Ukweli usemwe mashabiku wa soka Bongo wengi ni vilaza.
Mwingine ananiambia pale Camara bora angedaka ingekua penati na angepewa kadi ya njano. Namuambia sio kweli pale angekua amewanyima Fountaine Gate nafasi ya kupata goli hivyo angepewa kadi nyekundu na ingepigwa faulo ndogo ndani ya box.
Ananiambia hakuna faulo ndani ya box, hiyo ni penalty. Imagine mtu ana miaka zaidi ya 35 hajui kama kuna indirect freekick, kweli?
Ukitoa Simba na Yanga mashabiki wa Bongo vichwani weupe hadi sio poa. Huyo Chasambi atapata shida kwasababu yupo kwenye nchi ambayo watu hawajui chochote kuhusu mpira.