#COVID19 Azim Dewji amvaa Gwajima sakata la chanjo, amwambia ana akili ya kuhubiri siyo Sayansi

Gwajima yeye anachokataa ni hiari yenye ulazima kwa baadhi ya makundi ya watu,anataka kama chanjo ni hiyari iwe hiyari kwa kila mtu sio hiyari kwa machinga anetembea km 49 kwa siku Ila lazima kwa mwanajeshi anayeshindia kambini

Ila uzuri kawatahadharisha majeda kuwa wakilegea watachanjwa na kuwa mdebedo kama kina James delicious
 
Unaweza kuta ni mkakati wa kuzima kelele za tozo na kuhusu mbowe,kwa sasa habari imekua gwajima tozo zinaendelea kama kawaida,mbowe yupo lupango kama kawaida,chezea siasa wewe nakumbuka wakati nipo shule ya msingi enzi hizo,kulikua na soma linaitwa siasa.

Mwalimu wa somo akingia dalasani akaanza kufundisha, mwisho akasema kama kuna mwenye swali aulize,mm nikanyosha mkono nikamuuliza,siasa nini akajibu kwa halaka tu,siasa ni uongo ulio komaa, ukikua utajua zaidi, na kweri nimejua zaidi kwa sasa.
 
Baki nae hadi siku atakapo mfufua mama yake Kama alivyodai
Gwajima ana utaalamumu gani wa bailogia na kemia achilia mbali viriology ?
Nyie subirini hekaya zake Kama hutaki chanjo nani kakulazimisha?
Achana na habari ya utalamu tupa kule inawezakuwa na wewe ni mbumbumbu tu.Ni mwananchi ana haki yake kikatiba kutoa maoni.Em jibu hoja kwa hoja kama huna kaa kimya.Siyo utoe maneno ya vitisho ukafikiri kila mtu analala sebleni kwa shemeji kama wewe.
 
Sasa ndio aende kuuliza kanisani? Mbona majibu ya hayo maswali yapo na ni mepesi tu
 
Ilitakiwa kwanza Selikali iitishe kura ya maoni kwa Watanzania wote wangapi wanataka Chanjo na wangapi hawataki na kule zipigwe Hadharani na kuoneshwa live.. 80% ya watz kuanzia miaka 18+ wasingekubali huu upuuzi.
 
Gwajima sio mtumishi wa Mungu.
Mtumishi wa kweli wa Mungu hawezi kuungana na watesaji watu, wakandamizaji na wauwaji. Angekuwa mkweli asinge ungana na mwendazake wala kupokea ubunge wa kupora.
Sifa hizi zinafanya aondolewe kabisa kwenye orodha ya wanao weza kuwa watumishi wa Mungu.
 
Nadhani sifa ya UNAFIKI inatakiwa kuingizwa kama moja ya tabia za Watanzania; simuungi mkono Gwajima lakini pia sitaki kumlaumu Gwajima. Tuweni wakweli, hivi hayati rais wa awamu ya TANO hakuzungumza kitu kinacho fanana na hiki? Wanaweza kua wametumia maneno tofauti but mtazamo wao utabakia kua sawa tu, sina hakika Azim Dewji ni msomi wa kitu gani ( i think ni masomo ya biashara ) but remember marehemu Magufuli alikua ni mwana sayansi, mengi ya maneno yake kuhusu corona yana ishi hadi leo so kumkaripia Gwajima ilihali ni miezi michache tu (hata miezi 6 haijapita ) kiongozi mkubwa wa nchi alisema the same thing ni kuonesha kiwango kikubwa sana cha UNAFIKI. Tukumbuke, yapo maandishi hadi ya kina Hamisi Kigwangala mitandaoni kuhusu chanjo, Hamisi ni daktari wa magonjwa ya binadamu, Hamisi anajua zaidi mambo ya afya kuliko Azim Dewji. Sina maana kama nampinga kaka Azim na wala sina maana kwamba naungana mkono na askofu Gwajima ila nashangaa hu ukali unaosemwa sasa hivi as if hi kitu ndio kwanza tunaisikia wakati sio kweli. Hayo ni yale yaliotokea nchini mwetu, huko nje je? Ni kweli na wenyewe wapo tu kimya???? Hatusomi? Hatuoni??? Bado serikali yetu imesema suala la chanjo ni la HIYARI, hivi ndui, pepopunda na vyenyewe kwanini havikufanywa kua vya HIYARI badala yake watoto/wajukuu zetu hua ni lazima wachanjwe? Hapa yapo maswali, serikali iseme ukweli, something is wrong here.
 
Azim Dewji anahaki na yeye kuelezea kuhusu chanjo na manufaa yake.
Muache gwajima aeleze kwa anachokijuwa ubaya wachanjo.

Watanzania watapima na kumfuata aliyebora au sahihi.
 
Maana nadungwa chanjo na kuwa zombi, alafu navaa mabarakoa kuninywima hela.mashetani hawataki tuvute hewa safi. Yatanilipa shilling ngapi kuvaa sindilia usoni.wasifanyie biashara kwenye afya zetu.sisi hatutaki mabarakoa wala chanjo feki
 

Mwambieni sio lazima wataalamu wa huku Afrika wakawa huru kuongea kitaalamu.

Atuambie kama chanjo au surua zingekuwa zinaambukiza wale wadio chanjwa kungekuwa na mtu kabaki hapa duniani. Ajibu hoja zilizo ibuliwa ndio wstu wsnataka kusikia.

Asijiangalie yeye na uwezo wake wa kifedha. Ajiulize Mtanzania aliye Mwanakwerekwe wa maisha ya hali ya chini anasaidiwa vipi akipata side effects ya chanjo ya corona. Tunayo mitungi ya gesi ya oksijeni ya kutosha kwenye zile zahanati 400 na ushee tulizojengewa na JPM chini ya usimamizi mahiri wa Jaffo?
 
Dah...natamani sana kuskia Gwajima atakavo jibu. Ingekua kipindi cha Magu angemjibu shombo vibaya mno🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…