Azam tv msirushe tamthilia yenye jina hili, mtakosea

Movie za kutafsiriwa zinapoteza uhalisia wa movie.
Utaona km una enjoy lkn huwezi kujua mtiririko wa matukio kulingana na wahusika wanavyopanga.
Mtafsiri alikuwa marehemu lufufi tu,hizi mbuzi zingine zinakera masikio ti
 
 
Usikute hii tamthilia ya beki 3 ndio itakua tamthilia pendwa ya wadada wa kazi, yaani binti anajitahidi kufanya kazi zake fastafasta ili asipitwe kuangalia uhondo wa beki3.
Lile tangazo la hiyo tamthilia huwa nakutana nalo kwenye channel za mpira na ertugul, dada wa kazi akiliona anaondoka kabla halijachanganya kwa kuzuga kama anakwenda kupokea simu au kuna dharura fulani, hapendi kuliona kukiwa na watu wengine. Ndio nikapata maono ya kuandika huu uzi. Sio kweli akina dada wataipenda, huenda wataipenda kama itaanza kuonyeshwa saa 3 asubuhi wakati mabosi wake wameenda kazini na watoto wako shuleni hawapo nyumbani siku za kazi.
 
Wewe unapotosha, sikiliza tangazo linasema nini kuhusu hiyo tamthilia, wanaongelea categorically mfanyakazi wa ndani, nakwambia huyo mtunzi na Azam tv kama wanazo hela za bure hebu walirushe hewani.
 
Nimekuelewa mkuu na kwa upande mmoja imenigusa kuona hata huyo dada wa kazi anakwazika kwa namna fulani.
Kama hio tamthilia ina dalili za udhalilishaji ni bora azam tv watumie busara kwa kusitisha kuionyesha.
 
Guys kama kuna mtu anahitaji king'amuzi complete/full kit cha AZAM cha DISH ambacho ni kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa chaneli zote kwa miezi mitatu. naomba anicheki DM tufanye biashara, kinapatikana kwa 165k (non-negotiable price)
 
Umekurupuka mzee.Tamthiliya ni sanaa na maudhui yake yanaweza kuwa na tafsiri tofauti katika hadhira tofauti, na inaposababisha mjadala mkubwa, ndiyo kiashiria kuwa ujumbe uliokusudiwa umefika umefikishwa!
 
au kama kuna mtu ana king'amuzi cha STARTIMES cha DISH nimpe cha AZAM cha DISH ambacho bado kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa miezi mitatu but ataniongeza 60k
 
au kama kuna mtu ana king'amuzi cha STARTIMES cha DISH nimpe cha AZAM cha DISH ambacho bado kipya kabisa hakijamaliza hata mwezi na kimeshalipiwa miezi mitatu but ataniongeza 60k
Uko wapi nikuuzie, maana ninavyo vyote cha Azam na cha Startimes
 

Wafanyakazi wa ndani huwa cna mazoeanao,,kazi kazi,,hakuja kuangalia tv wala kuckiliza redio wala kuangalia cinema. Ataangalia baada ya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…