Azam Tv mnavyozidi kujitangaza msisahau kuongeza/maintain chaneli Bora kuwe na machaguo tofauti

Azam Tv mnavyozidi kujitangaza msisahau kuongeza/maintain chaneli Bora kuwe na machaguo tofauti

The Anfield

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2025
Posts
290
Reaction score
374
Mfano sasa ivi kwenye tamthlia/filamu mmeziondoa au kushindwa kuzibakisha chaneli za muvi za Kinaijeria za AMC chanel na AMC series, Wakati wenzenu DStv wanazo mpaka chanel za tamthlia/muvi za Wasauzi,Ghana na Kenya na za Lugha zao za makabila...
Hivyo kwenye muvi machaguo ni machache, mteja kama hupendi muvi za waturuki Azam One& two au za Wahindi starlife sijui Star Gold au za Waarabu MBC, inabidi ubaki kuangalia tu Sinema zetu kusapoti wasanii wetu wa kitanzania Ina maana italazimu ulipie kifurushi kidogo Cha elfu12 tu maana unalipia Cha Bei juu kiasi Cha Mpira cha elfu28 siku hakuna mechi Kali za Simba sijui Yanga na Al Ahly, Sijui Afcon au Real Madrid na Barcelona Kwenye La Liga unakosa kabisa Cha kuangalia Hela inakuwa kama inaenda Bure japo ni nafuu Bei zenu za vifurushi...
Kwenye chaneli za muziki pia, machaguo ni machache , Trace Mziki,MTV base nazo zimeyayuka, yamebaki machaneli meeengi ya Dini na Chaneli za Rwanda, Uganda na Kenya wakiongea vilugha vyao vya asili.. Naomba Kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom