Azam tv msirushe tamthilia yenye jina hili, mtakosea

Azam tv msirushe tamthilia yenye jina hili, mtakosea

Movie za kutafsiriwa zinapoteza uhalisia wa movie.
Utaona km una enjoy lkn huwezi kujua mtiririko wa matukio kulingana na wahusika wanavyopanga.
Mtafsiri alikuwa marehemu lufufi tu,hizi mbuzi zingine zinakera masikio ti
 
Tuanze hapo kwenye beki tatu wewe unaelewa Nini..

Maana ya beki tatu ni ulinganifu wa mfanyakazi wa ndani na beki namba tatu wa mchezo wa mpira wa miguu kazi ya beki namba tatu kwenye mpira ni ulinzi wa na kuuza mashambulizi kwa team sasa vijana wamnyumbulisha hiyo maana akapewa pia mfanyakazi wa ndani ya nyuma ikimaanisha majukumu yake ni kama Yale wa beki namba 3 kwenye mchezo wa mpira wa miguu Kuhakikisha home pako salama wakati wote
 
Usikute hii tamthilia ya beki 3 ndio itakua tamthilia pendwa ya wadada wa kazi, yaani binti anajitahidi kufanya kazi zake fastafasta ili asipitwe kuangalia uhondo wa beki3.
Lile tangazo la hiyo tamthilia huwa nakutana nalo kwenye channel za mpira na ertugul, dada wa kazi akiliona anaondoka kabla halijachanganya kwa kuzuga kama anakwenda kupokea simu au kuna dharura fulani, hapendi kuliona kukiwa na watu wengine. Ndio nikapata maono ya kuandika huu uzi. Sio kweli akina dada wataipenda, huenda wataipenda kama itaanza kuonyeshwa saa 3 asubuhi wakati mabosi wake wameenda kazini na watoto wako shuleni hawapo nyumbani siku za kazi.
 
kwan isidingo ilkua inamaana gan au ilkua inamhusu nan katika miaka yote ya kuonyeshwa kwake? iko hiv mwandsh anapotoa jina halileng moja kwa moja iko unachokiwaza kwamfno ndan ya iyo bek 3 kutakua na watu wa maoficn ugomvi ma kazni ndoa kuvunjika mafumaniz madanguro nk kwann ww umgaid mtunz kwa uelewa wako tu?
Wewe unapotosha, sikiliza tangazo linasema nini kuhusu hiyo tamthilia, wanaongelea categorically mfanyakazi wa ndani, nakwambia huyo mtunzi na Azam tv kama wanazo hela za bure hebu walirushe hewani.
 
Lile tangazo la hiyo tamthilia huwa nakutana nalo kwenye channel za mpira na ertugul, dada wa kazi akiliona anaondoka kabla halijachanganya kwa kuzuga kama anakwenda kupokea simu au kuna dharura fulani, hapendi kuliona kukiwa na watu wengine. Ndio nikapata maono ya kuandika huu uzi. Sio kweli akina dada wataipenda, huenda wataipenda kama itaanza kuonyeshwa saa 3 asubuhi wakati mabosi wake wameenda kazini na watoto wako shuleni hawapo nyumbani siku za kazi.
Nimekuelewa mkuu na kwa upande mmoja imenigusa kuona hata huyo dada wa kazi anakwazika kwa namna fulani.
Kama hio tamthilia ina dalili za udhalilishaji ni bora azam tv watumie busara kwa kusitisha kuionyesha.
 
Guys kama kuna mtu anahitaji king'amuzi complete/full kit cha AZAM cha DISH ambacho ni kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa chaneli zote kwa miezi mitatu. naomba anicheki DM tufanye biashara, kinapatikana kwa 165k (non-negotiable price)
 
Unyanyapaa ni kosa sawa na makosa mengine, hasa likifanywa na taasisi

Wafanyakazi wa ndani ni kundi kubwa sana kwenye jamii zetu, ambao kazi zao ni muhimu sana. Kazi Yao inawaingizia kipato lakini pia inasababisha utulivu mkubwa maofisini miongoni mwa watumishi wenye watoto wadogo nyumbani kwakuwa ndio wanaoachiwa kazi zote za kulea watoto, usafi, upikaji chakula, kufanya manunuzi na hata ulinzi wa mali za mabosi wao. Watu hawa wanastahiki kuheshimiwa kama watu wengine.

Faida nyingine ya watumishi wa ndani ndio wanaotumia umeme nyumbani mchana kutwa kuangalia TV na video na kusikiliza radio nyakati za mchana (faida kwa tanesco na serikali) wakati mabosi wao wako kwenye majukumu yao ya siku.

Pia wafanyekazi hawa ni ndio wadau wakubwa wa channel ya Azam tv ya Sinema zetu, watanunua kifurushi japo Cha wiki ili waangalie Sinema zetu. Hivyo ni faida kwa Azam media.

Hoja Iko hapa: Nasikia kuwa Kuna tamthilia inayokwenda kwa jina la Beki 3 inaenda kuonyeshwa kwenye channel ya Simema zetu Azam tv. Kama ni kweli jina hili la "Beki tatu" halileti heshima kwa jamii hii ya watumishi wa ndani. Jina hili ni kejeli kwa watumishi wa ndani, hivyo sio vizuri kutumika kwenye TV kubwa kama Azam tv.
Napinga jina/title lakini sipingi mafundisho/ujumbe yaliyomo kwenye hiyo tamthilia.

Mimi nitakuwa wa kwanza kwenda mahakamani kuuliza tafsiri ya Beki tatu, na kama ni sawa hawa watu kuitwa Beki 3 na Azam tv, wasanii na wadau wengine au la!.

Heshima ni kitu Cha bure.

Nawasilisha.
Umekurupuka mzee.Tamthiliya ni sanaa na maudhui yake yanaweza kuwa na tafsiri tofauti katika hadhira tofauti, na inaposababisha mjadala mkubwa, ndiyo kiashiria kuwa ujumbe uliokusudiwa umefika umefikishwa!
 
au kama kuna mtu ana king'amuzi cha STARTIMES cha DISH nimpe cha AZAM cha DISH ambacho bado kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa miezi mitatu but ataniongeza 60k
 
au kama kuna mtu ana king'amuzi cha STARTIMES cha DISH nimpe cha AZAM cha DISH ambacho bado kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa miezi mitatu but ataniongeza 60k
Uko wapi nikuuzie, maana ninavyo vyote cha Azam na cha Startimes
 
Faida nyingine ya watumishi wa ndani ndio wanaotumia umeme nyumbani mchana kutwa kuangalia TV na video na kusikiliza radio nyakati za mchana (faida kwa tanesco na serikali) wakati mabosi wao wako kwenye majukumu yao ya siku.

Pia wafanyekazi hawa ni ndio wadau wakubwa wa channel ya Azam tv ya Sinema zetu, watanunua kifurushi japo Cha wiki ili waangalie Sinema zetu. Hivyo ni faida kwa Azam media.

Wafanyakazi wa ndani huwa cna mazoeanao,,kazi kazi,,hakuja kuangalia tv wala kuckiliza redio wala kuangalia cinema. Ataangalia baada ya kazi.
 
Back
Top Bottom