Azam TV yaongeza channel mpya Azam Sports 5 HD

Azam TV yaongeza channel mpya Azam Sports 5 HD

online GOVT applications

Senior Member
Joined
Sep 7, 2026
Posts
185
Reaction score
182
Kampuni kubwa ya media East Africa Azam media wameongeza channel mpya ya mpira ya Azam sports 5 HD na kufanya wawe na jumla ya channel 10.

Katika hizo channel 10, tisa ni HD na moja ni ya matangazo, hii inafanya iwe ni kampuni kubwa inayomilikiwa na wazawa Afrika nzima

Haya ni mapinduzi makubwa mno katika sekta ya habari, Na tunaomba na kampuni nyingne ziige huu uwekezaji wa Azam

Kwa taarifa za ndani haya ni maandalizi kwaajiri ya kuonesha mechi za EPL mwakani 2027/2028 au 2028/29 na vilevile UEFA champions league na Europa na conference league miaka ya mbele

Hongera kwao
 
Ving'amuzi havina maana siku hizi. Una installation app kwenye laptop, una subscribe kwa elfu 45 kwa mwezi, una connect TV kupitia HDMI unaangalia ligi yoyote duniani
 
Ving'amuzi havina maana siku hizi. Una installation app kwenye laptop, una subscribe kwa elfu 45 kwa mwezi, una connect TV kupitia HDMI unaangalia ligi yoyote duniani
Na gharama za internet? Halafu jumlisha na hiyo 45k si utakua unatumia 120k+ kwenye tv kwa mwezi!!! Asilimia 98 ya watanzania hawamudu hili na hao ndo target ya azam media


Mwisho Katika kaya zaidi ya milion 40 Tanzania kaya zinazomiliki laptop na tv kwa pamoja hazifiki 39.9m
 
Ving'amuzi havina maana siku hizi. Una installation app kwenye laptop, una subscribe kwa elfu 45 kwa mwezi, una connect TV kupitia HDMI unaangalia ligi yoyote duniani
nakuunga mkono na wakati huohuo nakupinga vikali.

wakti wewe unasema unalipia elfu 45 kwa mwezi kuna wengine wasema mchawi bando tu.

hata mimi nikiwa mdau wa hizi sstreaming, swali je streaming hizi tunazofanya za bure zitadumu ikiwa wenye channel, kina azam , supersport, fox, skyspor, canal, espn na wengineo wakifiklisika?

tuzitakie mema kampuni za ving'amuzi na official online streaming zifanye vyema, zikiteteleka hata sisi burudani itaanguka
 
Ving'amuzi havina maana siku hizi. Una installation app kwenye laptop, una subscribe kwa elfu 45 kwa mwezi, una connect TV kupitia HDMI unaangalia ligi yoyote duniani
Ukitaka kuamini King'amuzi ni King'amuzi angalizia hiyo stream yako karibu na wanaocheki kwa TV. Wanaanza wao kushangilia sekunde 10 baadae unafata wewe.

Ni sawa ukae na mtu anayesikiliza mpira kwa redio. Dunia ya sasa watu wanataka vitu in realtime hizo IPTV ni nyongeza tu.
 
Vifurushi vita duplicate bei jiandaeni kwa ilo kama EPL n UCL zitaoneshwa
 
Back
Top Bottom