la around 2B kwa mwaka ambayo roughly ni kama 10% ya Pato lake.

Hio 22B ni ligi Ya Tanzania tu, bado analipa Ligi za nje, chanel za kulipia kama za Kihindi, movies na series wanazo tafsiri etc.

3. Naunga hoja wanaohoji miaka 10 wana point, Kwa muono wangu hili deal linamungizia Hasara Azam kwa short term, no way Ligi yetu iwe na thamani hii.

DSTV analipa around Bilioni 500 kwa nchi takriban 46 za kusini mwa jangwa la sahara hii ni around 10B kwa kila Nchi. Kwamba ligi ya Tanzania ina thamani kuliko Epl?

Inaonekana Azam wame project kwa miaka 10 baadae Ligi yetu inaweza kuwa na thamani zaidi ya hii, hivyo mapema tu wamejipanga na kununua kabisa.

Ama kuna faida nyengine wa napata Toka serikalini kama Ruzuku.
Ndio maana ni muhimu kulinda uwekezaji wake kwa miaka 10,,kwamba pengine amefanya tathimini kwamba pengine baada ya kuonesha wamepata ujuaji mkubwa wa wateja sasa wameamua ku risk kwa mda mrefu ili kurudisha pesa zao
 
Wakuu nimedhamiriq Kupeleka Maoni yangu Wizara ya Michezo na Utamaduni, Kimsingi Nitaandika Maoni Yangu Kwa Wizara Husika Kuhusu Mkataba Wa Tff na Azam TV. Kesho Tu... Naombeni Mniunge Mkono
 
Hivi Ni Kosa Kutupa Mikataba Kama Sisi Wadau Tukasoma na Kutoa Maoni?
 
Tunaongelea Full Package 225 billion bila kuangalia hiyo miaka 10 yenyewe tutakuwa wapi katika Ramani ya Soka na Mtazamo wa Soka lenyewe kwa Mapana yake.
 
Back
Top Bottom