Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Sawa Azam walishika nafasi ya pili sisi tukaumia sana lakini tukumbuke sisi tulijiumiza wenyewe, sisi hatukuwa watu wa kushika nafasi ya pili, hata sasa hivi tunakwenda vizuri lakini mbeleni huko tutakorofisha tena mtani abebe ndoo na Injinia kashasema Simba haimnyimi usingizi, anajua anachokifanya ndani ya timu yetu, yaani Yanga kumfunga Simba ni sure bet kwenye kamari sasa hivi.
Azam wana timu nzuri, wana wachezaji wazuri na jana kaondolewa kwenye michuano, mimi kwa maoni yangu haikufungwa Azam, imefungwa nchi, aibu ni ya nchi, viongozi wakuu wa nchi wanaweza kuwa wanatambiana kuwa Rwanda ana timu nzuri kuliko Tanzania, ndio ukweli wenyewe.
Azam kuondoshwa kwenye michuano ya mabingwa hatua za awali kabisa ni msiba ndugu zangu watanzania, sio jambo la kuleta utani, matusi, au kujiona mjanja kuwadhalilisha viongozi wao na wachezaji, mimi naheshimu sana uhuru wa kutoa maoni lakini tunapoiombea mabaya Azam aondolewe kwenye level ya kimataifa wewe kama mtanzania unaona ni sawa kweli?
Haya mambo lazima tuyaangalie vizuri, humu ndani tupambane na kutaniana wenyewe kwa wenyewe lakini utani hadi tunapokwenda kupambana na nchi nyingine, kweli? Mbona jana hatukuona timu za Rwanda zikishangilia Azam? Hatukuiona Rayon wala Polisi jana, mashabiki wote waliungana kuwa kitu kimoja kuisapoti APR ambayo kiukweli imedhamiria kufanya vizuri ingawa kwa namna walivyocheza jana hawana timu nzuri bado, jana dakika za mwishooooni Jibril Sylla alikuwa awalize warundi wale lakini bahati haikuwa kwetu watanzania.
Tuache habari hizi za kijinga jinga, tushauriane kwenye level za kimataifa tufanye nini kwa sababu mwisho wa siku inatajwa Tanzania, sio Azam.Huu ni ujinga, ulofa, upumbavu sana.