Nimecheka sana leo, semaji la Azam Hashim Ibwe akiwa hana aibu wala haya ameonekana akiuelezea mchezo wa kirafiki baina ya Azam vs Stade Tunis huko Tunisia.
Alianza vizuri kwa kusema kuwa walipigwa bao la kwanza, wakapigwa la pili, wakapigwa la 3, Dube akachomoa kimoja.Waarabu wakapata penati ili wawachomeke Azam la 4, kocha wa Azam akawatoa wachezaji nje akidai refa alikuwa akipendelea.
Waarabu walipewa penati 2, penati ya 2 Azam wakatoa timu.
Mchezo umevunjika dakika ya 60 baada ya kuona mabao yanaweza kufika 5, sasa najiuliza ikiwa kama hali ndio hiyo mtaweza kweli msimu ujao mkikutana na akina Asukile?
Siku ile walioofungwa na Esperence walisema "kufungwa sio kitu muhimu kwenye hii mechi."
"Kuna kitu kocha anakiangalia hivyo malengo yoa ore season sio ushindi."
"Tunacheza ili kujua eneo gani ni bora ili tuwekeze nguvu kulifanya liendelee kuwa bora na eneo gani ni dhaifu ili tuweke nguvu kulifanya liwe bora"
Sasa leo anaposema walikataliwa goli lao ndio anaponiacha njia panda. Ina maana round hii ushindi umekuwa muhimu?
Kwanini wasicheze tu wakijua kuwa ni goli hata kama refa amekataa kwasababu malengo sio kufunga bali kuangalia eneo gani ni bora walilonde lisipotee na eneo gani ni dhaifu walifanyie maboresho.
NB: Ila hoja ya mchezaji kuvunjwa mkono kams ni kweli basi inaweza kutoa reflection halisi kuwa haukuwa mchezo wa kistaarabu
Aloooooooooooo.
tatizo la azam wana ntantalila nyingi kwe mpira wa uwanjani.
simba na yanga wana tantalila nje ya uwanja ndo maana wakiingia dimbani ni kazkaz na ndio maana wanafanya vizuri kimataifa.
azam wabadilike la sihivyo wataendelea kuwa wasindikizaji tu na asipoangalia hata kina singida watamuacha mbali.
Nimecheka sana leo, semaji la Azam Hashim Ibwe akiwa hana aibu wala haya ameonekana akiuelezea mchezo wa kirafiki baina ya Azam vs Stade Tunis huko Tunisia.
Alianza vizuri kwa kusema kuwa walipigwa bao la kwanza, wakapigwa la pili, wakapigwa la 3, Dube akachomoa kimoja.Waarabu wakapata penati ili wawachomeke Azam la 4, kocha wa Azam akawatoa wachezaji nje akidai refa alikuwa akipendelea.
Waarabu walipewa penati 2, penati ya 2 Azam wakatoa timu.
Mchezo umevunjika dakika ya 60 baada ya kuona mabao yanaweza kufika 5, sasa najiuliza ikiwa kama hali ndio hiyo mtaweza kweli msimu ujao mkikutana na akina Asukile?
Azam mmefanya Jambo jema Sana. Mmetukumbusha wakati tunacheza Chandimu timu ya mwenye mpira imifungwa anachukua mpira wake na Mechi inaishia hapo hapo.