Azam tv msirushe tamthilia yenye jina hili, mtakosea

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Unyanyapaa ni kosa sawa na makosa mengine, hasa likifanywa na taasisi

Wafanyakazi wa ndani ni kundi kubwa sana kwenye jamii zetu, ambao kazi zao ni muhimu sana. Kazi Yao inawaingizia kipato lakini pia inasababisha utulivu mkubwa maofisini miongoni mwa watumishi wenye watoto wadogo nyumbani kwakuwa ndio wanaoachiwa kazi zote za kulea watoto, usafi, upikaji chakula, kufanya manunuzi na hata ulinzi wa mali za mabosi wao. Watu hawa wanastahiki kuheshimiwa kama watu wengine.

Faida nyingine ya watumishi wa ndani ndio wanaotumia umeme nyumbani mchana kutwa kuangalia TV na video na kusikiliza radio nyakati za mchana (faida kwa tanesco na serikali) wakati mabosi wao wako kwenye majukumu yao ya siku.

Pia wafanyekazi hawa ni ndio wadau wakubwa wa channel ya Azam tv ya Sinema zetu, watanunua kifurushi japo Cha wiki ili waangalie Sinema zetu. Hivyo ni faida kwa Azam media.

Hoja Iko hapa: Nasikia kuwa Kuna tamthilia inayokwenda kwa jina la Beki 3 inaenda kuonyeshwa kwenye channel ya Simema zetu Azam tv. Kama ni kweli jina hili la "Beki tatu" halileti heshima kwa jamii hii ya watumishi wa ndani. Jina hili ni kejeli kwa watumishi wa ndani, hivyo sio vizuri kutumika kwenye TV kubwa kama Azam tv.
Napinga jina/title lakini sipingi mafundisho/ujumbe yaliyomo kwenye hiyo tamthilia.

Mimi nitakuwa wa kwanza kwenda mahakamani kuuliza tafsiri ya Beki tatu, na kama ni sawa hawa watu kuitwa Beki 3 na Azam tv, wasanii na wadau wengine au la!.

Heshima ni kitu Cha bure.

Nawasilisha.
 
Hebu fafanua zaidi kwa uelewa wako hilo jina beki 3 limetoka wapi na kwa nini likahusianishwa na wafanyakazi wa ndani na kisha fafanua sasa madhara yake ni yapi yaani sifa zinazobebwa na hilo jina beki 3 linamuathiri vipi huyo mfanyakazi wa ndani.

Je! Azam wametamka kuwa mfanyakazi wa ndani anaitwa beki 3 au wewe ndio umetafsiri hivyo? Halafu una uhakika kwenye hiyo tamthilia mfanyakazi wa ndani atakua akiitwa beki 3? Au atakua akiitwa kwa jina lake?
 
Azam sio watunzi.
 
Tutajua hukohuko mahakamani muda ukifika, usivuke daraja kabla hujalifikia. Hayo yote atayajibu mwandishi wa tamthilia. Beki tatu maana yake nini, kwani tamthilia inabeba jina hili.

Mahakama ndiyo itatoa majibu kuhusu uhalali au ubaya wa jina hili. Na wanawake wenyewe watasema kama ni sawa au sio sawa, na wafanyakazi wenyewe utaulizwa kama ni sawa au sio sawa.
 
Tuanze hapo kwenye beki tatu wewe unaelewa Nini..

Maana ya beki tatu ni ulinganifu wa mfanyakazi wa ndani na beki namba tatu wa mchezo wa mpira wa miguu kazi ya beki namba tatu kwenye mpira ni ulinzi wa na kuuza mashambulizi kwa team sasa vijana wamnyumbulisha hiyo maana akapewa pia mfanyakazi wa ndani ya nyuma ikimaanisha majukumu yake ni kama Yale wa beki namba 3 kwenye mchezo wa mpira wa miguu Kuhakikisha home pako salama wakati wote...

Sasa hapo shida ni Nini?
 
Kwahiyo mtu yeyoye anaebaki nyumbani kulinda nyumba na watoto hata kama ni mama yako mzazi anaitwa Beki 3?
 
Ukombozi wa mwanamke utaanzia hapa
 
Sio jina zuri. Hao watunzi wa hiyo tamthilia hawajachekecha vyema mbongo zao.

Hiyo ni kama vile baba zetu tunavowaita dingi, faza au mashua ukiwa kitaa lakini mkiwa nae unamwita baba na yeye anajua kua mwanangu ananiita baba.

Ndivo hivo hata kwa hao wadada, tukiwa kitaa na wana tunapiga story tunawaita beki 3 lakini sio vizuri yeye kuskia akiitwa ama kuskia watu wakimtambua kwa jina la ajabu namna hiyo. Dada wa nyumbani/Dada wa kazi au dada tu inatosha.
 
Familia hufananishwa na team ya mpira. Mama ni golikipa na baba always ni fowadi. Sasa kama mzee anaupiga mwingi, golikipa inabidi awe na beki 3 imara. Hapo ndipo mfanyakazi wa ndani anapojizolea umaarufu anapohakikisha golikipa hapati madhara. Ndio tukampa jina la beki 3 kwa umahiri wake. Nadhani mafowadi mmenielewa zaidi na sioni dharau kwenye hilo jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…