Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Nimecheka sana leo, semaji la Azam Hashim Ibwe akiwa hana aibu wala haya ameonekana akiuelezea mchezo wa kirafiki baina ya Azam vs Stade Tunis huko Tunisia.
Alianza vizuri kwa kusema kuwa walipigwa bao la kwanza, wakapigwa la pili, wakapigwa la 3, Dube akachomoa kimoja.Waarabu wakapata penati ili wawachomeke Azam la 4, kocha wa Azam akawatoa wachezaji nje akidai refa alikuwa akipendelea.
Waarabu walipewa penati 2, penati ya 2 Azam wakatoa timu.
Mchezo umevunjika dakika ya 60 baada ya kuona mabao yanaweza kufika 5, sasa najiuliza ikiwa kama hali ndio hiyo mtaweza kweli msimu ujao mkikutana na akina Asukile?
Mna wachezaji wazuri lakini mipango hamna.